Tafuta

Vatican News
Maaskofu nchini Afrika Kusini wakemea serikali kufuatia na utapeli wa mfuko wa fedha kwa ajili ya dharura ya janga la corona Maaskofu nchini Afrika Kusini wakemea serikali kufuatia na utapeli wa mfuko wa fedha kwa ajili ya dharura ya janga la corona 

Afrika Kusini:Maaskofu wasikitishwa na utapeli wa mfuko wa Covid-19!

Maaskofu nchini Afrika Kusini wamekeme serikali kuhudu utapeli wa mfuko wa fedha kwa ajili ya covid-19 na wanasema ni lazima kuimarisha imani kwa watu katika wakati huu wa janga kutokana na ahadi za rais aliyeko madarakani za kuzuia rushwa na ufisadi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kufuatia na tukio kutapeliwa kwa mfuko wa  Covid-19, maaskofu nchni Afrika Kusini wanasikitishwa  na kusema “Wakati tunashtushwa sana, habari za uporaji wa rasilimali za umma wakati wa janga la virusi vya corona, lakini siyo  kwa mshangao mkubwa. Tunawasihi viongozi wetu kuzingatia kwa uangalifu jinsi walivyoruhusu utamaduni wa kutokujali rushwa na kuuendeleza na kwa njia  hiyo kujenga mazingira mazuri ya kutekeleza vibaya mfuko wa fedha kwa ajili ya  COVID-19”. Kadhalika  waaandika katika taarifa yao  Maaskofu wa Afrika Kusini juu ya kesi kubwa za utapeli na ufisadi kwenye pesa zilizotengwa kutibu wagonjwa wa janga la corona  na kuzuia janga hilo. “Katika miaka iliyopita, licha ya tuhuma nzito, hapakuwapo  na kukamatwa,  wala kesi za mahakama kwa wanasiasa na familia zao”.  

Mikataba mibaya ya viongozi wa serikali na kampuni za kusambaza vifaa

Nchini Afrika Kusini, ambayo ina zaidi ya nusu milioni ya kesi ya maambukizi ya  COVID-19, ripoti imeonesha mikataba mibaya kati ya viongozi wa serikali na kampuni zinazosambaza vifaa vya matibabu, pamoja na vifurushi vya misaada ya chakula kwa maskini. Wauguzi wamelalamikia upungufu mkubwa wa PPE na matokeo yake kusababisha kuongezeka kwa maambukizo kati ya wafanyakazi na wagonjwa wengine hospitalini.

Katika matokeo ya ufisadi imani ya raia imepungua kwa viongozi

Maaskofu wamemgeukia Rais Cyril Ramaphosa, ambaye alikuwa ameahidi kukomesha ufisadi baada ya kashfa za mtangulizi wake, Jacob Zuma. “Ni wazi kuwa kashfa ya hivi sasa ya ufisadi imeondoa kabisa  imani ya maoni kwa  umma katika ofisi ya Rais na uwezo wake wa kumaliza saratani ya rushwa ambayo inaendelea kurarua  roho ya taifa letu”, wanasisitiza maaskofu. Kwa njia hiyo  maaskofu wanasema “tunaomba Rais achukue hatua za ujasiri kurudisha imani ya wazalendo  katika urais kama taasisi.”

Raia hawawezi kuvumilia vitendo vya serikali na ofisi ya rais

Maaskofu wa Afrika Kusini aidha wanasema “ufanisi wa vita vya sasa dhidi ya janga la corona na kushuka kwa uchumi unahitaji uingiliaji wa haraka wa rais ambaye una uwezo wa kuchota kutoka  katika ngazi kubwa ya umma. Katika kipindi hiki chote kigumu cha taifa letu ambapo maisha ya mamilioni ya watu yamo hatarini, nchi haiwezi kuvumilia upungufu mkubwa wa imani kwa serikali katika ofisi ya Rais”, inabainisha taarifa hiyo. Maaskofu wanahitimisha kwa kuomba kurudishwa kwa kitengo maalum cha kupambana na rushwa cha Polisi (Scorpions) na uimarishaji wa mahakama maalum katika kesi za rushwa.

20 August 2020, 14:57