Tafuta

Vatican News
2020.07.15 Siku kuu ya kutabarukwa kwa Kanis Kuu la Kaburi Takatifu Yerusalem 2020.07.15 Siku kuu ya kutabarukwa kwa Kanis Kuu la Kaburi Takatifu Yerusalem  (Nadim Asfour /CTS)

Nchi Takatifu:Kaburi Takatifu ni ishara ya uzuri ulioharibiwa na kubadilishwa kwa njia ya Kristo na Kanisa!

Uzuri ulioharibiwa na uzuri uliobadilishwa ni mfano unaofupisha ujumbe wa mahali hapa na katika siku kuu hii.Mantiki hizi zinatazama Yesu wa Nazareth aliyesulibiwa na kufufuka,yanatazama Kanisa na kila mmoja wetu.Ni maneno ya mahubiri ya Padre Patton msimamizi wa maeneo matakatifu Yerusalem,tarehe 15 Julai 2020 wakati wa misa ya kumbu kumbu ya kutabarukwa kwa Kanisa kuu la Kaburi Takatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Msimamizi wa maeneo Matakatifu, Padre Francesco Patton, ambaye tarehe 15 Julai 2020 huko Yesuralemm ameongoza maadhimisho ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumbu kumbu ya kutabarukwa kwa Kanisa Kuu la Kaburi Takatifu iliyowekwa wakfu kunako tarehe 15 Julai 1149, amesema “Uzuri ulioharibiwa na uzuri uliobadilika ni mfano unaowezekana kutoa ufupisho  wa ujumbe katika mahali hapa na katika sikukuu hii. Mantiki hizi zinatazama Yesu wa Nazareth aliyesulibiwa na kufufuka, yanatazama Kanisa na kutazama kila mmoja wetu.”

Uzuri umeharibiwa na dhambi za watoto wa Mungu

Kwa mujibu taa taarifa kutoka katika Tovuti ya Upatriaki wa Yerusalem,  mahubiri yake katika Siku Kuu  hiyo  Padre Pattone amesema “ katika eneo hili, na sikukuu ya leo inatukumbusha kuwa kuna uzuri ulioharibiwa na kubadilishwa hata katika Kanisa”. Ni kama vile kwenye  eneo hii linabeba mwili na siyo kumbu kumbu tu ya mateso na ufufuko wa Bwana, lakini pia hata mateso na ufufuko wa Kanisa”. Padre Patton aidha amesisitiza kuwa “uzuri wa Kanisa umeharibiwa hasa na dhambi ya watoto wake, kashfa ambazo mara nyingi zinaibuka na wakati mwingine kwenda kinyume na mahubiri na matendo ambayo bado yanaonesha kashfa nyingi na zaidi  tabia na mienendo yetu  ambayo ni  kinyume na matakwa ya  Injili. Kashfa hizi na nyingine pia zinajioneshwa kila wakati katika vyombo vya habari kwa bahati mbaya na kuongezea zaidi kashifa hizi katika uzuri wa Kanisa, amesisitiza Padre Patton.

Uzuri unaoneshwa na ushuhuda wa wanandoa,watawa na wachungaji waaminifu

Kwa kufafanua zaidi Padre Patton ameongeza wakati huo huo uzuri uliobadiliwa na Kanisa ni ushuhuda ambao unaangazwa na kuoneshwa na wanandoa, wanaopendana kwa namna ya uamanifu na yenye kuzaa matunda; kwa watawa, ambao wanajikita kupanda mbegu yaudugu katika ulimwengu wa leo ambao umejaribiwa na kiburi, ubinafsi na maslahi; kwa wachungaji hasa wale ambao kwa dhadi wanatambua kubaki karibu na zizi la Kristo kwa uaminifu hata katika hatari ya maisha, kwa sababu hawataki kuacha na kwenda mbali na zizi ambalo walikabidhiwa.

Mungu anatupenda hadi kutoa mwanae wa pekee

Hatimaye, Padre Patton amesema, uzuri ulioharibiana kubadilishwa karibu ni kwa kila mmoja wetu na kwamba ikiwa dhambi inaharibu kazi ya Mungu ndani mwetu, upendo usio na mwisho ambao Mungu anatupenda, hadi kutoa mwanae kwetu sisi ambaye kwa mara nyingine tena  anatupati fursa ya kurudisha uzuri uliobadilishwa wa mtu aliyekombolewa na ambaye anashiriki Pasaka ya Yesu.

Kanisa Kuu la Kaburi Takatifu lilijengwa 355

Kwa utashi wa Mfalme Costantino na mama yake Elena lilijengwa Kanisa Kuu la Kaburi Takatifu kunako mwaka 355. Kaburi Takatifu, au Kanisa Kuu la “Anastasis”, yaani Pasaka  ni mwingiliano wa majengo aambayo yamepata mabadiliko kadhaa kwa karne nyingi. Leo, hii ni mahali muhimu sana hasa  kwa Wakristo ulimwenguni kote na pia ni muundo wa mabaki ya ujenzi wa Konstantino na kazi ya wapita njia ambayo inaunganisha Kalvari na Kaburi la Yesu, kana kwamba ni kuashiria kisichoonekana cha kifo na  ufufuko wa Mkombozi.

18 July 2020, 13:27