Tafuta

Vatican News
2020.08.27 Huduma ya Sakramenti nchini Brazil 2020.08.27 Huduma ya Sakramenti nchini Brazil 

Togo:Ask.Mkuu-Kuhani tetea wanaokandamizwa &dumisha haki!

Mapadre watetee wanaokandamizwa na kudumisha haki.Siyo makuhani wakati wanapovaa nguo kuadhimisha Ekaristi,baadaye watu wa kawaida kwa nguo za kiraia.Kinyume makuhani watambue wao ni makuhani kwa sababu ukuhani hautengenishwi nao.Huduma yao ni ya wakati wote,haiwezi kupunguzwa kuwa riziki au jukumu la kazi,au kutimizwa muda mfupi kana kwamba ni hali fulani za maisha yasiyomgusa.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Askofu Mkuu Nicodème Anani Barrigah, wa jimbo kuu katoliki la Lomé, nchini Togo hivi karibuni tarehe 8 Septemba 2020 wakati wa mahubiri yake kwenye misa ya kutoa Sakramanti ya Kipaimara amewageukia mapadre kwa kuwashauri watetee wanaokandamizwa na kudumisha haki. Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari la ACI-Afrika linabainisha kuwa Maadhimisho ya Kipaimara yalikuwa yafanyike kunako tarehe 9 Aprili 2020 kama jinsi ambavyo huwa ni kipindi karibu ulimwengu mzima kwa kutoa sakramenti ya Kipaimara na ambavyo iliharishwa kwa sababu ya janga la ugonjwa wa Corona.

Katika misa iliyoadhimishwa katika Parokia mahalia ya Kristo Mfufuka, Askofu Mkuu amesisitiza juu ya mahitaji makuhani ambao waweze kugundua kwa upya Thamani ya huduma ya kikuhani huku wakitoa umakini kwa walio na shida zaidi na kufanya kazi kwa ajili ya kuhamasisha haki kijamii. Kama mapadre amesema Askofu Mkuu hawawezi kufunga macho yao mbele ya hali halisi za ukosefu wa haki, ufisadi, ubaguzi na dhuluma kwa jirani, hawezi kubaki kimya mbele ya ubaya ambao unazunguka kwa sababu ya wito wao unawajibisha kukemea.

Askofu Mkuu Anani Barrigah zaidi amekumbusha mapadre kuwa huduma yao ni ya muda wote na haiwezi kupunguziwa katika nafasi za shughuli. Na zaidi amewakumbusha makuhani kuwa huduma yao ni ya wakati wote na haiwezi kupunguzwa kuwa riziki tu au jukumu la kazi, au kutimizwa kwa muda mfupi(part time), kana kwamba ni hali fulani za maisha ambazo hazimhusu hapana. Siyo makuhani wakati wanapovaa nguo za kikuhani kuadhimisha Ekaristi tu, na baadaye   kuwa watu wa kawaida wanapovaa nguo za kiraia, Askofu Mkuu, amekemea kwa ukali kwamba badala yake watambue kuwa wao ni makuhani kwa sababu ukuhani hauwezi kutengenishwa nao.

Kwa kupokea upako wa kikuhani, amesisitiza kiukweli, kuhani anakuwa mtumishi wa Mungu: “yeye siyo mali yake binafsi, bali mwili wake wote na roho yake inaingizwa na kuwa na kitambulisho kipya anachopokea wakati wa kuwekwa wakfu”. Hatimaye Askofu Mkuu wa Lomé amewaalika makasisi wote wa eneo hilo kuzingatia kila wakati maadili muhimu ya maisha, bila kusahau masikini na walio katika mazingira magumu sana, kwa sababu amesema kuwa “wale ambao hawawezi kuona shida za majirani zao, kiukweli wao hawana uhuru ni wafungwa binafsi”.

15 September 2020, 12:52