Tafuta

Vatican News
2020.02.06 Zambia Malawi Zimbabwe Bishops with Zambian Republican President 2020.02.06 Zambia Malawi Zimbabwe Bishops with Zambian Republican President 

Zambia:Maaskofu kuwaalika wananchi kuomba Mungu zaidi katika wakati huu!

Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Zambia (ZCCB) limewataka wananchi wa Zambia kumtafuta Mungu kipindi hiki cha janga la Corona lakini wakati huo huo kwa kufuata sheria za kujilinda na kulindwa wengine.

Na Sr. Angella Rwezaula -Vatican

Baraza la Maaskofu nchini Zambia (ZCCB) limetoa tamko lao likiwataka waamini kuendelea kumfuata Mwenyezi Mungu. Tamko hili limetolewa na Rais wa Baraza hilo Maaskofu nchini Lusaka, Zambia. Katika tamko hili, Maaskofu Katoliki wanasema, Mwenyezi Mungu na huruma yake ameingilia kati na ataendelea kuwa kati ya watu ili awaokoe.   Kwa kutumia  mfano wa Kristo wakati akituliza dhoruba katika Injili ya Mtakatifu Marko (Mark 4:35-41) ambapo mtumbwi aliopanda Yesu na Mitume wake ulipoanza kuzama, wanafunzi walimwamsha Yesu na kumwomba awaokoe na Yesu aliiamuru dhoruba hiyo itulie nayo ikamtii mara!

Aidha, Rais  Baraza la Maaskofu amwatahadharisha watu waache tabia ya kumjaribu Mungu huku wakimwomba aliondoe janga la Corona bila kuchukua tahadhari yoyote.  Akiwaalika wanachi wote wa Zambia amewaomba watu kujenga umoja na kupambana na  adui mkubwa  anayetishia maisha ya watu. Na zaidi ikiwa hatua hii itafikiwa kwa   wananchi kutilia maanani ya kujikinga na kupunguza safari zisizo za lazima. Kanisa pia limeiomba Serikali kutoa vifaa vya kujikinga (PPE) na huduma zingine za Afya ili kupambana ipaswavyo na janga hilo la Ugonjwa wa Corona.  Mwisho Askofu George Lungu ameelezea hatua za Kanisa zilizochukuliwa kwa kusimamisha baadhi ya shughuli za kiuchungaji katika majimbo na kuacha tu zile kazi za lazima ambazo haziwezi kusimamishwa kamwe.

Caritas nchini Zambia imehamasisha Waandishi wa Habari kutoka sehemu mbali mbali za vyombo vya habari nchini humo ili kuwapa mafunzo juu ya jinsi ya kukuza kazi ya utetezi unaozungukia mbegu za kisiasa, mabadiliko ya tabia nchi na lishe.  Mtaalam wa mazingira ya kuishi wa  Caritas  nchini Zambia na mtaalam wa Programu ya Mabadiliko ya Tabianchi , Mubanga Musamba ameelezea maendeleo hayo kuwa

Kwa mujibu wa Caritas inasema"Kwa kushirikiana na PELUM Zambia, CSO SUN, Caritas Zambia itakuwa ikitoa mafunzo kwa waandishi wa habari 25 katika nyanja za siasa, mabadiliko ya hali ya tabianchi  na mazingira pamoja na lishe. Hii itafanyika kuanzia tarehe 28 hadi 29 Julai 2020 katika Nyumba ya Wageni ya Kapingila huko Lusaka”

Kwa mujibu wa Bi Mubanga zaidi alisema mafunzo hayo pia yanalenga kupata msaada, kuongeza mwamko, shauku na kwa wanahabari kuelewa kwa kina mbegu za kisiasa, mabadiliko ya tabia nchi na mazingira pamoja na lishe. “Mafunzo haya yameandaliwa kwa ajili ya  kuwajengea uwezo wa waandishi wa habari katika utetezi juu yambegu za  siasa mabadiliko ya hali ya hewa. Kusudi kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoa makala zinazoonesha  mabadiliko mazuri katika sera na mabadiliko ya tabia nchi” alisema Bi Musamba .

Katika kuleta mabadiliko ya kijamii, wanahabari ni kiungo muhimu katika kuelemisha haki za wadau na kuwapatia nyenzo za kimawasiliano ya pande zote mbili. Tasinia ya Habari inahitaji sana kujengewa uelewa juu ya nafasi ya maana ya siasa na nafasi yake katika jamii. Aidha, katika kuhitimisha, Bi Musamba amefafanua kuwa mafunzo hayo ni mwendelezo wa maandalizi ya utoaji wa tuzo kwa wanahabari utakaofanyika hapo baadaye.

28 July 2020, 15:28