Tafuta

Vatican News
2020.05.15 Askofu Natale Paganelli, Msimamizi wa kitume wa  Makeni inchini  Sierra Leone   2020.05.15 Askofu Natale Paganelli, Msimamizi wa kitume wa Makeni inchini Sierra Leone  

Sierra Leone:Ask Paganelli atoa wito wa utulivu dhidi ya mafachuko mji wa Makeni!

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Kitume Askofu Paganelli ameonesha wasi wasi mkubwa kufuatia na ghasia zilizojitokeza nchini Sierra Leone na kusababisha vifo vya baadhi ya vijana.Kwa mujibu wake anasema Kanisa litaendelea kusali ili roho za marehemu zipumzike kwa amani na kwa majeruhi walioko katika hospitali ya Makeni wapone kwa haraka.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Msimamizi wa kitume wa jimbo la Makeni nchini Sierra Leone, Askofu Natale Paganelli katika taarifa yake ametoa wito ili kutulia baada ya ghasia na machafuko ya hivi karibuni katika mji wa Makeni na kuwaalika wote wajikite katika mapambano dhidi ya Covid-19. Machafuko yalizuka usiku wa tarehe 17 Julai 2020. Vijana wa jiji hilo walijaribu kuzuia uhamishaji wa jenereta ya joto ya Megawati 1.65 kwenda katika mji wa Lungi, mahali  ambapo kuna uwanja wa ndege wa kimataifa. Kikosi cha ulinzi na usalama walifyatua risasi na kuwaua karibu watu watano na kuwajeruhi wengine wengi.

Kanisa kuendelea kuwaombea waathirika 

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Kitume Askofu Paganelli tarehe 26 Julai ameonesha wasi wasi mkubwa na suala la kupoteza vijana. Amesema Kanisa litaendelea kusali ili roho za marehemu zipumzike kwa amani na kwa majeruhi walioko katika hospitali ya Makeni mjini Freetown, wapone kwa haraka. “Kama jimbo, tunaonesha masikitiko yetu ya kina, mshikamano na salam za rambi rambi kwa wazazi wao, familia zao na marafiki wanaoomboleza. Mungu mwenyezi awape nguvu na faraja kutokana na mahangaiko yao katika wakati huu mgumu”, Anaandika Askofu. Aidha akipongeza ishara ya rais wa jamhuri kwa kutuma uwakilishi wake wa nguvu katika mji huo ili kutathimini machafuko, Askofu amesema kuwa jimbo linatoa wito kwa watu wa Makeni kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi. Uchunguzi wa haraka, ulio wazi ili kukabiliana na sababu za ghasia na kwa ajili ya waliowekwa mbaloni kuachiwa kwa haraka. Askofu Paganelli anasema kuwa, kuwaachia walioshikiliwa na vyombo vya umma inaweza kupungunguza mivutano, hasira na uchungu kati ya watoto wa mji wa Makeni, iwe nchini humo hata nchi za nje.

Siyo wakati wa kupteza mtazamo wa kupambana na covid-19

Siyo wakati wa kupoteza umakini juu ya mapambano ya pamoja dhidi ya adui Covid-19 na athari zake kijamii na kiuchumi juu yetu sisi amesema. Kama Kanisa tunalaani kila aina ya kutumia nguvu na ambayo tunaifikiria kama uharibifu mkubwa na usio na tija.  Aidha amesema kuwa Mafundisho ya Kanisa yanathibitisha kuwa kila maisha ya binadamu ni matakatifu na yenye thamani isiyo na kifani ya Mungu Muumba. Amewaalika watu wote kuheshimu, kulinda, kupenda na kuhudumia maisha, kila maisha ya mwanadamu, kama sura ya 5 ya Wosia wa Evangelium Vitae, Hati ya Kanisa juu ya thamani na maisha yasiyokiukwa ya mwanadamu. Katika tamko lake amewaalika wote kufuata mfano wa mchako wa njia ya mazungumzo mema na ya kujenga, kuheshimiana, na mapatano yenye matunda. Askofu Paganelli aidha ametumia maneno ya Papa Mstaafu Benedikto XVI katika hati ya baada ya Sinodi ya Afrika 'Africae Munus’, kuwa “maridhiano yanashinda migogoro, yanarudisha hadhi ya wat una kufungua njia ya maendeleo na amani ya kudumu kati ya watu kwa kila ngazi” . Askofu wa Makeni ametoa ushuri kwa wito kutafuta amani, msimamo na maelewano katika Nchi na kuzuia sera za kisiasa zenye migawanyiko.

Lazima kusali kwa ajili ya amani ya nchi

Amewawaalika wanaparokia wote, watu wenye mapenzi mema waendelee kusali ka ajili hiyo  na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya nchi “ili mawingu meusi ya migawanyiko, chuki, ukosefu wa imani na sera mbaya za kisiasa ambazo kwa sasa zinazunguka ndani ya vichwa, ziweze kuisha haraka na nyota angavu ya mapenzi mema, ya maelewano, ya umoja na mapatano viangaze sana katika ardhi hii tunayoipenda ya Sierra Leone.” Hili ni tamko la pili la Askofu Paganelli karibia kwa miezi miwili hivi. Tamko la kwanza lilitolewa tarehe 13 Mei 2020, baada ya machafuko katika mji na mauaji ya wafungwa wengi katika gereza la Pademba jijini  Freetown. Yeye alikuwa amewashauri watu wote wa Sierra Leone kutulia na kutunza amani kwa kuzuia migawanyiko ya makabila na kukumbatia mazungumzo. Alikuwa ameomba kufafanya uchunguzi kuhusiana na ghasia hizo na kuheshimu maisha ya mwanadamu.

31 July 2020, 10:26