Tafuta

Nchini Papua Guienea wameadhimisha siku ya toba kitaifa Nchini Papua Guienea wameadhimisha siku ya toba kitaifa 

Papua Guinea Mpya:Siku ya Toba kitaifa:Ni chombo muhimu kwa ajili ya amani!

Katika kusheherekea Siku ya Toba Kitaifa,maaskofu nchini Papua Guinea Mpya wanathibitisha kuwa ni chombo msingi kwa ajili ya amani.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Baraza la Maaskofu nchini Papua Guinea Mpya  wanathibitisha kuwa Toba ni zana msingi kwa ajili ya ujenzi wa amani, wakati wa kusheherekea Siku ya kitaifa ya Toba, katika maadhimisho ya iliyoongozwa na Katibu wa Mawasiliano ya kijamii ya Baraza la Maaskofu, Padre Ambrose Pereira tarehe 26 Agosti  2020 huko Port Moresby. Kwa mujibu wa kiongozi huyo amesema kuwa  “Ikiwa sisi wenye dhambi tunatubu, Mungu daima yuko tayari kusamehe”. Maadhimisho hayo yalikuwa yameambatana na ishala za vifaa ili kukumbuka hata uhai wote wa waamini hasa umuhimu wa kutubu kwa mfano waling’iniza noti za fedha kwenye matawi ya miti, ikiwa ni ishara ya amani na  kuonyesha uaminifu uliopatikana kwa mara nyingine tena, wakati ubadilishanaji amani walikuwa na matawi ya karanga za areka zikionyesha kwao  mwisho wa mizozo kati ya watu wote. Vitu vyote hivi baadaye viliwekwa chini ya altare ya madhimisho ya misa.

Washiriki wa tukio hili pia walisari Rosari ya Huruma ya Mungu na iliyoongozwa na  Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu, Padre Giorgio Licini. Siku ya Tiba  kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Baraza la Maaskofu ya Walei na mwandaaji wa tukio hilo Bi. Eva Wangihama, amesema ni siku ya siku kuu, kwni ni jambo ambalo linapaswa kuadhimishwa na kukumbukwa kila siku hata kwa wakati ujao. Ni muhimu kukumbuka kuwa Papua Guinea Mpya katika, siku ya Toba hufanyika mikutano mingi ya sala katika nchi yote na kwa maana hiyo ni suala lenye tabia ya kiekumene, kwa kuunganisha hata madhuhebu mengine mengi. Siku hii ilipendekezwa kwenye miaka iliyopita na kikundi cha makanisa, mwaka 2011 wakati wa Waziri Mkuu Peter O'Neill aliporidhia Katiba ya nchi.

04 September 2020, 12:55