Tafuta

Vatican News
Milo ya Maria ni mpango wa mshikamano pia ulioungwa mkono na Papa Francisko ili kuhakikisha chakula cha watoto maskini barani Afrika na kwingineko Milo ya Maria ni mpango wa mshikamano pia ulioungwa mkono na Papa Francisko ili kuhakikisha chakula cha watoto maskini barani Afrika na kwingineko  (WFP/Gabriela Vivacqua)

Slovakia:Mpango wa kupata mlo unaoungwa mkono hata na Papa!

‘Mary’s Meals’ yaani Milo ya Maria ni mpango wa mshikamano pia ulioungwa mkono na Papa Francisko ili kuhakikisha chakula cha watoto wengi maskini lakini pia Afrika na kwingineko,utakaofanyika kwa njia ya mashindano ya hisani tarehe 19 Septemba 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baada ya mafanikio ya kushangaza ya mwaka jana ambayo yalileta fedha kwa waandaaji kwa ununuzi wa milo 43,000, mpango wa Milo ya Maria utarudiwa kuanzia Septemba ijayo tarehe 19 huko Tatranská Lomnica nchini Slovakia. Wakati huo huo,  wamenzisha siku za hivi karibuni nchini Slovakia kupitia mtandaoni mbiu hiyo ambazo zitaisha Jumapili ijayo. Ni ishara ndogo ambazo hubadili ulimwengu. Miongoni mwa wahusika wakuu wa mbio ya hisani ya 'Milo ya Maria' pia ni mwanariadha wa Kislovakia Ján Volko, ambaye mwaka huu ni mmoja wa ushuhuda wa mbio maarufu ya hisani ambayo inataka kumhakikishia chakula cha mtoto maskini, kwa mwaka mzima wa shule, hivyo kuwasaidia kujifunza kusoma na kuandika.

Ukaribu kwa watoto maskini

Ada ya usajili ni euro 18.30, ambayo ni kiasi muhimu kununua chakula kwa mtoto kwa mwaka mzima. “Chakula huandaliwa na watu wa kujitolea katika shule hizo hizo, kwa kutumia bidhaa zinazolimwa na wenyeji. Chakula huvutia watoto ambapo wasinge hudhuria shule hizo kwa mujibu wa Alexandra Murínová, mratibu na mwanakujitolea  wa  "Milo ya Maria" nchini Slovakia. Wanaofaidika na mpango huo ni watoto 1,667,067 wa nchi za  Malawi, Liberia, Zambia, Zimbabwe, Haiti, Kenya, India, Sudan Kusini, Uganda, Ethiopia, Benin, Lebanon, Sria, Myanmar, Thailand, Ecuador, Nigeria, Madagascar na Romania.

Mpango wa Milo ya Maria kutiwa moyo na Papa

Miongoni mwa watoa msaada huo  pia ni Papa Francisko na Malkia Elizabeth wa Uingereza kwa mujibu wa maelezo ya  Murínová, na kuongeza kusema kwamba kwa mtindo huo wa gharama nafuu, shukrani inayowezekana kufikiwa na watu wa kujitolea 80,000, wanaweza pia kusaidia uchumi wa eneo hilo. 'Milo ya Maria' ni mpango ulianzisha mnamo mwaka 2002, wakati Magnus MacFarlane-Barrow alipotembelea nchini Malawi wakati wa njaa na alikutana na mama aliyekuwa anakaribia kufa na ukimwi. Magnus alimuuliza mtoto wa mwanamke huyo kuhusu  ndoto zake na matarajio yake yalikuwa nini. Mvulana huyo alijibu kuwa angependa kula kila siku na kwenda shule. Tangu wakati huo ndipo ulianza mchakato huo kwa mujibu wa mwanakujitolea huyo. Papa Francisko alikutana na mwanzilishi wake mnamo  tarehe 11 Mei 2016, baada ya Katekesi yake. Baada ya kusikiliza kwa makini kuhusu Mpango wao wa 'Milo ya Maria', Papa huyo alihimiza kikundi hicho na kuwatia moyo akisema “endeleeni mbele na Mungu abariki kazi yako”.

14 September 2020, 17:54