Tafuta

Vatican News
2020.08.08 mfuko wa Kanisa la Marekani kwa ajili ya Kanisa la Afrika  2020.08.08 mfuko wa Kanisa la Marekani kwa ajili ya Kanisa la Afrika  

Zambia#coronavirus:Ombi la maaskofu ili kusaidia maskini na waathiriwa zaidi!

Kutokana janga la virusi vya corona vinavyoendelea kusambaa katika jamii mbali mbali za nchi ulimwenguni na kuongezea madhara makubwa ya kijamii,kiuchumi na kiafya,Askofu Hamungole nchini Zambia anaomba watu wenye mapenzi mema kuwasaidia maskini zaidi na walioathirika kwa kutoa kadiri ya kile ambacho kipo hata kidogo.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni kesi 12.025 kwa ujumla walioambukizwa na virusi vya corona nchini Zambia mahali ambapo pia wanahesabu tayari vifo vya watu 300. Kwa maana hiyo Kanisa mahalia kwa njia ya Askofu Moses Hamungole, wa jimbo katoliki la Monza ametoa wito kwa waamini wote na wenye mapenzi mema  misaada ili iweze kuongezeka zaidi hasa kwa ajili ya kusaidia na kupunguza mateso kwa maskini zaidi na walioathirika zaidi.

Kwa kusisitiza zaidi: “Hakuna chochote kilicho kidogo hata kwa kwacha  2 tu (zenye thamani ya senti 10 za euro) zinaweza kufanya makubwa kudhibiti njaa", ameeleza Askofu Hamungole kama anavyotajwa na shirika la habari katoliki Afrika (Cisanews Africa). Kwa ujibu wa Askofu anaongeza kusema “Ikiwa Janga la covid-19 litaendelea kurarua jumuiya, madhara yake hayatakuwa ya akiafya tu kwa watu, lakini pia hata katika sekta za kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa sababu watu wengi wamepoteza kazi wakati gharama za maisha zimeongezeka”.

Na wakati huo huo Askofu Hamungole, ameungwa hata mkono kutoka wafanyabiashara wengine mahalia ambao wametoa misaada kwa Kanisa ili kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya corona. “Kanisa limeitikia mwito wa kuchukua hatua ili kufikia jamii yenye usawa zaidi na limeonyesha ukweli huo kwa dhati hasa  kwa kutoa mavazi, chakula, umakini na utunzaji kwa wale ambao vinginevyo wasingeweza kupata na kuridhika kwa mahitaji haya”. Ni kwa mujibu watoa hisani kuhusiana na umakini wa Kanisa kwa ajili ya wenye shida. Msaada wa  wafadhili uliyopokelewa utasambazwa katika majimbo yote 11 Katoliki nchini Zambia, pamoja na mihimili mingine ya kiekumene, kama vile Baraza la kitaifa la Makanisa.

03 September 2020, 11:33