Tafuta

Vatican News
2018.06.21-Papa  Francisko katika Mkutano wa Kiekuemene kwenye Kituo kikuu cha Baraza la Makanisa Ulimwenguni -WCC huko Geneva 2018.06.21-Papa Francisko katika Mkutano wa Kiekuemene kwenye Kituo kikuu cha Baraza la Makanisa Ulimwenguni -WCC huko Geneva 

Wcc na jukwaa la kidini Geneva:dharura ya kiafya na tabia nchi

Baraza la Makanisa ulimwenguni (WCC)na Jukwaa la Kidini katika mkutano kuhusu dharura za kiafya na tabianchi,ambayo ni migogoro miwili inayoungana amezitaka Serikali kulinda haki za binadamu.Tamko linahitimisha kwa mapendekezo manne ili kutambua haki ya binadamu katika mazingira salama,kuhakikisha heshima ya haki za binadamu katika utumiaji wa hatua dhidi ya Covid-19;kuhakikisha usawa na haki za kiuchumi,kufuta deni la nchi maskini na marekebisho ya mfumo wa kodi duniani.

Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Dharura ya Covid-19 na mabadiliko ya tabia nchi ni migogoro miwili ambapo katika mzizi  wake kuna mfumo wa uchumi usio stahili na ekolojia endelevu ikiwa na matokea mabaya ya kina kwa watu ulimwenguni kote na kwa ajili ya haki ya binadamu. Ndiyo tamko la pamoja lililotangazwa na Jukwaa la Kidini kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, haki za binadamu na mazingira (Gif)huko Geneva ambapo pamoja na washiriki miongoni mwake ni Baraza la Makanisa Ulimwenguni (Wcc), Wadomenikani kwa ajili ya Haki na Amani na Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni. Tamko lao limewakilishwa katika Kikao cha 44 cha Baraza la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya haki na amani kikao kinachoendelea tangu tarehe 30 Juni hadi tarehe 17 Julai 2020 huko Jijini Geneva Uswiss na mahali ambapo Jukwaa hilo katika fursa ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wameandaa hata baadhi ya semina kupitia mitandaoni ambayo imejikita katika mada kuhusu “haki ya binadamu, maadili na mabadiliko ya tabianchi”.

Migogoro miwili inayounganika kati yao:hali ya hewa na afya

Katika Hati yao ya pamoja inaonesha mgogoro miwili ya kiafya na wa hali ya hew katika ulimwengu tunamoendelea kuishi lakini pia  hata kwa ajili ya muktadha wa haki za binadamu msingi kwa walio athirika zaidi, kuanzia na ile ya afya ambalo limetazamwa na Baraza la Umoja wa Mataifa kama lengo la tatu la maendeleo endelevu (SDGs).  Wataalam wengi kwa hakika wamekwisha onesha kuwa ukame uliosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na kukosekama kwa hewa safi unaongezewa zaidi na dalili za  Covid-19 na wanathibitisha kuwa gharama kubwa zaidi kwa maana ya maisha ya binadamu, zinalipwa na wale ambao hawana fursa, kama vile masikini, wanawake, makundi ya watu walio wachache, watu wa asilia, wahamiaji na wakimbizi.

Athari za kiuchumi

Dharura hizi mbili kwa mujibu wa jukwaa hili wanathibitisa kuwa zinafanana hata kwa matokeo yake kiuchumi. Katantini imepelekea kuongezeka kwa ukosefu wa ajira na kwa maana hiyo umaskini na njaa ulimwenguni kote , lakini pia mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaendeleo kuonekana madhara yake kwa namna ya pekee wakulima, wavuvu na watu wa asilia ambao wanakosa haki ya chakula na maji pamoja na haki nyingine msingi za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Pamoja na hayo, upungufu  wa zana kiuchumi, kijamii na ambao wanaoishi pembezoni ndiyo wenye pigo hasa, kwa mujibu wa hati hiyo ya pamoja.

Wito wa kubadili sera mpya za mifumo kiuchumi

Kwa kunukuu maneno ya Papa Francisko kwenye Laudato si, Jukwaa la kidini linabainisha “mgogoro huu umefunua wazi uhusiano wetu kama ubinadamu pekee na ukweli kwamba sisi ni sehemu ya jumuiya  kubwa inayoishi, japokuwa inakumbwa na kutokujali, ubinafsi na kutegemeana kwa haki zote za binadamu na wakati huo huo kuwa na hitaji la kuwekeza kwa dhati katika mifumo ya kusaidia kulinda haki hizo”. Kwa maana hiyo wanatoa wito wa kubadilisha sera mpya na mifumo ya kiuchumi ili kukuza haki za binadamu na kusaidia afya na ustawi wa watu na sayari hii. Hii yote inajumuisha hatua zilizoratibiwa, madhubuti na za mabadiliko na Mataifa kwa kushirikiana na sekta zote za jamii, wamesisitiza.

Mapendekezo manne ya Jukwaa la kidini

Hati yao inahitimishwa kwa mapendekezo manne: kutambua haki ya binadamu katika mazingira salama, safi na yenye afya kwa wote, hasa kwa kulinda baioanuwai na kupunguza uzalishaji wa gesi chafu katika nchi zote; kuhakikisha heshima ya haki za binadamu katika utumiaji wa hatua dhidi ya Covid-19; kuhakikisha usawa  kamili na wa haki za kiuchumi, kijamii, kitamaduni, kiraia na kisiasa katika kulekea mpito wa uchumi  na jamii endelevu yenye kuwa na hewa Zero ya kaboni katika kipindi cha baada ya Covid; hatimaye, kufuta deni la nchi maskini zaidi na marekebisho ya mfumo wa ushuru duniani.

07 July 2020, 12:32