Tafuta

2020.09.12 Kanisa Kuu la Mama Yetu la Yamoussoukro nchini Pwani ya Pembe 2020.09.12 Kanisa Kuu la Mama Yetu la Yamoussoukro nchini Pwani ya Pembe  

Pwani ya Pembe:Miaka 30 ya madhabahu ya Maria huko Yamoussoukro

Ilikuwa ni tarehe 10 Septemba 1990 ambapo Mtakatifu Yohane Paulo II aliweka wakfu Kanisa Kuu la Yamoussoukro kuwa chini ya Usimamizi wa Mama Yetu wa Amani.Katika kumbukizi la miaka 30 kwenye Madhabahu hiyo wametoa mwaliko wa kusali kwa ajili ya amani ya nchi hiyo, ya Afrika na ulimwengu mzima.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Hii ni Madhabahu iliyotolewa kwa Bikira Maria. Maria wa Nazareth, Maria ambaye alipokea kwa imani tangazo la wokovu(…) Maria, upinde wa Agano jipya la Mungu na watu! Pamoja na Kanisa hili, tunatoa heshima kwa Mama yetu wa Amani, Mama wa Mkombozi, wa Kristo ambaye alitupatia zawadi ya amani yake katika kesha wa sadaka yake ya wokovu”. Haya yalikuwa ni maneno yaliyotamkwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kunako tarehe 10 Septemba 1990 huko Yamoussoukro, nchini Pwani ya Pembe wakati wa kutabaruku Basilika mahalia ambayo ilikabidhiwa katika usimamzi wa “Mama Yetu wa Amani”.

Katika miaka 30 kamili tangu tarehe hiyo, eneo hilo la sala na ibada limeona kwa mara nyingine tena aadhimisho kuu lilioongozwa na Askofu Alexis Touably Youlo wa Jimbo la  Agboville na masimamizi wa Kitume wa mji. Jubilei ya kweli imeahirishwa hadi mwaka 2021 kwa sababu ya janga la corona. Katika mahubiri yake Askofu Touably Youlo amesema Madhabahu hiyo ni mwaliko wa kusali kwa ajili ya amani ya nchi hiyo, kwa ajili ya Afrika na ulimwengu mzima. Hawawezi kuwa na jengo kama hilo ishara ya mapatano, katika moyo wa Taifa lao na baadaye kuwanza kutenganishwa na mizozo isiyo na maana. Kwa sababu na Kanisa hilo, changamoto ya amani imezinduliwa kwa watu wote wa Pwani ya Pembe.

Kwa upande wa  msimamizi wa mahali hapo Padre Franck Allatin, alitangaza kwamba  jengo hilo, katika  hatua kwa hatua litaanza kukarabatiwa, awali ya yote ku kuhakikisha wanazuia upitishaji wa maji. Kwa upana wa mita 150 na uwezo wake wa kukaa waamini  18,000, na mabenchi 7,000 , Kanisa kuu la Yamoussoukro ni miongoni mwa majengo makubwa ya dini Katoliki ulimwenguni. Ujenzi wake uligharimu faranga bilioni 40 kwa fedha za ndani, zilizotolewa na  mwanzilishi wake wa Pwani ya Pembe (Ivory Coast) yaani Baba wa Taifa , marehemu Félix Houphouët Boigny, aliyekuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo mnamo 1960. Leo, hii Kanisa kuu linasimamiwa na Mapadre wa Shirika la Kitume katoliki, ambao wanaitwa Mapadre Wapallottini, waliopewa jina la mwanzilishi wao, Mtakatifu Vincent Pallotti.

15 September 2020, 12:39