Tafuta

Vatican News
2020.05.09 Yesu alisema mimi ni njia, kweli na maisha ( Yh 14,6) 2020.05.09 Yesu alisema mimi ni njia, kweli na maisha ( Yh 14,6) 

Brazil:Maisha yana thamani gani?ndiyo Kampeni ya maaskofu dhidi ya biashara ya binadamu na utumwa!

Maisha yana thamani gani ni Kampeni ya Baraza la Maaskofu nchini Brazil,ambayo inakusudia kuangazia umakini kwa wakuu wa umma kuhusu uhamasishaji na ujumuishwaji wa kijamii kwa waathirika wa biashara ya binadamu na utumwa kwa ajili ya uhakika wa haki zao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Maisha yana thamani gani? ndiyo swali msingi linaloulizwa na Baraza la Maaskofu katoliki nchini Brazil(Cnbb) kama kauli mbiu ya kuongoza kampeni dhidi ya kupinga biashara mbaya ya binadamu. Shughuli hii imeanzishwa na Tume ya kichungaji kwa ajili ya kupambana dhidi ya biashara mbaya ya binadamu na utumwa (Cepeeth), ambayo imezinduliwa  tangu Jumapili tarehe 26 Julai  na itakayomalizika siku ya Alhamisi, tarehe 30 Julai 20, tarehe ambayo inaadhimishwa “Siku ya Kupambana na Biashara ya Binadamu Kimataifa.

Kwa mujibu wa Tovuti ya Maaskofu nchini Brazil, “Kampeni inakusudia kuangazia umakini kwa wakuu wa umma juu ya uhamasishaji na ujumuishwaji wa kijamii kwa waathirika na juu ya uhakika wa haki zao. Kwa sababu hii hata wakati wa siku hizi itazinduliwa video mbili, matangazo ya redio na vifaa vya  habari kuhusu  mada ya biashara mbaya ya wanawake, watoto na wahamiaji. Tarehe 29 Julai, wanafanya mkutano kwa njia ya mtandao kwa wajumbe wa Baraza la maaskofu mahalia katika  Kituo cha Wascalabrini cha Mafunzo ya Uhamiaji. Mkutano unatangazwa moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii ya Caritas nchini Brazil.

Watangazaji wa kampeni pia wanamasishwa kufanya ishara halisi, kama vile kuwasha mshumaa na, katika maombi, kukaa kwa kwa kimya kwa dakika chache  kwa ajili ya waathiriwa wa biashara hii mbaya  ya binadamu. Tume ya Baraza la Maaskofu Brazili wanasisitiza kwamba mbele ya uhalifu wa wanaomba kuwepo na matendo thabiti kwa upande wa Taasisi ya umma ili wapambane dhidi ya uhalifu huo na kuwaadhibu wanaohusika. Maaskofu wa Brazil wanasisitiza kuwa biashara mbaya isiyo ya kibinadamu ambayo hubadili watu kuwa kama bidhaa na kuondoa hadhi zao mbili muhimu, bila kujali ikiwa imeingiliwa sana na lengo la ngono, kazi, za suluba, biashara ya  viungo au kwa kupitishwa na kuuza haramu watoto.

Baraza la Maaskofu, nchi Brazil Cnbb hatimaye wanatoa miito mingi iliyotolewa na Papa Francisko dhidi ya usafirishaji na biashara ya binadamu,wakati wa sala ya Malaika wa Bwana kunako tarehe 9 Februari, siku ambayo ilikuwa ni siku kuu kiliturujia ya Mtakatifu Giusephine Bakhita, sambamba na siku kuu ya kimataifa ya maombi na tafakari kuhusu biashara ya watu,  alisema ni  pigo la kweli na  lilokuwamba wanyonge zaidi, ambapo lazima kuwepo jitihada za wote katika kunusuru watu hao. Taasisi, vyama na mashirika ya elimu kama inavyobaisha tafiti kadhaa kuwa, mashirika ya jinai yanazidi kutumia njia za kisasa za mawasiliano  kuwaadaa hawa waathiriwa.  Suala hili linahitajika kwa upande mmoja kuelimisha juu ya utumiaji mzuri wa njia za kiteknolojia, kwa upande mwingine, kusimamia kidete na kupambana dhidi ya wahalifu hawa.

Kila tarehe 30 Julai ni siku ya Kupambana na Biashara ya Binadamu Kimataifa. Ikumbuke kuwa kila tarehe tarehe 30 Julai inaadhimisha Siku ya Kupambana na Biashara ya Binadamu ulimwenguni.  Ni siku maalum iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa ili kusaidia juhudi za kimataifa kuwajibika katika kuhakikisha mapambano na athari hizo katika maisha ya binadamu. Jambo ambalo linamwondolea hadhi binadamu. Kila mwaka kuna mamilioni ya watu wanaotumbukia katika mifumo ya utumwa mamboleo, hususan katika kazi za suluba, utalii wa ngono na biashara haramu ya viungo vya binadamu.

Hivi karibuni, mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva, akihutubia katika baraza la Usalama la Umoja wa Ulaya  OSCE alibainisha ni kwa jinsi gani kuna mapungufu makubwa katika sheria ili kudhibiti uhalifu huu, adhabu ndogo inayotolewa pamoja na baadhi ya watu kutofahamu madhara ya biashara. Kwa maana hiyo hii ni changamoto kubwa sana ambazo pia zimebainishwa na wanaharakati wengi sana dhidi ya biashara ya binadamu na utumwa wa kisasa. Waathirika ulimwenguni ni wengi sana ambapo jitihada  za kuondoa aina zote za utumwa mamboleo, bado zinahitajika na zaidi katika maeneo mengi yenye kinzani na ghasia na nchi maskini ambazo zimezabisha hata wimbi la ukimbizi duniani kote.

28 July 2020, 12:04