Tafuta

Vatican News
2019.03.19 mitandao ya kijamii,mawasiliano ya watu,interneti,mitandao ya kidigitali na simu za mikono 2019.03.19 mitandao ya kijamii,mawasiliano ya watu,interneti,mitandao ya kidigitali na simu za mikono 

Marekani:mkutano kwa ajili ya uinjilishaji katika kipindi cha kiteknolojia!

Mkutano wa Tatu wa Mawasiliano katoliki wa ushirikiano wa Jimbo Kuu la Los Angeles,nchini Marekani kwa siku ya tarehe 4 na 5 Agosti, unakusudia kujikita katika kutazama uinjilishaji wa kipindi cha kiteknolojia au kuweka kuona matunda ya uzoefu na ufundi wa kidigitali ili kuboresha jitihada na kuhusisha parokia na shule katoliki.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Uinjilishaji wa kipindi cha kiteknolojia au kuona matunda ya uzoefu na ufundi wa kidigitali ili kuboresha jitihada na kuhusisha parokia na shule katoliki, ndiyo lengo la mkutano wa Tatu wa Mawasiliano katoliki wa ushirikiano ulioandalia kufanyika  na Jimbo Kuu la Los Angeles, nchini Marekani kwa siku ya tarehe 4 na 5 Agosti 2020.

Kufuatia na dharura ya kiafya ya Covid-19, tukio hili litafanyika kwa njia ya  mtandao kwenye Tovuti ya jimbo la (c3.la-archdiocese.org.). Katika taarifa yao wanasema janga la sasa limeonesha wazi kwamba tunapaswa kuwa tayari kukabiliana na hali halisi na changamoto bila kusita. Mkutano huo ni muafaka ili kujifunza, kufanya uzoefu na kukuza uwezo wa kitaaluma wa kila mmoja. Siku ya kwanza ya kazi itajikita kusikiliza, kushirikisha, kujifunza na kujumuisha maparokia mengine, walimu wa shule na watu wa kujitolea.

Tarehe 5 Agosti 2020 mkutano wao utaangazia kusikiliza, kujifunza, kutafakari na kuonyesha hatua nzuri za kuwezesha ufundishaji, ujifunzaji na huduma katika nyakati hizi zenye mashaka na usumbufu mkubwa kufuatia na janga la corona. Vikao hivyo vitawakilishwa, makatekista, wakurugenzi wa kiliturujia, walimu, wasimamizi na wafanyakazi kutoka sehemu mbali mbali za Jimbo kuu.

Baraza hili lizinduliwa mnamo 2009, ambalo linataka kukuza juhudi za kiteknolojia katika tasnia ya elimu na mafunzo na  kwa lengo la kutoa mawasiliano thabiti bila waya kwa Jimbo Kuu zima la Los Angeles. Hali kadhalika ni katika kudumisha , kuhamasisha kozi  za mitandaoni, kukuza mifano endelevu ya kifedha na kuhimiza ufadhili kwa mtandao katika  uhusiano wa shule.

29 July 2020, 13:17