Tafuta

Vatican News
Kwa mujibu wa Pax Christo wanasema ubaguzi wa rangi unapenya kila hali ya maisha nchini Marekani na kwamna kuna ugaidi ambao unaendelea kutishia na kuua watu weusi Kwa mujibu wa Pax Christo wanasema ubaguzi wa rangi unapenya kila hali ya maisha nchini Marekani na kwamna kuna ugaidi ambao unaendelea kutishia na kuua watu weusi   (2020 Getty Images)

Uchaguzi Marekani:Uthibitisho wa misingi ya Pax Christi!

Katika Waraka wa Pax Christ chama cha harakati katoliki kwa ajili ya amani nchini Marekani unaangazia imani ya kina kupitia ujumbe wa Injili ya Yesu unaotukumbusha kuwa msingi kwa kila uamuzi tunaofanya ni jukumu letu kumpenda Mungu kupitia upendo kwa jirani, wa mbali na kuwa na upendeleo kwa maskini.Pili kutumia Mafundisho Jamii Katoliki inayoongoza jamii kujikita katika matendo ya Injili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Pax Christi nchini Marekani imetangaza tarehe 16 Septemba katika ukurasa wa tovuti yao Azimio lao   katika fursa ya uchaguzi  utakaofanyika nchini Marekani mwaka huu, ili kusaidia wajumbe wote, washirika na watu wote kuwa na dhamiri ya kufanya uamuzi wa nguvu ambao utawagusa idadi kubwa ya watu wa Marekani na ulimwengu wote na kuchagua viongozi wenye maadili, tabia na uadilifu unaohitajika kuhudumia jamuiya.

Katika Waraka wa  Pax Christi nchini Marekani ambacho ni chama cha harakati katoliki kwa ajili ya amani  unaangazia awali ya yote imani ya kina kupitia ujumbe wa Injili ya Yesu unaotukumbusha kuwa “msingi kwa kila uamuzi tunaofanya ni jukumu letu kumpenda Mungu kupitia upendo kwa jirani, wa karibu na wa mbali na kuwa na upendeleo hasa kwa masikini; pili, kutoka katika misingi ya  mabadiliko ya Mafundisho Jamii Katoliki, iliyoundwa kwa ajili ya kutuongoza katika kutumia ujumbe wa Injili kwa maisha yetu ya pamoja kama watu wamoja, ndani na nje ya mipaka ya leo”.

Katika kujitoa kwake kufuata nyayo na mfano wa Yesu, Pax Christi Marekani katika waraka huo, wanaheshimu, kwanza,  shukrani ardhi na mito na watu wa asilia, wa zamani na wa sasa, ambao wamesimamia Kisiwa cha Kobe, eneo ambalo linajumuisha kile kinachojulikana kama Mataifa ya Marekani na inatambua kwamba eneo kubwa la Marekani halijapewa dhamana na kwamba Watu wa Asili wanaendelea kutofurahia na wala kutambuliwa na serikali. Kwa maana hiyo chombo hiki kinasisitiza vitendo vya kudharaulika vya biashara ya watumwa kupitia Atlantiki ambayo ilifungua njia za ubaguzi wa rangi dhidi ya weusi na anajuta kuhusu jukumu la taasisi ya Kanisa Katoliki katika mchakato wa ukoloni na ujumuishaji wake kwenye dhambi za ubaguzi wa rangi, utumwa na kutengwa.

Ubaguzi wa rangi unapenya kila hali ya maisha nchini Marekani kwa mujibu wa taarifa hiyo huku   wakieleza kwamba unapanda ugaidi ambao unaendelea kutishia na kuua watu weusi, kuendeleza kutukuza wazungu na kuacha ubinadamu wote umeharibika. Kwa kukabiliwa na ukweli huu, vuguvugu la wanaharakati Wakatoliki linathibitisha kwamba maisha ya weusi yanahesabiwa na kwamba vurugu zilizomo katika ubaguzi wa kimfumo ni dharau kwa Mungu anayeumba, anakomboa na kutakasa wote na kutuita pamoja kama familia moja. Kwa njia hiyo inaunga mkono kuhusu fidia kwa mateso yaliyowakumba weusi kwa sababu ya utumwa, kwa sheria za Jim Crow na wafungwa wengi wanaolengwa, kama ilivyo pia kusaidia kikamilifu haki ya watu kuhama na kutafuta kimbilio, uraia na haki, ya watu kutohama na kuishi katika hali salama katika jamuiya zao za asili”.

Hatimaye  katika wakati ambapo mabadiliko ya hali ya hewa hayalazimishi watu katika nchi maskini   tu na zenye shida kuhama, lakini pia kuchochea umaskini, ukosefu wa chakula, makazi yao na vurugu katika jumuiya zinazozunguka Marekani, Chombo hiki kinalitaka taifa hilo kutoa tamko wazi la mgogoro wa hali ya hewa kuwa dharura ya kitaifa, kwa kutumia Mkataba wa Paris, ili kuimarisha Sheria ya Hewa Safi, kuwekeza katika vyanzo vya nishati safi na kutafuta njia ya kimataifa ya haki, kama ilivyoonyeshwa katika Mpango Mpya wa Kijani wa Marekani. Jitihada za harakati za Pax Christi Marekani (USA), katika chaguzi hizi, kwa kuongozwa na hali ya kiroho ya kutokutumia nguvu, ya historia yao wajenzi wa amani na jitihada za kufanya kazi kwa ajili ya haki hiyo ambayo inathibitisha utu wa wanadamu wote, mmoja mmoja na kwa pamoja na kuhakikisha amani kwa viumbe vyote”.

17 September 2020, 16:40