Tafuta

Vatican News
Siku ya XXXIV ya Viajan PANAMA 2019  22-27 Januari 2019 Siku ya XXXIV ya Viajan PANAMA 2019 22-27 Januari 2019 

Venezuela:Harakati za Mkutano wa Vijana na mwezi wa kimisionari!

Kanisa halina budi kuzisaidia kuweka mpangilio wa elimu katika familia ili kujinasua katika umaskini na kujipatia maendeleo,huku wakizuia mfumo mbaya wa malipo duni yanayoathiri jamii kwa ujumla.Baraza la Maaskofu Nchini Venezuela,wamesimama kidete kuweka mkakati madhubuti wa Utume wa kimisionari utakaongoza katika nyanja za kichungaji,kiuchumi na kijamii.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baraza la Maaskofu Nchini Venezuela, barani Amerika ya Kusini wamesimama kidete wakiweka mkakati madhubuti wa Utume wa kimisionari utakaongoza katika nyanja za kichungaji, kiuchumi na kijamii. Hayo yamewakilishwa katika shirika la habari za kimisionari Fides ambapo baraza la maaskofu wanakazia uwepo wa huduma za kisiasa, kiuchumi na kijamii unaounganishwa na maslahi ya umma na usalama. Kanisa halina budi kuzisaidia kuweka mpangilio wa elimu katikafamilia ili kujinasua katika umaskini na kujipatia maendeleo, huku wakizuia mfumo mbaya wa malipo duni yanayoathiri jamii kwa ujumla.

Mungu yu pamoja nanyi  hatawaacha kamwe

Katika waraka wao uliotangazwa tarehe 10 Julai 2020 wenye kauli mbiu “ Mungu yu pamoja nanyi  hatawaacha kamwe! (Kumb 31:6): ni hali halisi”, Maaskofu wa wamejikita kuelezea juu ya Kanisa la hija lililoathirika kwa uwepo wa mitafaruku mbalimbali. Wamewatia matumaini makubwa Taifa la Mungu kwamba  Mungu hawezi kuwatupa kamwe. Wakristo wanaalikwa kuijenga Venezuela ya sala kwa nguvu ya Injili na kwa kufanya kazi. Kanisa linajipambanua kuwa ni chombo kinachomjali mnyonge na kufungamana na walio wahitaji zaidi.  Katika kipindi cha janga la virusi vya Corona ambalo limesabisha madhara makubwa ulimwenguni ikiwemo vifo na kudidimia kwa nguvu ya uchumi, Kanisa linatoa mwaliko wa kusonga mbele bila kujibakiza wakiwasaidia makundi yanayohitaji zaidi kama wahamiaji na wakimbizi, maana wahamiaji wanarudi kutoka nchini mwao pasipokuwa na rasirimali na uhakika wa kuishi.

Maisha ni Utume

Naye Padre Richard Guillén Mkurugenzi wa Kitaifa wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari nchini Venezuela katika mkutano huo  amewasilisha mada yake itakayowekwa katika mkutano  Mkuu wa Baraza la Maaskofu utakaofanyika Mwezi Oktoba 2020 inayohusiana na Kampeni ya kulishirikisha Kanisa katika fursa na changamoto za sasa. Mada yenyewe inaongozwa na Kauli mbiu ya “Maisha ni Utume” inayooangaza ulimwengu katika maisha ya wakristo wanaofurahia kukutana na Mwenyezi Mungu na katika Jumuiya.

Utume wa Kanisa kutetea na kuhamasisha maisha

Padre Guillén ametangaza juu ya mitandao minne itakayosambaza utume huo. Katika kufafanua amesema, “mwezi wa kimisionari una mambo makuu manne: wito wa kitume katika kuhuisha maisha. Utume wa Kanisa ni kutetea na kuhamasisha maisha. Wakimbizi na wahamiaji, waliotengwa, na mabadiliko ya mazingira katika ulimwengu”.

Kongamano la sita la kitaifa la vijana wamisionari

Tukio jingine la uinjilishaji lililowasilishwa ni kuhusu Kongamano la Sita la Kitaifa la Vijana wamisionari litakalofanyika tarehe 21 hadi 30 Agosti 2020. Kongamano hilo litaongozwa na kauli mbiu: “Kijana na changamoto za kimisionari” katika mwanga wa Wosia wa Kitume: ‘Christus vivit’ yaani Kristo anaishi na katika muktadha wa maandalizi ya Mkutano wa kichungaji. Mkurugenzi wa Kitaifa uwasilishaji wake katika  Mkutano huo kwa kuwashirikisha hata ujumbe kutoka Shirika la kimisionari la Jimbo Katoliki la Tete, Venezuela na Msumbiji!

16 July 2020, 12:03