Tafuta

Vatican News
Chama cha Kiristo nchini Nigeria kinawaalika waamini wakristo na wenye mapenzi mema kufanya sala ya kiekuemene tarehe 23 Agosti kwa ajili ya nchi yao. Chama cha Kiristo nchini Nigeria kinawaalika waamini wakristo na wenye mapenzi mema kufanya sala ya kiekuemene tarehe 23 Agosti kwa ajili ya nchi yao. 

Nigeria:Tarehe 23 Agosti siku ya maombi ya kiekumene kwa ajili ya usalama wa nchi!

Chama cha Kikristo (CAN) nchini Nigeria kinaomba waamini wote na wenye mapenzi mema tarehe 23 Agosti 2020 kusimama kwa dakika 15 kwa pamoja kufanya sala kwa Mungu kuliombea taita la Nigeria ambalo limnazidi kukabiliwa na mauaji na kutumia nguvu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Chama cha Kikristo nchini Nigeria (CAN) kimetangaza kufanya Siku ya sala ya kiekumene kitaifa ili kuomba Mungu awasaidie  nchi hiyo kuondokana na hali mbaya ya kukosa  usalama. Siku iliyopendekezwa ni tarehe 23 Agosti 2020 ambapo wanaalika waamini  wote na watu wenye mapenzi mema kujikita kwa uhai wote kuomba Mungu Baba Mwenyenyezi.

Mapenzi ya Mungu yatimie nchini Nigeria

Katika taarifa kwa namna ya pekee iliyotiwa sahini na Katibu Mkuu  Daramola Joseph Bade, wajumbe wa CAN wameomba makanisa yote nchini humo katika tarehe hiyo kwa dakika karibu 15 angalau  kijikita kwa ajili ya sala ya pamoja katika lengo moja hilo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo lengo lake ni lile la kumwomba Mungu kwa sauti moja ili mapenzi yake yatimie nchini Nigeria. Kwa mujibu wa taarifa hiyo inaeleza kuwa jambo hilo sio kwa mara ya kwanza kwa Chama hiki Can kupendekeza ushauri wa namna hii, kwani mwaka huu 2020  kwa hakika kiungo hiki kimeomba mara nyingi sala kwa ajili ya kuponywa na mapatano kitaifa, hasa hivi karibuni katika muktadha mgumu wa janga la covid-19 ambalo limegandisha nchi nyingi ujumla ulimwenguni.

Chama cha kikristo Nigeria ni kikubwa katika Afrika Magharibi

Chama hiki cha kikristo (CAN) nchini Nigeria ni kiungo kikubwa sana cha kiekumene  katika Afrika ya Magharibi na kinaunganisha makundi tofauti kitaifa, miongoni mwake ni pamoja na baraza la Kikristo, Sektretarieti Katoliki, Kanisa la kipentekoste na lile la kiinjili.

Tarehe 22 Agosti hadi 30 Septemba , siku 40 za sala

Hata hivyo ni lazima kukumbuka kuwa tarehe 22 Agosti hadi tarehe 30 Septemba 2020 watawafanya siku 40 za maombi kwa Mungu  zilizotangazwa na Baraza la Maaskofu kitaifa  kwa ajili ya kumwomba Mungu msaada wa kumaliza muktadha huo wa kutumia nguvu  na mauaji ambapo kwa walio wengi wameelezea  kama mauaji ya kimbari. Katika miezi ya hivi karibuni, kiukweli makundi tofauti ya kijeshi yamekumbana na mashabulizi tofauti, utekaji nyara na mauaji na mara nyingi walengwa ni wakristo. Kutoka hata katika Makanisa mahalia viongozi wake  wametoa wito wa mara kwa mara  kwa serikali ili iweze kuingilia kati kwa uamuzi sahihi kusitisha hali hii ngumu sana katika nchi hiyo. 

18 August 2020, 12:28