Tafuta

Vatican News
2020.06.10 -HUU NDIYO MWEILI WA YESU KATIKA EKARISTI 2020.06.10 -HUU NDIYO MWEILI WA YESU KATIKA EKARISTI 

Uruguay-Siku ya Kitaifa ya Katekesi:Twaeni na mle:huu ndiyo mwili wangu!

Asante Mungu kwa kuwaita,kuwachagua,kuwa wahudumu wa Ufalme wa nchi,kwa ajili ya ukarimu wao,ishara ya upendo wa Mungu kwa maisha yao.Ndiyo shukrani ya Askofu Msaidizi wa jimbo la Montevideo nchini Uruguay kwa kuwapongeza makatekista katika siku ya Katekesi kitaifa iliyofanyika Jumapili tarehe 23 Agosti 2020 nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

“Twaeni na mle: huu ndiyo mwili wangu” ndiyo mada iliyochaguliwa na Kanisa kwa ajili ya kuongoza Siku ya Kitaifa ya Katekesi tarehe 23 Agosti 2020 nchini Uruguay. Katika fursa ya siku hiyo, Askofu msaidizi Pablo Jourdan, wa Jimbo katoliki la Montevideo na mhusika wa kitengo cha Katekesi cha Baraza la Maaskofu nchini humo, ametangaza ujumbe wake kuwalenga makatekista wote wa nchi huku akimshukuru Mungu kwa kuwaita, kuwachagua ili wawe wahudumu wa Ufalme wa nchi, kwa ajili ya ukarimu wao ambao ni  ishara ya upendo wa Mungu katika maisha yao.

Katika mwaka huu ambao kwa namna ya pekee unajikuta katika janga la virusi vya corona, vilivyoonea ulimwenguni kote anasema Askofu Jourdan kwamba: “ maisha yetu yamezingirwa  na  kile tulichokuwa tumepanga kimeweza kuenenda na hali halisi hii mpya”. Kwa maana hiyo Katekesi imeweza kuendelea kulingana na hali halisi katika  kutafuta njia bunifu  mpya na njia mpya za kutembea kwa pamoja karibu na makatekista huku wakisindikizwa na hali halisi tofauti za familia,na  kumshukuru Mungu na Kanisa lake ambalo lipo katika wakati usio kuwa na uhakika na usalama.

Pamoja na hayo yote, Askofu msaidizi wa jimbo la Montevideo, amebainisha kuwa wanao utambuzi kwamba kila wakati “Bwana anatenda na anakuwapo katikati ya watu wake wanaoteseka. Katika wimbi hili kama alivyosema hata Papa Francisko limetufanya tutambue kuwa “ sisi sote tumo ndani ya mtumbwi mmoja, mdhaifu na tusiokuwa na mwelekeo, na wakati huo huo lakini wenye kuhitajiana mmoja na mwingine na wanaoalikwa kupiga kasia pamoja”.

Askofu anatoa matashi yake kwamba mwaka huu licha ya yote yanayoendelea ya janga la virusi lakini uwe ni kipindi muafaka cha neema kwa ajili ya katekesi, ambamo tafakari na kuishi kunaleta pamoja chachu ya kazi zao. “Kama watu wa Mungu katika safari ya hija kwenye ardhi hii, hatuwezi kusimama, sala zetu na upendo wetu lazima ubaki hai na ushuhudie Mungu ambaye anajifanya kuwa karibu na ambaye anabaki katikati ya Kanisa lake kwa njia ya eukaristi , sakramenti ambayo tumejifunza kuthamanisha kwa kiasi kikubwa kwenye  nyakati hizi.

25 August 2020, 14:06