Tafuta

2020.06.02 Kanisa Kuu la Mtakatifu  Sofia nchini Uturuki 2020.06.02 Kanisa Kuu la Mtakatifu Sofia nchini Uturuki 

Uturuki:Kanisa Kuu la Mtakatifu Sofia kuwa Msikiti

Rais Erdogan wa Uturiki ametoa amri baada ya hukumu ya Baraza la Nchi hiyo kufuta mabadiliko ya makumbusho ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Sofia tangu 1934 na kulifanya Msikiti.Rais mwenyewe ametangaza kuwa sala ya kwanza kwa Waislamu itafanyika tarehe 24 Julai.Kanisa la Kiorthodox ulimwenguni linaonesha maskitiko makubwa kwa uamuzi huo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican


Tulitarajia kuwa mamlaka ya Uturuki ingeweza kufikiria kwa upya maamuzi yao lakini kwa masikitiko makubwa wameamua kufanya hivyo. Ndiyo uchungu mkubwa kwa Waorthodox duniani, unavyojieleza kutokana na kwamba wakristo wa Kiorthodox ulimwenguni wamekuwa wakiheshimu Kanisa Kuu la Mtakatifu Sofia lenye umuhimu mkubwa kwao, kama ilivyo kwa wakatoliki katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Roma. Kanisa hilo lilijengwa kunako karne ya VI na kuwekwa kama msimamizi wa Kristo Mwokozi na kwa maana hiyo  waorthodox wanasema "kwetu sisi litabakia daima kama Kanisa la Mwokozi." 

Maamuzi kuleta dosari ya mahusiano

Patriaki Hilarion, Rais wa Kitengo cha Mahusiano ya nchi za Nje ya Upatriaki wa Moscow amefafanua hayo wakati akihojiwa na (“Russia 24”) kuhusu uamuzi uliochukuliwa na mamlaka ya nchi ya Uturuki katika kutaifisha Kanisa Kuu la Mtakatifu Sofia jijini Istanbul ambalo lilikuwa ni jumba la Makumbusho na sasa linabadilishwa kuwa Msikiti. Kwa mujibu wa Patriaki wa Makanisa yote mawali ya Kiorthodox nchini Urusi wanasema kwamba uamuzi uliochukuliwa kwa hakika utaathiri uhusiano wa nchi hiyo na ulimwengu wa Ukristo, kwa sababu zaidi ya mara moja, hata katika siku chache zilizopita, "tumesikia sauti ya viongozi wa Kikristo ambao wamealika viongozi wa Uturuki wache kuchukua uamuzi huo".

Kanisa la Mtakatifu Sofia ni lenye thamani

Hata hivyo kuhusu suala hili hata Patriaki wa Moscow Kirill alikuwa amesema katika taarifa iliyochapishwa tarehe 6 Julai 2020 na alielezea wasiwasi wake juu ya hatima ya mojawapo ya kazi yenye thamani zaidi ya utamaduni ya Kikristo. Kwa maana hiyo viongozi wote hao wa Mosco Patriaki Kirill na Patriaki Hilarion wamesisitiza kuhusu uhusiano wa karibu sana kati ya historia ya Ukristo huko Urusi na Mtakatifu Sophia. "Picha ya Kanisa hili imekuwa mzizi mkuu katika tamaduni na historia yetu” anaandika Kirill. Na ikumbuke kuwa Istanbul ni makao makuu ya Patriaaki wa Konstantinople.

Jaribio la kudhalilisha urithi wa kiroho wa milenia

Katika taarifa yake Patriaki wa Urusi anakumbuka kwamba japokuwa hivi karibuni kumekuwa na vipindi wakati mwingine vigumu katika historia ya uhusiano kati ya Urusi na Constantinople, lakini pamoja na  uchungu na hasira, watu wa Urusi wamejibu  huko wakisahau mambo ya zamani hasa katika jaribio lolote la kudhalilisha au kukanyaga urithi wa kiroho wa milenia ya Kanisa la Konstantinople.

Onyo la Patriaki Bartholomew

Patriaki wa Konstantinople Bartholomew, katika siku za hivi karibuni, alikuwa amekemea hatari ya uamuzi na kusema tukio hili litashinikiza mamilioni ya Wakristo ulimwenguni kote dhidi kuwa na migongano ya dini mbili. "Kwa kufahamu utakatifu wake, Mtakatifu Sophia, ni kituo cha maisha ambamo Mashariki na Magharibi hukumbatia, na ubadilishwaji wake kuwa mahali pa  ibada ya Kiislam utasababisha kuvunjika  uhusiano katika dunia  hizi mbili".  Aidha Patriaki alisema "Karne ya 21 ni upuuzi na hatari kwamba katika Mtakatifu Sophia,mahali ambapo imekuwa ik ikiruhusu watu hao wawili kukutana nasi na kuvutiwa na ukuu wake, inawezakanaje  tena kuwa sababu ya kupingana na kugongana?
 

11 July 2020, 15:12