Tafuta

Mwezi wa Kimisionari Oktoba 2020 Mwezi wa Kimisionari Oktoba 2020 

Uganda:Kutangaza Injili ni zawadi ya kushirikishana!

Kutangaza Injili ni zawadi ya kishirikshana.Kama wakristo,wafuasi wa Yesu,mtindo wetu wa maisha lazima uangazie imani yetu,tujiulize kwa kina sisi ni nani na kwa nini tunaishi.Hatuko peke yetu.Kristo ni msikilizaji wa kimya kwa kila uongofu na anabisha hodi katika mioyo yetu kwa kusubiri aweze kufunguliwa ili aingie na kuishi.Ni maneno ya Padre Kaweesa Mkurugenzi wa PMS katika kukaribisha mwezi wa Kimisionari.

Katika harakati za maandalizi ya Mwezi wa Kimisionari ulimwenguni, Oktoba 2020, Padre Pontian Kaweesa, Mkurugenzi wa Shughuli za Kipapa za Kimisionari (PMS) nchini Uganda amezungumzia juu ya maandalizi yanayofanywa na Kanisa mahalia kwamba: “Kutangaza Injili ni zawadi ya kishirikshana”. “Kama wakristo, wafuasi wa Yesu, mtindo wetu wa maisha lazima uangazie imani yetu, tujiulize kwa kina sisi ni nani na kwa nini tunaishi. Hatuko peke yetu. Kristo ni msikilizaji wa kimya kwa kila uongofu na anabisha hodi katika mioyo yetu kwa kusubiri aweze kufunguliwa ili aingie na kuishi nasi”, amesema Padre Kaweesa.

Shughuli za Kipapa za Kimisionari (PMS) nchini Uganda zinasindikiza waamini kuishi na kukua kama ndugu, kaka na dada ambao lazima waendelee kujua wema, huruma na upendo wa Mungu. Wiki iliyopita anaripoti Padre Pontian kuwa serikali ya Uganda imefungua shughuli za kiliturujia ambazo baada ya miezi saba hivi ilikuwa imekatazwa mikusanyiko ya Ibada kutokana na Janga la COVID-19. Idadi ya waamii washiriki kwa kila adhimisho la Misa hawapaswi kuzidi watu 70. Kwa mujibu wa  Mkurugenzi wa kitaifa wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari( PMS) amesema, “tumewahamasisha wabatizwa wote kusali pamoja katika familia zao na hivyo Kanisa kuendelea na kazi yake ya uinjlilishaji wa familia.

Neno la Mungu limetangazwa na Makatekista, na waamini walei wanaotimiza wajibu wao vyema na Makasisi ambao wameendelea kuwatembelea familia na Jumuiya ndogondogo za kikristo na kuwahudumia kwa kuwapatia sakramenti za ubatizo, Ekaristi Takatifu na Ndoa Takatifu. Kwa kujivunia  katika umoja na Baba Mtakatifu, Padre Kaweesa amesema, wamevuka salama kipindi hiki cha janga la Corona huku wakiwasaidia wagonjwa na jamii zilizoathirika. Madhara makubwa yaliyoletwa na janga hili ni kuharibika kwa uchumi huku familia nyingi zikikosa uwezo wa kujikimu kimatibabu.

Hata hivyo, kwa ufafanuzi zaidi amesema kuwa huduma nyingi zimeweza kutolewa na waamini wa Kanisa Katoliki wa Uganda na pia wakibuni mbinu mbalimbali za kuandaa siku ya kimisionari duniani mwaka 2020. Padre Pontian vile vile ameelezea kwamba wameandaa mikakati inayowasilisha utume wa kimisionari wa Kanisa zima na Kanisa mahalia utakaotangazwa kwa njia ya televisheni ya kikatoliki Uganda (UC TV) na matangazo mbashara kupitia Radio Maria ili kuzungumzia utume wa kimisionari katika nyakati hizi za janga la COVD-19.  

Kwa upande wa habari za kimataifa, wamewaomba Maaskofu kuridhia pendekezo la kufungua akaunti ambapo waamini watawekeza fedha na mbinu nyingine za kifedha. Wakurugenzi wa PMS wamewaandikia Maaskofu wa Majimbo (POM) ili kuwaomba waamini waendelee kuombea umisionari wa Kanisa na kufanya Novena kabla ya maadhimisho ya siku ya Misioni duniani wakiongozwa na kauli mbiu “tazama mimi hapa nitume” (Is 6:8) iliyosambazwa katika mitandao. “sasa ni wakati wa kuipeleka Injili mbele” amehitimisha Padre Kaweesa huku akisisitiza kuwa kila zawadi ni vema ikashirikishwa kwa wengine.

29 September 2020, 12:15