Tafuta

Vatican News
Askofu Mstaafu Linus Okok Okwach: 20 Oktoba 1952 - 13 Septemba 2020. Askofu Mstaafu Linus Okok Okwach: 20 Oktoba 1952 - 13 Septemba 2020. 

Askofu Mstaafu Linus O. Okwach: 20 Oktoba 1952-13 Septemba 2020

Marehemu Askofu mstaafu Linus Okok Okwach alizaliwa mwaka1952 huko Ojola, Kisumu. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 10 Desemba 1980. Tarehe 18 Oktoba 1993, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Homa Bay na hatimaye, akawekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 31 Desemba 1993. Tarehe 20 Februari 2002 akang’atuka kutoka madarakani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Askofu mstaafu Linus Okok Okwach wa Jimbo Katoliki la Homa Bay, nchini Kenya aliyefariki dunia, tarehe 13 Septemba 2020, atazikwa kwenye Kanisa kuu la Jimbo Katoliki la Homa Bay, Jumanne, tarehe 22 Septemba 2020. Itakumbukwa kwamba, Marehemu Askofu mstaafu Linus Okok Okwach alizaliwa tarehe 20 Oktoba 1952 huko Ojola, Kisumu. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 10 Desemba 1980 akapewa daraja Takatifu ya Upadre.

Tarehe 18 Oktoba 1993, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Homa Bay, Kenya na hatimaye, akawekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 31 Desemba 1993. Tarehe 20 Februari 2002 akang’atuka kutoka madarakani. Jumapili tarehe 13 Septemba 2020 akafariki dunia kwenye Hospitali ya St. Monica, Jimbo kuu la Kisumu baada ya kuwaongoza, kuwafundisha na kuwatakatifuza watu wa Mungu kama Padre kwa miaka 39 na Askofu kwa miaka zaidi ya 26.

Msiba Kenya
19 September 2020, 15:48