Tafuta

Vatican News
Kipindi cha kazi ya uumbaji kuanzia Mosi Sept hadi 4 Oktoba. Kipindi cha kazi ya uumbaji kuanzia Mosi Sept hadi 4 Oktoba. 

Kipindi cha Kazi ya Uumbaji-Cecilia Dall’Oglio:kazania udugu!

Mada ya toleo la 2020 ni Yubilei ya Dunia:mwenendo mpya wa matumaini. Mahojiano na Vatican news na Cecilia Dall’Oglio mwanaharakati wa chama katoliki ulimwenguni kwa ajili ya tabianchi na Mjumbe wa Kamati tendaji ya kiekumene katika Kipindi cha Kazi ya Uumbaji anasisitizia juu ya utunzaji wa nyumba yetu kwa mtazamo na ushauri wa Papa Francisko.

Tarehe Mosi Septemba imeanza kipindi cha kazi ya Uumbaji. Ni maadhimisho ya kila mwaka hasa kuhamasisha matendo ya dhati kwa ajili ya kulinda nyumba yetu ya pamoja ambapo wanashiriki madhehebu yote ya wakristo wote na wenye mapenzi mema. Mada ya toleo la 2020 ni “Yubilei ya Dunia: mwenendo mpya wa matumaini”. Katika Mahojiano na Vatican news na Cecilia Dall’Oglio mwanaharakati wa chama katoliki ulimwenguni kwa ajili ya tabianchi na Mjumbe wa Kamati tendaji ya kiekumene katika Kipindi cha Kazi ya Uumbaji. Kwa mujibu wa Bi Dalloglio kuhusiana na mada anakumbuka hasa kwa mwaka huu katika sala ya Papa Francisko mwezi Machi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican.

Papa Francisko wakati wa sala yake  alifananisha janga la virusi vya Corona kama dhoruba kali  isiyotarajiwa na yenye hasira ambayo ilitukumba na kuweza kutambua kuwa  sisi sote tuko katika mtumbwi moja, lakini wote ni  wadhaifu na wasio na mwelekeo japokuwa ni muhimu na lazima wote kuitwa kubaki pamoja wenye kuwa na  mahitaji wa kusaidiana kwa pamoja. Mada iliyochaguliwa na kamati tendaji ya Kiekumene kwa ajili ya Kipindi cha Kazi Uumbaji ilichaguliwa kabla ya kuzuka kwa janga. Lakini hata bado inaangazia hali halisi ya kipindi tulichomo ambacho tumelazimika kupumzika na tumeonja kwa dhati nini maana ya kuathirika. Kwa maana hiyo mada ya Yubilei ya Dunia katika Kipindi cha kazi ya Uumbaji 2020, kwetu sisi ni mwaliko mkubwa wa uwajibikaj ili kweli tuweze kuanza kwa upya kwa sasa na baada ya mgogoro huu amesisistiza Bi Dall'oglio.

Katika Kipindi cha Kazi ya Uumabji lazima kutafuta kwa dhati michakato mipya ya safari ya kielekolojia fungamani na ambayo  inafungamanisha na ubinadamu wote kama ndugu. Tunatambua kuwa katika Laudato kwamba ni waraka wenye tunu msingi wa safari hii, amebainisha. Ni muhimu wakati wa kipindi hiki kuonesha wazi ubunifu kwa ajili ya kuhamasisha zaidi maombi, uongofu wa kijumuiya na kibinafsi na juhudi zaidi za utunzaji wakazi ya Uumbaji.  Hata hivyo kauli mbiu inayoongoza mwaka huu, inakumbusha kitabu cha Walawi,  katika Agano la kale kama kipindi cha kurejea tena na kupumzika kwa dunia, vile vile  hata kwa kukombolewa kwa watumwa.

Kutokana na hilom hapa ndiyo maana sisi pia tunahitaji kukombolewa kutokana na kukosa mwelekeo wa  hatima, kutokuwa na tumaini, hasa mtazamo wa kile kiitwacho uchumi fulani kama vile Papa Francisko alivyosema kuwa "unaua na ambao uendelea kuunda kutokuwa na usawa na mizozo mingi ulimwenguni, lakini pia ambayo inaharibu maelewano ya mwanadamu, ya mwanamke na uumbaji”.

Lazima tuamini, kama isemavyo Wosia wa Laudato si, kwamba mambo yanaweza kubadilika, katika kuwasiliana na jamuiya zetu kwamba zinawezekana kubadili mwelekeo, na kwamba tunaweza kuwa na mwanzo mpya kwa pamoja. Kipindi cha Kazi ya Uumbaji kwa namna hiyo  ni wakati wa kutembea kwenye njia hizi mpya za kiekolojia fungamani hatua kwa hatua. Na ndivyo kwa hakika Chama cha wanaharakati katoliki wa mabadiliko ya tabia nchi wanavyoitikia mwito wa kuchukua hatua hizo za utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja kwa mujibu wa ushauri wa Wosia wa Baba Mtakatifu Francisko.

01 September 2020, 14:35