Tafuta

Vatican News
Maisha ya kikanisa ni shule bora ya unyenyekevu na huruma kwani  na matendo hayo yanatukumbusha mara kwa mara kuwa Yesu aliishi utimilifu katika mantiki hizi mbili. Maisha ya kikanisa ni shule bora ya unyenyekevu na huruma kwani na matendo hayo yanatukumbusha mara kwa mara kuwa Yesu aliishi utimilifu katika mantiki hizi mbili.  (Vatican Media)

Ureno:Mpango mpya wa kichungaji,Lisbon:kutoka nje na Kristo ili kukutana aliyepembezoni!

Patriaki huko Lisbon nchini Ureno amewakilisha mapango mpya wa kichungaji 2020-2021,unaoongozwa na kauli mbiu“kutoka nje na Kristo kwenda kukutana na aliyepembezoni.Ili kuweza kuinjilisha na kukua kama Kanisa inahitajika kujua nguvu ya wokovu wa maisha ya maskini na kuwaweka katika kitovu cha safari yetu ya maisha.

Na Sr. Angela Rezaula – Vtican

Kutoka nje na Kristo ili kukutana na wote walioko pembezoni ndiyo kauli mbiu mpya ya kichungaji itakayoongoza mwaka 2020/2021 iliyowakilishwa na Upatriaki wa Lisbon nchini Ureno. Katika kuwasilisha Mpango wa kichungangaji  Patriaki, huyo  Kardinali Manuel Clement, anaandika kuwa “Ili kuinjilisha ulimwenguni na kukua kama Kanisa inahitajika kujua nguvu ya wokovu wa maisha ya maskini na kuwaweka katika kitovu cha safari yetu ya maisha.”

Kuendeleza shughuli za mshikamano

Kwa mujibu wa Patriaki  Clement pia ni mwaliko wa kufanya Kanisa liwe kama ‘mtandano wa mahusiano kidugu’, hasa katika kipindi hiki cha janga virusi vya corona au covi-19 lililosababaishwa matatizo makubwa ya kijamii na kiuchumi. Katika mtazamo huo Kardinali Clement anawashauri waamini wote wapeleke mbele shughuli nyingi za ubunifu, upendo na mshikamano zilizo anzishwa katika mwezi Machi wakati watu wote wako karantini ya Covid-19.

Kwa kuwajibika inawezekana kufikia lengo

Kardinali Clement wakati huo huo, anawatia moyo wa uwajibikaji kikanisa kwa pamoja kwa anasema  ni kwa njia hiyo  tu wanaweza kufikia malengo ya kutimiza wema wa kiroho na kimwilli, iwe binafsi, lakini pia hata kwa wengine. Maisha ya kikanisa ni shule bora ya unyenyekevu na huruma kwani yanatukumbusha mara kwa mara kuwa Yesu aliishi utimilifu katika mantiki hizi mbili.

Kanisa ni chachu la upendo na linakuwa kwa mshikamano

Kanisa la upendo ni chachu kubwa ya kukua kama Kanisa katika mshikamano na uwajibikaji na kuweza kujumushwa hata Katekesi. Katekesi kwa hakika haijakamilifua bila kuwa na matendo ya upendo kwa ndugu wahitaji zaidi. “ Kwa hakika mwaka kesho utakuwa mwaka wenye nia njema hata mazoezi mema, kwa maana hiyo tusali kwa ajili ya kuufanya uwe hivyo hivyo”, anahitimisha barua yake Kardinali wa Lisbon.

03 July 2020, 10:27