Tafuta

Vatican News
Rais Mattarella akiwasha taa huko Loreto katika madhabahu Rais Mattarella akiwasha taa huko Loreto katika madhabahu  (ANSA)

Rais wa Italia awasha taa ya amani ishara ya kuanza kwa upya

Katika fursa ya siku kuu ya kuzaliwa kwa Bikira Maria,Rais wa Jamhuri ya nchi ya Italia Bwana,Sergio Mattarella,amewasha taa ya amani ambayo ni kwa miaka 22 tangu kuanza tukio hili sambamba na Jubilei ya Bikira Maria na kuwa na maana kubwa ya kimataifa.Askofu Mkuu Dal Cini amesema viongozi wote wawe halisi wa ujenzi wa amani ya kweli.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Madhahabu ya kimataifa ya Mama Maria wa Loreto, Jumanne tarehe 8 Septemba 2020, ikiwa mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Mama Maria, Rais wa Jamhuri ya nchi ya Italia Bwana   Sergio Mattarella ameweza kuwasha mshumaa wa amani katika Kanisa Kuu la Nyumba takatifu  ambapo karibia watu 250 walikuwamo na wakati  huo huo katika uwanja karibia watu 600  walikuwapo kwa kufuata sheria za kuzuia maambukizi ya covid-19 na  kusali pamoja sala ya Malaika wa Bwana.

Ni karibia masaa mawili ya ziara ya rais Matarella ambaye amekuwa ni kiongozi mkuu wa Pili wa Italia kuwasha taa hiyo baada ya rais Mstaafu Carlo Azeglio Ciampi kunako mwaka 2002. Alialikwa mwezi Januari mwaka huu na Askofu Mkuu na mwakilishi wa Kipapa katika Madhabahu hiyo ya Loreto, Askofu Fabio Dal Cin. Rais wa nchi ameudhuria Misa takatifu iliyoongozwa na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano wa kimataifa.

Katika mahuburi yake ya Askofu Gallagher amesisitiza kuhusu maombi kwa ajili ya amani yanavyo leta maana kubwa sana katika mantiki ya Jubilei ya Bikira Maria na  ambayo iliyoongezwa na Papa hadi tarehe 10 Desemba 2021, kwa maana ya  kuomba amani  kwa ajili ya  ulimwengu wote. Hata hivyo mara baada ya kuwasha taa hiyo, rais Matarella ametembelea kwa faragha katika Kikanisa cha Mama Maria katika Nyumba Takatifu na baadaye akashiriki sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja wa Kanisa Kuu  na  kupokea baraka ya ulimwengu mzima pia kuona tamasha la wanaanga.

Jubilei ya Bikira Maria inahusiana na miaka 100 tangu kutangazwa kwa mama Maria wa Loreto kuwa msimamizi wa marubani wa anga. Katika mahojiano na Askofu Mkuu Dal Cin na Vatican News amesisitiza jinsi ya umakini wa maombi unavyokumbatia ubinadamu wote hasa katika kipindi hiki kigumu cha janga na ambacho kinatakiwa kuanzia na ushirikishano. Katika mahojiano hayo aidha Askofu Mkuu anabainisha kuwa wakati wa maombi ilikuwa, kukumbuka, kutafakari kwa kina na rahisi sana ambapo pia baadaye taa iliwashwa hasa kwa  nia hii ya maombi kwa ajili ya  wakuu wote wa serikali, watu, mataifa, na watawala wote, ili wawe waaminifu kweli na wajenzi wa amani na mema ya watu waliokabidhiwa

Vile lengo la kuwasha taa ni kama kielelezo cha nia hiyo ya maombi ambayo inakwenda kwa Mungu moja kwa moja kupitia kwa Mama Maria hasa mwaka  huu wa Jubilei na kwa wakati huu maalum kwa wanadamu wote ambao wanataka kuanza kwa upya safari ya udugu na kushirikishana. Kushirikishana siyo tu mateso, lakini pia mipango ya kujenga kitu bora na kwa roho ya matarajio ya Waraka mpya ambao Papa Francisko  ataweza kuutoa kutoka Assisi tarehe 3 Oktoba ijayo, Amesisitiza Askofu Mkuu Dal Cin.

Akizungumza juu ya mwaliko kwa Rais Matarella, pia kutokana na janga la virusi alifikiri haitawezekana, lakini ushiriki wake ulikuwa kwa namna fulani  na ushiriki wa watu pia kwa kufuata sheria za dharura ya kiafya, wa maana  na hivyo ilikuwa ishara kubwa ya tumaini na kwa hilo wanamshukuru Bwana, na amesema kuwa amemwona hata rais mwenyewe akifurahi kushiriki katika ibada rahisi, lakini yenye  upeo mkubwa wa ulimwengu.

Jambo muhimu pia lilikuwa uwepo wa Katibu wa Vatican wa Uhusiano na ushirikiano wa kimataifa Askofu Mkuu  Gallagher, ambaye ameunganisha pamoja maombi ya amani hapo Loreto pamoja na wakati mgumu ambao tulio nao  katika muktadha wa sera za kisiasa kimataifa. Na alipendelea uwepo wake kwa hakika katika nafasi yake aliyo nayo kwa sababu analo jukumu, hasa kuonyesha na kuhamasisha wito wa Papa Francisko  juu ya amani ulimwenguni ambayo yeye kama katibu wa mahusiano ya kimataifa yuko mstari wa mbele kuikuza. Kwa kutoa mfano, Askofu Dal Cin amesema, tufikiri juu ya uwepo wa Kanisa katika nchi nyingi za ulimwengu hasa kwa lengo hili la kuwa ishara na chombo cha amani ulimwenguni.

08 September 2020, 18:46