Tafuta

Vatican News
Matatizo ni mengi hata ya maji katika mji wa Harare nchini Zimbabwe Matatizo ni mengi hata ya maji katika mji wa Harare nchini Zimbabwe  (ANSA)

Zambia:Maaskofu wapongeza ujasiri na nafasi ya kinabii ya Kanisa

Maaskofu nchini Zambia wanapongeza ujasiri wa nafasi ya kinabii wa Kanisa nchini Zimbabwe katika kipindi cha sasa cha mgogoro unaoendelea wa kiuchumi, kijamii na kiafya.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Hata maaskofu katoliki nchini Zambia wanaonesha mshikamano wao kwa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Zimbabwe, kufutia na mashambulizi makali  ya maneno kutoka kwa Serikali ya Harare kutokana na kutokubali kukoselewa  dhidi ya maandamano ya watu  kutokana na usimamizi mbaya wa mgogoro wa kiafya na kiuchumi nchini humo. Katika ujumbe wa Maaskofu uliotolewa kwenye Blog ya Shirikisho la mabaraza ya maaskofu Afrika Mashariki(AMECEA) Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Zambia  (Zccb), Askofu  George Lungu, anapongeza ujasiri wa nafasi ya kinabii ya maaskofu wa Zimbabwe katika barua yao ya hivi karibuni tarehe, 14 Agosti 2020 ikiangazia wahusika katika hali halisi ya sasa ya mgogoro wa kiuchumi na kiafya katika nchi kwa kupinga vikali haa suala la kipekee janga la ufisadi.

Katika barua hiyo inasema : “Kama Baraza la Maaskofu wa Zambia tunashirikishana uchungu ambao sehemu kubwa ya wazimbabwe wanajumuishwa hata maaskofu wakatoliki, ambao wanaishi kipindi hiki kwa sababu sisi sote tu kiungo cha familia moja ya Mungu. Kama asemavyo Mtakatifu Paulo Mtume kuwa ;“ikiwa kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho. Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo,  (1 Cor12,26-27)”. Ujumbe wao kwa maana hiyo unaonesha matumaini mema ya kwamba serikali na watu wote nchini Zimbabwe wasiache njia ya mazungumzo ya dhati ili kutatua changamoto ambazo wanapaswa kukabiliana nazo.

Katika waraka huo wanaandika: “Sisi, kwa upande wetu, tutaendelea kuombea hili haimaye ipatikane amani kutokana na  mgogoro”,  anahitimisha Rais wa Baraza la Maaskofu wa Zambia ambaye anawashauri  “dada na kaka wa Zimbabwe wasipoteze tumaini, kwa sababu Mungu hajawahi kuacha na kamwe hataacha zizi lake”.  Mshikamano wa maaskofu wa Zambia unafika pamoja na ule uliooneshwa Jumapili iliyopita tarehe 16 Agosti 292 kutoka kwa Balozi  wa kitume  Askofu Mkuu Paolo Rudelli, ambaye binafsi alimwonesha  kwa kumtembelea Askofu Mkuu Robert Christopher Ndlovu wa jimbo katoliki la Harare, na msaada wake kwa maaskofu wote wa nchi, aidha ukaribu  ulioonyeshwa kutoka kwa Baraza la Maaskofu nchini Afrika Kusini (Sacbc), kutoka  Mkutano wa Kanda ya  Maaskofu wa Afrika Kusini (IMBISA) na Makanisa mengine ya Kikristo ulimwenguni.

24 August 2020, 12:04