Tafuta

Vatican News
2019.07.09 .Upandaji wa miti kama sehemu ya kampeni y a Kipindi cha Kazi ya Uumbaji 2019.07.09 .Upandaji wa miti kama sehemu ya kampeni y a Kipindi cha Kazi ya Uumbaji 

Ufilippini:Miti 60elfu imepandwa kwa siku moja wilaya ya Bohol!

Mapadre,watawa na walei wenye mapenzi mema hasa vijana na watoto wamepanda miti katika Parokia zinazozungukia Jimbo la Tagbilaran,kama sehemu ya jitihada ya Kampeni ya Kipindi cha Kazi ya Uumbaji.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jimbo katoliki la  Tagbilaran nchini Ufilippini kwenye Wilaya ya Bohol katika Kampeini ya Kipinidi cha Kazi ya Uumbaji Jumapili iliyipotoa maelefu ya watu wameweza kupabda miti 60,000 ili kuendeleza mazingira bora katika kisiwa hicho. Hawa  walikuwa ni mapadre, watawa, walei na hasa vijana ambao wamewezaa walipanda miti yenye kuzaa matunda na miti migumu katika parokia za jimbo hilo, Askofu Alberto Uy wa Tagbilaran amesema.

Kupanda miti 10 kila mmoja

"Hivi ndivyo tulivyoomba kwamba watu, hasa vijana, watajifunza kupenda kazi ya uumbaji na kutunza mazingira", amesema askofu huyo wa miaka 53.  Mpango huo ni mojawapo ya shughuli nyingi za Kanisa la Ufilipino kwa wakati huu wa kipindi  cha sasa cha kiekumene cha 'Kazi ya  Uumbaji', tangu tarehe Mosi hadi tarehe 4 Oktoba . Zaidi ya makanisa  70 na mashirika ya asasi za kiraia tangu  Septemba Mosi  walizindua sherehe ya Kipindi cha Kazi ya Uumbaji  ambayo inahimiza watu kuitikia wito wa kutunza sayari ambayo ni nyumba yetu ya pamoja. Kanisa nchini Ufilipino  hata hivyo litaongeza kipindi hicho kwa wiki moja hadi tarehe 11 Oktoba 2020. "Kwa hakika angalau watu wa kujitoleoa 100 katika kila parokia ya Tagbilaran wamejiunga na mpango huo na kupanda miti 10 kila mmoja katika mazingira yao, nyuma ya nyumba zao, na maeneo mengine yaliyotengwa". Askofu Uy amesema na kuongeza kuwa  kila Mkristo ameitwa kujali kazi ya uumbaji wa Mungu, akionyesha kwamba miti siyo tu inapamba mazingira lakini pia inaleta faida nyingi kwa watu. “Naomba sisi sote tuendeleze upendo kwa kazi ya  maumbile na tuanze kutunza mazingira”.

Kupoteza sehemu kubwa iliyopandwa miti

Kulingana na takwimu kutoka shirika la  Uangalizi wa Misitu Ulimwenguni (Global Forest Watch (GFW), ambalo huangalia misitu ya ulimwengu karibu kwa wakati halisi, inainisha kwamba nchi ya Ufilipino ilikuwa na hekta milioni 13.2 za msitu wa asili, ikiongezeka zaidi ya 62% ya eneo lake la ardhi. Mnamo 2019, ilipoteza hekta 48.2,000 za msitu wa asili, sawa na tani milioni 19.1 za uzalishaji wa CO₂. Kuanzia 2001 hadi 2019, nchini Ufilipino imepoteza hekta milioni 1.23 zinazofunika msitu wa miti, sawa na kupungua kwa 6.6% kwa kifuniko cha miti tangu 2000, na tani milioni 498 za uzalishaji wa CO₂.

Jitiha za jimbo 

Shirika la usimamizi wa Misitu Ulimwenguni (GFW) pia lilibaini kuwa kunako 2010, Bohol ilikuwa na hekta 165,000 za kifuniko cha miti, ikiongezeka hadi zaidi ya asilimia 41 ya eneo lake la ardhi. Katika 2017 hata hivyo, kisiwa cha marudio cha watalii kilipoteza hekta 583 za kifuniko cha miti, ikipoteza uwezo wa kuufikia sawa na kilo 57.4 za uzalishaji wa kaboni dioksidi. Askofu Uy, ambaye jimbo lake  linaongoza katika mipango mingine ya hatua za kijamii ikiwa ni pamoja na utoaji wa nyumba za gharama nafuu kwa watu wasiojiweza, ameeleza  kuwa badala ya kutafuta aina nyingine ya mimea kwa sasa Bohol inaelekea katika kupanda miti ya kawaida migumu na yenye kuzaa matunda.

11 September 2020, 15:33