Tafuta

Vatican News
Maaskofu nchini Marekani wanapinga adhabu ya kifo kwa sababu haikubaliki na ni kinyume na Injili na maisha ya mwanadamu. Maaskofu nchini Marekani wanapinga adhabu ya kifo kwa sababu haikubaliki na ni kinyume na Injili na maisha ya mwanadamu. 

Marekani:adhabu ya kifo ni kinyume na Injili na maisha ya mwanadamu!

Tume ya Haki za Ndani na Maendeleo ya Binadamu ya Baraza la Maaskofu Marekani,inapinga adhabu ya kifo kwa sababu haikubaliki na ni kinyume na matakwa ya Injili na maisha ya mwanadamu kama zawadi kutoka kwa Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Adhabu ya kifo haikubaliki, ni kinyume cha Injili na heshima kwa maisha ya mwanadamu. Wanaandika katika taarifa na  Askofu Mkuu Paul Coakley, wa jimbo kuu la  Jiji la Oklahoma na Rais wa Tume ya  Haki za Ndani na Maendeleo ya Binadamu ya Baraza la Maaskofu Marekani (Usccb). Kauli yake imefika mara baada ya Mahakama Kuu ya Marekani katika   utawala wa Trump kuangazia njia huru ya kurudisha adhabu ya kifo kwa ngazi ya kishirikisho.

Mahakimu kutosikiliza rufaa

Utekelezaji huo unaweza kuanza tena kunako tarehe 13 Julai mara baada ya miaka 17 ya kusimamishwa kwake, kwa kurudi nyuma katika utawala wa Bush. Mahakimu wa katiba, kwa dhati wameamua kutosikiliza rufaa iliyowekwa na wafungwa wanne katika mikono ya kifo. “Ni lazima tukaze mapambano anaadika  Askofu Mkuu Coakley, kwa sababu Maaskofu wamekuwa wakiomba kwa miongo kadhaa juu ya mwisho wa hukumu ya kifo.

Kifungu cha KKK n. 2267

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Coakley anakumbuka hata miito mingi iliyotolewa dhidi ya hukumu ya kifo iliyotamkwa na Mapapa miongoni mwake akiwa Mtakatifu Yohane Paulu II, Papa Mstaafu Benedikto XVI na Papa Francisko na ambaye miaka miwili iliyopita yaani 2018, aliidhinisha Hati maalum ya kurekebisha kifungu cha  n. 2267 cha  Katekisimu ya Kanisa  Katoliki, na  ili kufafanua juu ya adhabu ya kifo ambayo haikubaliki.

Kuwa na huruma kwa ajili ya hadhi ya maisha ya binadamu

Rais wa Kamati ya Haki za Ndani anakumbuka wito wa zamani uliotolewa na Baraza la Maaskofu wake (Usccb) kunako 2019, ambapo ulisisitiza kwamba kupinga hukumu ya kifo haimaanishi kuunga mkono  uhalifu, lakini pia  kuwa na huruma kwa ajili ya hadhi ya maisha ya binadamu. Kwa maana hiyo  Askofu Mkuu Coakley anahitimisha barua yake kwa kutoa wito kwa Wakili Mkuu, William Barr na kwa Rais wa Merekani, Bwana Donald Trump, ili  warudi nyuma kufikiria hatua zao na kusitisha kabisa utekelezaji wa adhabu ya kifo. Itakumbukwa kuwa kunako tarehe 23 Machi, huko Colorado imekuwa serikali ya 22 ya Marekani  katika kuondoa adhabu ya hukumu ya kifo, kwa idhini hiyo na Gavana Jared Polis, kwa muswada wa SB20-100. Katika fursa hiyo, maaskofu wa eneo hilo walitoa pongezi kwamba idhinisho hili lilikuwa ni tendo la kihistoria katika  ulimwengu wa sheria.

01 July 2020, 17:24