Tafuta

Vatican News
Watawa wa ndani wanaalikwa mara nyingi na Papa Francisko  kusali kwa ajili ya Kanisa lote na shughuli za kimisionari ulimwenguni Watawa wa ndani wanaalikwa mara nyingi na Papa Francisko kusali kwa ajili ya Kanisa lote na shughuli za kimisionari ulimwenguni  (AFP or licensors)

Malawi:Jitihada hai kwa ajili ya Kanisa kwa mwezi wa Kimisionari

Watawa wa Shirika la ndani nchini Malawi wameonesha nia ya kuendelea kutoa msaada wao ulio hai wa sala kwa ajili ya kuombea Kanisa la ulimwengu katika Mwezi wa kimisionari Oktoba.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kusaidia kwa njia ya matendo ya dhati ya kitume, sala na maisha ya kutafakari kwa kina na Kanisa ambalo linatarajia kusheherekea Mwezi wa Kimisionari ndiyo jitihada ambazo zimeazimiwa na Watawa wa ndani wa Monasteri ya Maria Malkia wa Ulimwengu pamoja na ya Mama wa Huruma huko Maula, jimbo kuu katoliki la Lilongwe nchini Malawi kwa mujibu wa taarifa kutoka Amecea. Jitihada hizi zimewakilishwa rasmi na Mama mkuu wa Shirika la watawa wa ndani, Sr. Mary Monica Phiri, katika fursa ya toleo la mafunzo kwao katika Monasteri yaliyo ongozwa na Mkurugenzi wa kitaifa wa shughuli za Kimisionari (PMS) nchini Malawi Padre Vincent Mwakhwawa.

Akizungumza baada ya toleo la mafunzo hayo, Mama Mkuu Sr. Monica alisema kuwa watawa wamekubali mwaliko wa Kanisa ulio omba watawa wa ndani waweze kusali  kwa ajili ya utume wa Kanisa  na la ulimwengu na ameonesha furaha kwa niaba yao  ya kupokea ujumbe wa Papa Francisko uliotolewa kwa ajili ya fursa hii ya Siku ya Kimisionaria ulimwenguni 2020, siku itakayofanyika tarehe 18 Oktoba 2020 bila mabadiliko yoyote, kama ulivyobainishwa hivi karibuni na msemaji wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu. “Tutasaidia Kanisa la ulimwengu kusali kwa ajili ya maandalizi ya Mwezi wa Kimisionari, kwa namna kwamba hata kama nchi zote ulimwenguni ikiwemo Malawi, watakuwa bado wanakabiliana na  janga la virusi vya corona au covid-19” amesema mama mkuu huyo.

Akiendelea kufafanua zaidi aidha Mama mkubwa huyo amesema “Maandalizi yanaweza kuendelea bila vikwazo” na kusisitiza kwamba wanaamini kabisa kuwa sala hazina mpaka, na kiukweli matokeo ya sala ni mkubwa katika miyo ya maisha ya wanadamu na juu ya shughuli zote za Kanisa. Naye Mkurugenzi wa Kitaifa wa shughuli za kipapa za kimisionari nchini Malawi ameandaa toleo hili la mafunzo kwa watawa kwa lengo la kuwafanya wawe na utambuzi kati yao wa mahitaji ya kimisionari ya sasa ya Kanisa mahalia na  la ulimwengu, kwa  kushirikishana mipango ya maandalizi ya ofisi ya kitaifa na ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya Kimisionari ulimwenguni itakayofanyika tarehe 18 Oktoba 2020.

Shughuli za kipapa za kimisionari (PMS) nchini Malawi imeendesha siku hii ya mafunzo ya kimisionari katika monasteri ya watawa wa ndani ili kuwafanya  watambue kwa dhati shuhuli zote za kimisionari kwa Kanisa mahalia na la ulimwengu mzima, wongozo wa Papa Francisko na maaskofu wa Malawi katika maandalizi ya Mwezi wa Kimisionari Oktoba”, amebainisha mkurugenzi. Aidha kwa mujibu wake “Nimewataafu watawa kuhusu shauku ya Papa Francisko kwamba watawa wa ndani wasali mara nyingi kwa ajili ya shughuli za kimisionari za Kanisa na wasali kwa ajili ya upyaisho wa kimisionari katika wakati wa sasa”, amehitimisha Padre Mwakhwawawa.

01 September 2020, 13:51