Tafuta

Vatican News
Uinjilishaji Uinjilishaji 

Australia:Teknolojia yawasaidia wakatoliki watu asilia dhidi ya changamoto!

Kufuatia na janga ugonjwa wa mapafu unatokana na virusi vya Corona kumechochea ubunifu wa namna mpya ya kuadhimisha misa za Dominika ya watu wa asilia wa kisiwa cha Torres huko AAustalia kupitia mitandao ya kidijitali.Maadhimisho ya Misa Takatifu iliyoadhimishwa katika Kanisa Kuu la Francisko wa Xaveri huko Adelaide

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baraza kuu la Kitaifa la Watu wa asilia na Wahariri wa kisiwa cha Torres Strait (NATSICC) linaloongozwa na Maaskofu Katoliki Nchini Australia, wamejivunia teknolojia mpya iliyosaidia kuadhimisha Sherehe za Dominika kwa Watu wasilia  Domika tarehe 5 Julai 2020.  Sherehe hizo zilihudhuriwa na idadi kubwa ya wakatoliki 130,000 waliokusanyika kusali, kuadhimisha sakramenti pamoja na kutoa ukarimu wao kwa wagonjwa na wafungwa.    Maadhimisho hayo ambayo mwaka huu yamekumbwa na janga la virusi vya Corona kwa maana hiyo yameadhimishwa na namna ya pekee sana huku Kanisa likiona fursa mpya zilizojifunua kwa utumiaji wa teknolojia katika uinjilishaji.

Kufuatia na janga ugonjwa wa mapafu unatokana na virusi vya Corona kumechochea ubunifu wa namna mpya ya kuadhimisha Dominika ya watu wa asilia  wa kisiwa cha Torres kupitia mitandao ya  kidijitali. Maadhimisho ya Misa Takatifu iliyoadhimishwa  katika Kanisa Kuu la Francisko Xaveri  wa Adelaide yamerushwa moja kwa moja na vyombo vya habari yakiwa na lengo la kuhamasisha na kuzingatia maelekezo ya watalaam ya kutunza umbali kati ya mtu na mtu lakini katika hali ya udugu na upendo.

Haya yamesemwa na Rais wa Kamati ya ushauri ya Wakatoliki kwa ajili ya watu wa asili katika kisiwa cha Torres Bwana John Lochowiak katika maadhimisho ya hayo ya siku ya wakazi wa Torres, huku akionesha namna wakatoliki walivyokuwa na shauku kubwa na ya muda mrefu  ya kumshukuru Mwenyezi Mungu. Kipindi hiki cha janga la Corona kimeamsha ari mpya mioyoni mwa wakatoliki ya kufikiria upya ule mtindo wa maisha ya kikristo. Wakiongozwa na Neno la Mungu katika maandiko Matakatifu, wamefarijika kuona Mwenyezi Mungu bado anawapigania.

Janga la Corona kwa wananchi wa Australia, limewafika baada ya kipindi kirefu cha ukame na uchomaji moto wa misitu.  Pamoja na changamoto mpya zilizowakumba kwa kipindi hiki lakini, wameona ni muhimu kuendelea kuweka tumaini kwa Mungu na kutafuta zaidi tunu  za kiroho za huruma, urafiki na upendo. Aidha, Bwana Lochowiak ameendelea kufafanua kuwa kuwepo na huduma ya kidijitali ambayo imewezesha waamini wengi  Wasilia kushiriki Misa Takatifu ya Dominika ni hamasa kubwa katika utumiaji wa teknolojia mpya. Vyombo hivi vya habari vimewawezesha watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi kukutana katika tovuti na kusherehekea licha ya kuwa na umbali wa kijiografia

08 July 2020, 16:32