Tafuta

Vatican News
Virusi vya corona mwaka huu vimeleta madhara makubwaya kiuchumi hata sekta ya utalii Virusi vya corona mwaka huu vimeleta madhara makubwaya kiuchumi hata sekta ya utalii   (POLONIO VIDEO)

Siku ya 41 ya Utalii Duniani.Askofu Roman:kuzaliwa upya kunaweza kuanzia maeneo ya vijijini!

Ili kusherehekea siku ya Utalii Duniani,Mchungaji wa kitengo cha Utalii nchini Brazil ameandaa Wiki ya Kitaifa ya Utalii kuanzia tarehe 21 hadi 27 Septemba na shughuli mbali mbali za mikutano ya mitandanoni licha ya maadhimisho ya pamoja katika manispaa za Brazil.Amemabinisha kuwa suala la utalii linaweza hata kudhaminishwa na kuanzishwa kuanzia maeneo ya vijijini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Dominika tarehe 27 Septemba ni Siku ya 41 ya Utalii Duniani, sekta mojawapo maalum ambayo imeguswa sana na janga la Covid-19 katika Nchi nyingi sana zilizokubwa vibaya na janga hili kwa mfano Brazil. Kupitia tovuti ya Baraza  la  Maaskofu nchini  Brazil, hasa kwa mhusika wa Kitengo cha uchungaji wa Utalii Askofu Mkuu Irineu Roman wa Santarém, , anasisitizia, kati ya mada nyingine nyingi, utalii katika mazingira ya vijijini, hali ya sekta ya utalii katika muktadha wa janga la Coronavirus na mitazamo ya janga baada ya janga.

Kaulimbiu mbiu yam waka huu unaangazia “Utalii na Maendeleo Vijijini” ambayo iliwasilishwa na Shirika la Utalii Ulimwenguni na kuuungwa mkono na  Vatican kupitia Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu. Kwa mujibu wa uratibu wa kitaifa, rais wa wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani Kardinali Peter Turkson, amethibitisha katika ujumbe kwamba “kaulimbiu iliyochaguliwa na Shirika la Utalii Ulimwenguni kabla ya janga la Covid-19 kwa siku zetu hizi, inaonesha moja ya uwezekano wa mchakato wa kuanza ka upya wa sekta ya utalii”. Katika Hotuba ya Kardinali inazungumzia hali ngumu sana ambayo ulimwengu wa utalii unakabili janga hilo, ikiwa moja ya sekta zilizoathiriwa zaidi na matokeo ya shida ya afya duniani.

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Roman, katika muktadha wa Brazil inawezekana kurudi katika maeneo makubwa ya vijijini kutoka kaskazini hadi kusini mwa nchi, maeneo ambayo bado yamejifichika, na zaidi hayajathaminiwa na ambayo yanaweza kugunduliwa sasa, kwa upya yakithaminiwa kama kuzindua tena utalii wa ndani. Mazingira ya vijijini anayeishi katika maeneo hayo, bado hayajachafuliwa, na ikiwa yatakuzwa kwa njia za utalii, watapata fursa kubwa za uendelevu na uboreshaji.

“Katika mazingira haya ya vijijini, kukuza utalii endelevu na uwajibikaji na kanuni nzuri za haki ya kijamii na kiuchumi, kuangalia heshima kamili kwa watu na tamaduni, kuthamini jamii za wenyeji, kuheshimu mila yao, katika utunzaji wa maendeleo endelevu, huo ni utalii unaoleta mwingiliano mzuri kati ya tasnia ya utalii, jamuiya na wasafiri”, amesema. Ili kusherehekea tarehe siku ya Utalii Duniani Mchungaji wa kitengo cha Utalii nchini Brazil ameandaa Wiki ya Kitaifa ya Utalii kuanzia tarehe 21 hadi 27 Septemba na shughuli mbali mbali za mikutano ya mitandanoni mbali na  maadhimisho ya pamoja  katika manispaa ya Brazil.

18 September 2020, 11:38