Tafuta

Vatican News
Ghasia kati ya raia na vyombo vya dola nchini Colombia ambapo Askofu mkuu Bogota ameona akiwataka kuwa na amani badala ya chuki na kuwa wahudumu wa maisha na msamaha Ghasia kati ya raia na vyombo vya dola nchini Colombia ambapo Askofu mkuu Bogota ameona akiwataka kuwa na amani badala ya chuki na kuwa wahudumu wa maisha na msamaha  (ANSA)

Colombia-Ask.mkuu Bogota:hakuna wamisionari wa chuki bali wahudumu wa amani!

Askofu Mkuu Luis José Rueda Aparicio,wa Jimbo Kuu katoliki Bogota wakati wa kufanya Ibada ya mkesha wa amani kati ya usiku wa Jumamosi tarehe 12 Septemba 2020 amesema wao siyo bwana wa maisha kwa yoyote bali wanapaswa kuomba kuomba msamaha,yeye akiwa wa kwanza.Ni kufuatia na machafuko na ghasia kati ya vyombo vya dola na raia wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu 14.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni mbele ya vurugu na mapigano kati ya wazalendo na vyombo vya dola ya katika mji mkuu wa Bogotha na katika Nchi nzima, kwa kuacha nyuma madhaya ya uchungu mkubwa wiki iliyopita kwa makumi ya majeruhi na vifo vya watu 14 miongoni mwao akiwemo wakiri mmoja Javier Ordóñez. Misa iliadhimishwa na ambayo ilitangazwa na Televisheni ya Cristovisión katika hitimisho la Wiki ya amani na kuwaombea roho za marehemu na familia zao. Katika siku ya sala, ambayo pia walikuwa na saa moja ya kuambudu Ekaristi Takatifu, wameomba hata msamaha na mapatano ya kitaifa.

Katika mahubiri yake Askofu Mkuu wa Bogotoa ameelezea mshikamano wake kwa familia zote ambazo amesema kuwa “wanafika katika mji kwa kutafuta fursa mpya, kwa matumaini ya kukuta mji, mahali ambamo wanaweza kuishi kwa amani, mahali ambamo wanaweza kufanya kazi, mahali ambamo wanaweza kujifunza, kinyume chake wanakumbana au kukabiliana  na  vurugu na chuki, ambazo ni janga la kubwa kitaifa ambalo bado halijapata tiba yake.” Nchi ambayo imeishi kwa makumi ya miaka kwa chuki hasira na  dhambi ambazo zinaharibu maisha, Askofu Mkuu wa Colombia amesisitiza kuomba Mungu ili kuufanya mji wa Bogota “uwe wa huruma, ukarimu na upendo. Huruma na msamaha wa Mungu nambao uanze hadi ufikie nyumba zetu. Tufungulie milango ya nyumba zetu kuwa hekalu la huruma”. Askofu Mkuu akiwageukia wanafamilia za waliojeruhiwa na waliokufa, katika wiki iliyopita kwenye  vurugu mbaya jijini Bogotha, askofu mkuu amesitiza kuwa: “sisi siyo wakamilifu, lakini tunaye Mungu ambaye ni mkamilifu na tunamwomba atufundishe kuwa watoto wake na vinasaba vyake vya huruma ili kuondoa chuki na hasira”.

Askofu Mkuu wa Bogotha amekataa kwa nguvu zote ule utamaduni wa adhabu na kulipiza visasi. Huo siyo uzalendo, na siyo tabia ya wana wa Mungu na kukumbusha njia ya kutotumia nguvu iliyoonesha na Yesu wa Nazareth: “Heri wahudumu wa amani, heri wenye usafi wa moyo”. Amewaalika viongozi wa kisiasa na kijamii, na viongozi wa serikali kujitambua kama ndugu ili pasiwepo na uongozi ambao unaondoa mwingine, badala la yake uongozi uwe kwa mfano wa Yesu wakati wa karamu yake ya mwisho alipovua nguo zake na kuwaosha miguu wafuasi wake.

Kwa kuwa na utambuzi wa nguvu ya maneno, kiongozi huyo amewaalika kuyadhibiti, kwani hayo yanaweza kuponya, kujenga, kutia moyo, lakini pia yaliyojazwa chuki na kiburi na kuleta uharibifu, aidha Askofu amerudia kusema kwamba “Kanisa halitachoka kufanya kazi kwa ajili ya amani”, akisisitizia hitaji la ufundishaji wa amani na msamaha. “ Upole, huruma na upendo ni nyenzo za kujenga ustaarabu wa upendo, amani na upatanisho. “Hatuhitaji manabii wa chuki, hatuhitaji wamisionari wa chuki, tunahitaji watumishi wa maisha, na  wa msamaha. Kama vile tunavyohitaji madaktari na wauguzi kutusaidia kushinda Covid- 19 na magonjwa mengine, tunahitaji dawa kwa ajili ya roho” amehitimisha.

14 September 2020, 18:17