Tafuta

Vatican News
Mafuriko nchini Niger yameleta madhara makubwa sana hata katika mikoa ya Kaskazini mwa Nigeria. Mafuriko nchini Niger yameleta madhara makubwa sana hata katika mikoa ya Kaskazini mwa Nigeria.  (AFP or licensors)

Niger:dharura ya mafuriko:Kanisa liko mstari wa mbele lakini msaada zaidi unahitajika!

Katika dharura ya mafuriko nchini Niger yaliyoikumba hata nchi ya Nigeria Kaskazini,Askofu mkuu Lompo anasema Kanisa liko mstari wa mbele japokuwa kunahitajika msaada zaidi wa haraka kutoka kwa watu wenye mapenzi mema ili kuwaokoa watu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni miezi miwili karibu nchini Niger ambapo mvua za nguvu zilizosasababisha mafuriko ambayo hadi sasa yameleta vifo vya watu 65, na zaidi ya watu 200,000 kukosa makazi , vile vile madhara makubwa kutokana na kuharibika kwa miundo mbini na kilimo katika nchi ambayo ni mojawapo ya nchi zilizo maskini zaidi katika bara la Afrika. Kwa mujibu wa maelezo yake Askofu Mkuu wa mji mkuu Niamey, Mhashamu Laurent Lompo, kupitia Tovuti ya Baraza la Maaskofu wa Kanda ya Afrika Mashariki(Recowa-Cerao)amebainisha kwamba kipindi hiki sehemu kubwa ya vijiji vilivyopo karibu na mto Niger, vimejaa maji.

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu anasema hali hiyo imesababaisha madhara makubwa sana katika mashamba, kilimo cha mpunga, lakini hata kupoteza maisha ya watu. Akifafanua tukio hili Askofu Mkuu wa Niamey anabainisha ni kwa jinsi gani wamepata pigo kubwa hasa kurudiwa kuwa na ukosefu vyakula. Mafuriko hayo yameukumba hata mji mkuu. Baadhi ya mitaa watu hawawezi kutembea tena. Hata Kanisa Kuu limekumbwa na maji. Katika parokia mmoja ambayo iko karibu na mto, waamini wengi wamebaki bila makazi. Katika parokia nyingine ambayo iko karibu na jumuiya ya Wamisionari wa Upando wa Mama Teresa wa Calkuta imebidi waache nyumba zao na wagonjwa wanaowatunza wamehamishiwa katika majengo mengine ya kiafya, amefafanua Askofu Mkuu Lompo.

Kakatika hali hii Askofu Mkuu Lompo amesema, Caritas mahalia, tayari imekwisha jikita mara moja kutoa msaada kwa waathiriwa, japokuwa haitoshi. Kutokana na  mantiki hiyo anawalekea watu wote wenye mapenzi ili wasaidie katika shughuli hii ya Kanisa. Kwa maelezo yake amesema ongezeko la msaada mwingine utawaruhusu kuendelea kusadia vema watu hao. Ameomba hayo huku akiwa na wasiwasi hata kuhusu ufunguzi wa mwaka wa shule nchini humo. “Ikiwa hatuwezi kusimika mahema na kuwawapatia chakula watu, ikiwa hatuangaikii afya ya watu hawa, hasa katika kipindi cha sasa cha mgogoro wa kiafya, ipo hatari kubwa! Hali halisi ya  huzuni ni kwamba wathirika wa Nigeria vile vile ni kama wa Nigeria ambao wanaendelea kuteseka kusikoelezeka” amesema Askofu Mkuu Lompo.

Mafurikio hayo yameikumba kwa nguvu zote hata kaskazini mwa Nigeria mpakani mwa Niger, ambayo yameikumba karibu mikoa nane. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa hivi karibuni na Baraza la mawaziri wa Nigeria, Hekari 7,000 za mashamba na hekari 3,082 za mazao yaliyopandwa vimemezwa na maji. Serikali ya Niamey imetangaza hatua za msaada kwa waathiriwa. Karibu kwa miaka kumbi hivi, nchini Niger inaendelea kusumbuliwa sana na makundi yenye silaha ya kijahadi, kama vile Boko Haram karibu na Nigeria, Aqmi, al-Qaeda katika Maghreb ya kiislam, Gsim(kundi linalosaidia waislam na la kiislam) Shirika salafita lililozaliwa kunako mwaka 2017 wakati wa vita vya Mali. Na mashambulizi yamekuwa mfululizo kwa miezi hii ya mwisho.

18 September 2020, 12:08