Tafuta

Nigeria:Vitendo vya kigaidi na mauaji vinaendelea Nigeria:Vitendo vya kigaidi na mauaji vinaendelea 

Nigeria:Idadi ya vifo vya wakristo nchini Nigeria vimezidi kuongezeka!

Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji linabanisha kuwa idadi ya wakristo waliouwawa nchini Nigeria inazidi kuongezeka kila kukicha.Maaskofu katoliki kutoka kanda ya Kaduna kwa miezi ya hivi karibuni walidhibitisha kuwa nchi iko katika machafuko yanayofanywa na magaidi wanaoonekana kuitawala nchi ya Nigeria huku watu wengi wanapoteza maisha yao.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatian.

Machafuko na vitisho huku upendo, msamaha na amani kutoweka nchini Nigeria kutokana na mashabulizi ya kigaidi yaliyodumu sasa takribani miaka minne yanapelekea idadi ya vifo vya wakristo waliouawa ndani ya miezi saba huko Kaduna nchini Nigeria kufikia 178. Taarifa iliyotolewa na Bwana Benoît de Blanpré Mkurugenzi Baraza la Kipapa la Makanisa hitaji nchini Ufaransa inasema, mauaji hayo yanayofanywa na kikundi cha kislamu cha Boko Haram yamepelekea watu zaidi ya 36 elfu kupoteza maisha na mamilioni ya watu kuteseka. Wakristo, waislamu na wafuasi wa dini za Jadi ndiyo wamekuwa wahanga wa vikundi vya Boko Haram na vikundi vingine vya kigaidi. Bwana Benoît de Blanpré amesema vita dhidi ya ugaidi iliyoanzishwa mnako 2012 nchini Nigeria inaendelea hasa Kaskazini mwa Nigeria ambako kuna mashambulizi ya kila siku na Serikali ya Nigeria bila kuchukua hatua madhubuti.  

Maaskofu katoliki kutoka Kanda ya Kaduna kwa miezi ya hivi karibuni walidhibitisha kuwa nchi iko katika machafuko yanayofanywa na magaidi wanaoonekana kuitawala nchi ya Nigeria huku watu wengi wanapoteza maisha yao. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni yale ya Benue, Kebbi, Plateau, Kaduna, Katsina, Nasarawa, Niger, Sokoto na Zamfara ambapo mashambulizi mengi yamefanywa na vikundi vya Boko Haram. Naye Padre Sam Ebute kutoka Shirika la kimisionari la Afrika wametaarifu kuwa, katika Jimbo la Kafanchan, Parokia ya Kagoro, wakristo 21 wa Parokia hiyo waliuawa na wengine 30 kujeruhiwa vibaya. Uvamizi mwingine ni ule uliofanyika tarehe 21 Julai 2020 katika kijiji cha Kukum Daji katika warsha ya vijana. Mashambulizi haya yanapelekea kukosekana kwa amani. 

Kwa muda wa miaka minne sasa kumekuwa na ongezeko la wasiwasi kwa kuwa wakati wowote wanaweza kushambuliwa na magaidi hao. Mashambulio hayo yanapelekea kudumaa kwa imani na kukosekana kwa amani kwani watu wa maeneo hayo wanaishi katika mashaka na wasiwasi mkubwa.  Ugumu bado unasababishwa na Serikali iliyoko madarakani kutokuchukua hatua ili kuzuia mauaji hayo. Uzembe huo wa Serikali unapelekea kukosekana kwa msamaha, upatanisho upendo na amani katika jamii

23 September 2020, 17:14