Tafuta

Vatican News
2020.01.28 Wakatoliki na walutheri 2020.01.28 Wakatoliki na walutheri 

Shirikisho la Kilutheri ulimwenguni:kumbatia wakati ujao kwa kujifunza kupitia maumbile!

Shirikisho la Kilutheri ulimwenguni(Lwf) limeandaa safu za mikutano kupitia mtandaoni kwa madhimuni ya kutaka kukumbatia wakati ujao kupitia kijifunza kutokana na maumbile. Mikutano hiyo inaongozwa na jina:“Kuwa Walutheri”. Ni katika muktadha wa maandalizi ya Mkutano wao mkuu utakaofanyika Septemba 2023 jini Krakow nchi Poland.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika swali la nini maana ya kuwa Mlutheri katika karne ya XXI, ndilo linaloibua safu za mikutano inayoongzwa na kauli mbiu: “Kuwa Walutheri”. Hii siyo kutaka kutoa majibu kama safu ya mambo mengi ya kutafakari bali ni juu ya kutaka  kuimarisha uelewa wa utambulisho wa Walutheri unaolenga utume wao wa  kutangaza Neno la Mungu kwa mtazamo wa uekumeni, kwa mujibu wa waandalizi wake. Mikutano hii ya moja kwa moja kupitia mtandaoni, imependekezwa na Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni (Lwf), kuanzia kila Jumatano ya kwanza ya kila mwezi ili kuwasilisha maoni tofauti ya kitaalimungu na hali ya kiroho ya Kanisa la Kilutheri kwa kuzingatia uzoefu wa jumuiya mahalia.

LWF 2023, Crakow, Poland:“Mwili Mmoja, Roho Moja, Tumaini Moja”

Mfululizo huu wa mikutano ni mojawapo ya matokeo ya mkutano wa kimataifa “We believe in the Holy Spirity: global perspectives on lutheran identities”, yaani “Tunaamini katika Roho Mtakatifu: mitazamo ya ulimwengu juu ya vitambulisho vya Kilutheri”, ambao ulifanyika mwezi Oktoba mwaka jana huko Addis Ababa nchini Ethiopia na ili kuendelea kuhamasisha kufikiria tena yale ambayo Walutheri wanapaswa kufanya ulimwenguni na zaidi ya hayo kuonesha uwepo kikristo. Matarajio hayo yote ni katika maandalizi ya mkutano mkuu ujao wa Shirikisho hilo LWF uliopangwa kufanyika Septemba 2023, jijini Krakow, nchini  Poland, ambapo wataongozwa na kauli mbiu: “Mwili Mmoja, Roho Moja, Tumaini Moja”. Hata hivyo katika mji mkuu wa Ethiopia wakati wa mkutano wao ilijitokeza umuhimu si tu kwa Kanisa la Kilutheri kuweza kushughulikia njia nyingi ambazo utamaduni unadhihirishwa pamoja,  lakini pia hata utofauti unaowezesha utambulisho wa Kilutheri na safari ya kushirikishana ya kiekumene  katika utafutaji wa pamoja  wa kila siku wa urithi wa imani.

Wakristo wawe mashuhuda wa tumaini ulimwenguni

Wazo la kukabiliana na utofauti huu limechukua thamani fulani wakati wote hasa katika kipindi cha janga la covid-19  ambalo limewataka Wakristo wawe  mashuhuda  wa tumaini ulimwenguni, kuzaliwa upya na kuwafanya waelewe maumivu, mateso na ubaguzi unaosababishwa na Covid-19! Katika kila mkutano mada itawasilishwa na msemaji mmoja au zaidi, huku wakiacha nafasi kulingana  na  jinsi inavyoonyeshwa katika muktadha tofauti. Katika mkutano wa kwanza tarehe 5  Agosti 2020  kwa mfano, walikabiliana na masuala yanayohusiana na uhusiano kati ya mafunzo na habari katika jamuiya mahalia. Madhumuni yao makuu yalikuwa ni mwaliko wa kutoa kipaumbele cha matendo ya kiekumene  kwa ajili ya Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni, kwa mujibu wa mapokeo ambayo zamani yalikuwapo, kwani tangu kuanzishwa kwake kunako mwaka 1947 huko Lund, chombo hiki kimejikita katika ujenzi wa ‘umoja’ kama malengo yake makuu.

Kumbu Kumbu ya Mageuzi imeonesha hatua msingi ya ukristo wa karne ya 21

Maadhimisho ya kumbu kumbu ya miaka miatano ya mageuzi ya kilutheri yameoneshwa wazi ule umuhimu wa ukristo wa karne ya 21, wenye uwezo wa kuishi umoja katika utofauti, katika upatanisho na katika kumbukumbu za kurudisha utajiri wa mafundisho ya kina na ya kiroho katika tamaduni za kikristo. Pamoja na mpango huo wa mikutano ya kila mwezi juu ya “kuwa mluther”,  Shirikisho la Kilutheri ulimwenguni (LWF) linapendekeza uimarishwaji wa utambulisho wa Walutheri kwa kushiriki kwa wingi katika utamaduni  ambao, tangu 1947, wamekuwa wakishirikishana kwa mtazamo wa umoja.  Kuimarisha utambulisho wa Walutheri kunawakilisha hatua msingi katika safari ya kiinjili na kiekumene ambayo inawataka Wakristo  wote kuishi pamoja ile zawadi za Kristo.

21 August 2020, 13:59