Tafuta

BANGLADESH-uchumi-utunzaji bora wa mazingira BANGLADESH-uchumi-utunzaji bora wa mazingira 

Bangladesh:mazungumzo ya kidini kuhusu kipindi cha utunzaji wa kazi ya uumbaji!

Jitihada za kulinda kazi ya uumbaji zina umuhimu mkubwa hasa nchini Bangladesh,ambayo iko kwenye mabonde ya mafuriko ya mto mkubwa kuliko yote ulimwenguni,ambayo huingia kwenye Ghuba ya Bengal,mita chache juu ya usawa wa bahari.Wanasayansi wanasema kuwa taifa la watu zaidi ya milioni 160 ni moja ya maeneo yaliyo hatarini zaidi ulimwenguni kwa kuzingatia kuongezeka kwa kiwango cha bahari.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Sayari hii siyo ya kwetu. Mungu mwenyezi alitupatia jukumu la kuitunza ardhi yetu na siyo kwa ajili tu ya kula au kujifurahisha. Licha ya hayo tumeitumia kwa mitindo mingi na ndiyo maana majanga ya ajabu yanaangukia juu yetu. Ndiyo mawazo ya hivi karibuni ya Askofu Gervas Rozario, wa jimbo katoliki la  Rajshahi na Makamu Raiswa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Bangladesh aliyotoa tarehe 17 Septemba 2020. Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari za Kanisa (UCA) Askofu Rosario amesema hayo katika fursa ya mkutano kwa njia ya mtandao uliokuwa unaongozwa na kauli mbiu “mazungumzo ya kidini kuhusu Kazi ya Uuumbaji/ kuzuia mabadiliko ya tabianchi na majanga”.

Katika mkutano huo wa masaa mawili na nusu kwa njia ya mtando ulifanyika kuunga mkono  katika kusherehekea Kipindi cha Kazi ya  Uumbaji na  mwezi wa maombi  ambao unawaalika Wakristo bilioni 2.2 wa sayari hii kutunza kazi ya uumbaji wa Mungu, iliyoandaliwa na Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Katoliki(ECJP), World Vision ya Bangladesh na shirika la kibinadamu la Kikristo, wameshiriki viongozi wa dini na mashirika wapatao 80 na mashirika  mbalimbali ya kidini  ambao wametoa ahadi za kujitoa kukuza maombi na umoja, wakati huo huo kuanzisha hata vitendo vya pamoja vya utunzaji wa mazingira na shughulikia matokeo ya kutisha ya mabadiliko ya tabianchi na majanga ya asili.

Hata Mchungaji John S. Karmokar, msaidizi mkuu na katibu wa Kanisa la Ubatizo la Sangha nchini humo, pia amesema Wakristo wana jukumu la kutunza na kuhifadhi mazingira. “Sisi Wakristo ni jamuiya ndogo huko Bangladesh, lakini tunaweza kuchukua jukumu muhimu katika kuhifadhi mazingira. Ikiwa tutafanya kazi pamoja na kushiriki mawazo yetu, mipango na matendo yetu yatakuwa na nguvu na ufanisi zaidi”.

Jitihada hizi za kulinda kazi ya uumbaji zina umuhimu mkubwa hasa nchini Bangladesh, ambayo iko kwenye mabonde ya mafuriko ya mto mkubwa kuliko yote ulimwenguni, ambayo huingia kwenye Ghuba ya Bengal, mita chache juu ya usawa wa bahari. Jiografia hii ya kipekee inaifanya nchi iwe katika hatari ya kukumbwa na majanga ya asili mara kwa mara, pamoja na vimbunga vikali, mafuriko na mmomomyoko wa mito. Wanasayansi wanasema kuwa taifa la watu zaidi ya milioni 160 ni moja ya maeneo yaliyo hatarini zaidi ulimwenguni kwa kuzingatia kuongezeka kwa kiwango cha bahari kutokana na kuyeyuka kwa barafu za nchi ya Kaskazini, kwa sababu ya joto na mabadiliko ya tabua nchi.

Ikumbukwe kwamba Kipindi cha Kani ya Uumbaji 2020 kilianza mnamo 1 Septemba, katika fursa ya Siku ya Kuombea Kazi ya Uutunzaji wa Mazingira nyumba yetu ya pamoja na ambacho kitahitimishwa tarehe 4 Oktoba, katika siku kuu ya Mtakatifu Francisko wa Assisi, mtakatifu mlinzi wa ikolojia. jSiku moja kabla ya sikukuu hiyo yaani tarehe 3 Oktoba 2020 Papa Francisko anatarajia kuadhimisha Ibada ya Misa takatifu majira ya jioni katika Kanisa lililoko chini ya Kanisa kuu la Mtakatifu Francisko wa Assisi, mjini Assisi, Italia. Katika siku hiyo anatarajia kutia sahini Waraka wake wa Kitume unaoongzwa na kichwa cha habari “Fratelli Tutti”, yaani “Wote ni Ndugu”: Kuhusu Udugu na Urafiki wa Kijamii”. Na Waraka huu utatangazwa kwa umma tarehe 4 Oktoba 2020 katika Sikukuu ya Mtakatifu Francisko wa Assisi mwenye sifa kuu ya usimamizi wa ekolojia.

19 September 2020, 15:27