Tafuta

Vatican News
2020.09.01 Kadinali Jean-Pierre Kutwa, Askofu Mkuu wa  Abidjan-Nchini Pwani ya Pembe (Ivory Coast) 2020.09.01 Kadinali Jean-Pierre Kutwa, Askofu Mkuu wa Abidjan-Nchini Pwani ya Pembe (Ivory Coast) 

Pwani ya Pembe:Kard.Kutwa atoa mwaliko wa viongozi kufanya mazungumzo na mapatano!

Kufuatia na mivutano ya kisiasa kijamii,nchini Pwani ya Pembe,katika harakati za uchaguzi wa rais,Kardinali Kutwa anawaalika viongozi wa kisiasa kufanya mazungumzao na mapatano. Upatanisho unaoaminika kwa wote, ni tendo ambalo baada ya mgogoro unaruhusu walio mstari wa mbele kuungana na kuanza kwa upya.Anawaalika kutafsiri kwa pamoja katiba ya nchi bila kuacha yawe maandiishi tu.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika ujumbe mrefu wa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Abidjan nchini Pwani ya Pembe Kardinali Jean Pierre Kutwa analahumu vikali juu ya ghasia zisizo kubalika na mapigano yanayoendelea baina ya sera za vyama vya kisiasa  kutokana  na matarajio ya uchaguzi mkuu wa urais. Kardinali anakumbusha kuwa hakuna amani bila kuwa na haki na shughuli ya kiongozi anayeoongoza nchi ni ile ya kufanya jitihada ya kuheshimu Katiba na kwa ajili ya mapatano  kitaifa.

Kwa maana hiyo askofu Mkuu wa Abidjan, katika ujumbe wake, anaonesha wasiwasi mkubwa kwa kile ambacho kinaendelea kutokea katika nchi kwa miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa urais na viongozi wa serikali. Kwa mujibu wa ujumbe wake anabainisha kwamba maisha ya siasa kijamii yanaelekea kufikia mapinduzi hatari, kwa maana hiyo Kardinali Kutwa anafafanua  kuwa ni ghasia zisizokubalika kama wale ambao, wakiwa wamejihami na marungu, mawe, mapanga na silaha za moto, wamekuwa na hatia ya mauaji ya kweli. Kwa kusikitishwa na mapigano ambayo yamesababisha vifo, majeruhi na uharibifu mkubwa wa vifaa, Kardinali Kutwa anataka kutokuwepo vurugu na ghasia, badala yake kuwepo mazungumzo na kuheshimu haki na sheria, kwani  “bila kuwapo yote hayo katika hali ya kisasa siyo rahisi kujenga amani”, anaonya kiongozi huyo.

Kwa kukazia zaidi amesema :“Haiwezi kusemwa vya kutosha kwamba hakuna amani bila haki na hakuna haki bila msamaha” amesisitiza askofu mkuu wa Abidjan. “Hii ndiyo ninataka kukumbusha wale ambao wana hatima ya watu wetu mikononi mwao, ili wale ambalo kila wakati wanaruhusu kuongozwa na chaguzi muhimu na nzito wanazopaswa kuufanya katika mwanga wa wema wa kweli wa mwanadamu, kwa mtazamo wa faida ya wote pamoja. Kardinali Kutwa ametoa wito kwa maana hiyo wa dhamiri nafsi na ya pamoja ili kwamba waweze kusitisha ghasia na kuunda nafasi pana ya mazungumzo. Akiendelea kufafanua amesema: “Upatanisho tunao uamini wote ni tendo ambalo baada ya mgogoro unaruhusu walio mstari wa mbele  kuungana na kuanza kwa upya na kwa maana hiyo ninawaalika kutafsiri kwa pamoja katiba ya nchi bila kuacha yabaki maandiko tu” amesisitiza Kardinali Kutwa. Aidha anawashauri wajikite kutafuta suluhisho la mgogoro huo wa kuwafanya watumaini kwa wakati endelevu ulio bora zaidi.  Kardinali anaangazia pia sheria msingi za nchi ambazo zinafunguliwa kwa utambuzi wa haki, uhuru na uwajibikaji kwa upande wa serekali na kubainisha kuwa matukio  ya siku hizi ni muonekano wa kile ambacho bado kinatakiwa kufanyika na kuwakumbusha wote juu ya haki, kuhisi  uwajibika wa kila mmoja na kwa wote.

Kwa mtazamo wake mkuu wa Kanisa la Pwani ya Pembe anasema: “Ninaamini kwa mtazamo wanu kuwa heshima ya sheria ni muhimu na kutoa heshima zaidi ya ushindi katika uchaguzi… tunaweza sisi katika roho ya kiraia na kwa uhakika kutoa sheria yote kwa nguvu ili iweze kusaidia kuishi katika haki, katika maridhiano na amani kwa mtazamo  wa maandalizi ya kukubaliwa kwa uchaguzi bila ghasia”, anasema Kardinali Kutwa. Hatimaye anaandika kuwa “Ninaweza tu kumwambia Rais wa Jamhuri na Mkuu wa Nchi, ambaye katika  kugombea uchaguzi huu ujao siyo kazi yangu, bali kwa maoni yangu ya unyenyekevu ni kwamba uwajibu wake mkuu wa kuhakikisha Katiba na umoja wa kitaifa unahitaji ushiriki wake wa kijasiri ili kurudisha utulivu wa nchi” . Kwa maana hiyo Kardinali Kutwa anahitimisha kwa kuwasindikiza kwa sala zake na kuwaombe ili kila mtu aweze  kutekeleza majukumu yake, na busara ya kufanya kila kitu kwa kufuata sheria (...) hasa kuhusu kuheshimu haki ya kuishi. Ukosefu wowote wa haki, kwa njia yoyote itakayotokea, itasababisha machafuko. Haki inayotambua sheria  na wajibu wa kila mmoja ndiyo itakayotuletea amani”.

03 September 2020, 11:45