Tafuta

Utume wa uinjilishaji wa habari unatakiwa uendane na na uaandaji wa vijana watakaokuwa mahiri katika uenezaji wa habari za mafundisho ya kikanisa na kijamii. Utume wa uinjilishaji wa habari unatakiwa uendane na na uaandaji wa vijana watakaokuwa mahiri katika uenezaji wa habari za mafundisho ya kikanisa na kijamii. 

Amecea:waandishi katoliki wakumbuke kuwa ujumbe ndiye Mfalme na ushiriki ni Malkia!

Waandishi wa habari Wakatoliki wahimizwa kuzingatia ujumbe na kukagua ukweli katika habari wanazozitoa kwa Umma.Akiwahutubia wakurugenzi wa Radio takribani 50 katoliki uliofanyika mtandaoni Kaimu Mtendaji wa wa AMECEA Padre Emmanuel Chimombo amewakumbusha kuwa makini katika kuchambua ujumbe wanaokusudia uifikie umma pamoja na mazingira yake kwani kiuandishi amekumbusha“ujumbe ndiye Mfalme na ushiriki ni Malkia”.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kaimu Mtendaji wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki (AMECEA) Padre Emmanuel Chimombo amewataka waandishi wa habari Wakatoliki kuwa makini katika ujumbe wanaoutuma kwa njia ya habari ili taarifa wanazozitoa ziweze kuthaminiwa. Akiwahutubia kwa wakurugenzi wa Radio mbalimbali  takribani 50 katika mkutano uliofanyika mtandaoni ukijumuisha washiriki kutoka nchi za Uganda, Tanzania, Malawi, Zambia na Kenya, Padre Emmanuel Chimombo amewakumbusha waandishi wa habari wa kikatoliki kuwa makini katika kuchambua ujumbe wanaokusudia uifikie umma pamoja na mazingira yake kwani kiuandishi “ujumbe ndiye Mfalme na ushiriki ni Malkia”.

Hata hivyo katika kuendela na mada hiyo Padre Chimombo hakukosa kuwaangalisha juu ya malalamiko yanayojitokeza juu ya ujumbe unaotolewa na wana habari. Akifafanua maada hiyo Padre Chomombo amekazia juu ya utume wa uinjilishaji wa habari unaoendana na uaandaji wa vijana watakaokuwa mahiri katika uenezaji wa habari za mafundisho ya kikanisa na kijamii. Hata hivyo ameahakikishia kwamba maaskofu wanajikita katika utatuzi wa mada zinazoibuka kila siku na kusisitiza kujenga daraja kati ya vyombo vya utendaji wa haki, uwajibikaji katika uongozi, na utunzaji wa mazingira.

Naye Padre Anthony Makunde Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki (Amecea) katika ufunguzi wa hotuba yake amesisitiza juu ya mchango wa mazingira husika katika utoaji wa maadili. Katika mkutano huo aidha watoa mada walikuwa kadhaa ambapo  mwakilishi kutoka nchi ya Malawi ameelezea umuhimu wa Kanisa kujihusisha na uenezaji wa habari kwa kunukuu tamko la Mtaguso wa II wa Vatican juu ya vyombo vya habari.

Mkutano huo ulifanyika kwa siku mbili ya tarehe 16 na 17 Septemba 2020 ambapo Kamati ya Mtandao wa Mawasiliano kutoka kenya (KCOMNET) ulifanyika katika kutathimini juu ya upotoshaji wa habari unaofanyika ndani ya Shirikisho la Baraza la Maaskofu la nchi za Afrika Mashariki. Padre Andrew Kaufa amebainisha tabia geugeu ya baadhi ya waamini kuonesha moyo wa ibada siku za Dominika na kuishi kinyume kabisa cha maadili ya Mungu kwa siku za kawaida.  Na mwisho katika Majadiliano yanayoonesha kukengeuka kwa waandishi wa habari huku wakiacha msingi na maelekezo ya Mtanguso mkuu wa pili wa Vatican, washiriki wa Mkutano huo wameweza kuamsha mori mpya katika Tasnia ya habari kwa nchi za Afrika Mashariki.

22 September 2020, 15:26