Tafuta

Vatican News
Mafuriko yameathiri zaidi ya milioni mbili ya watu huko Assam nchini India. Mafuriko yameathiri zaidi ya milioni mbili ya watu huko Assam nchini India.  (ANSA)

India:Mafuriko makubwa yasababisha madhara makubwa huko Assam

Kwa mujibu wa Askofu Thomas Pullopillil wa jimbo la Bongaigao akieleza katika chombo cha habari cha UCA amesema mvua kali zilizonyesha na mafuriko kama hayo ni matukio ya kila mwaka,japokuwa mwaka huu yamekuwa makubwa mno,pia ni kwa jinsi gani mashirika ya serikali na Kikanisa yanashughulika kidogo kinachowezakana ili kukabiliana na hali ngumu sana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua za msimu yamesomba sehemu kubwa ya majimbo ya Mashariki ya India ambako kuna idadi kubwa ya watu. Maafisa wameeleza kwamba zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kukaa kwenye makazi ya muda yaliyojengwa licha ya kitisho cha virusi vya corona.  Kwa mujibu wa Askofu Thomas Pullopillil wa jimbo la Bongaigao akieleza katika chombo cha habari cha UCA amesema mvua kali zilizonyesha na mafuriko kama hayo ni matukio ya kila mwaka, japokuwa mwaka huu yamekuwa makubwa mno, lakini pia kueleza jinsi gani mashirika ya serikali na yale ya Kikanisa yanashughulika kidogo ambacho wanaweza ili kabiliana na hali ngumu sana hivyo.

Umakini unahitajika kusaidia watu

Kwa bahati mabaya Askofu Pullopillil, amesema sasa hawana uwezo wa kufanya zaidi kwa wale wenye matatizo kwa sababu fedha zao walizokuwa nazo zimetumika kununua vyakula kwa ajili ya wafanyakazi wahamiaji walio kwenye karantini na maskini sana wakati wamejitenga kwa sababu ya janga la Covid-19. Vile vile amelalamika kuhusiana na jimbo hilo kutopata umakini wowote kuhusu habari za kitaifa licha ya kuwa ni janga kubwa. Mwezi ujao utakuwa labda ulio mbaya zaidi ya vipindi vya mvua amesema Askofu na ikiwa hali halisi itaendelea kuwa hivi na  hawajuhi jinsi gani wataishia.

Mkutano wa jukwaa la wakristo

Naye Allen Brooks, msemaji mkuu wa jukwaa la wakristo wa Assam, shirika ambao linaleta pamoja hata Makanisa ya Kikristo katika eneo hilo, lenye makao makuu huko Guwahati, mji mkuu wa biashara ya  Serikali ameliambia shirika la habari UCA kwamba viongozi wa Kanisa na madhehebu yote, tarehe 14 Julai  wametazama kwa pamoja hali halisi ambayo watu wanakabiliana nayo wa Assam na ambao wanahitaji kupata msaada  wa haraka katika wakati huu wa mgogoro mkubwa.

Vizuizi vya corona na kuongezea mafuriko

Mvua kubwa za msimu kimsingi ni muhimu kwa ajili ya kilimo katika eneo hilo la Asia ya Kusini, lakini kwa mujibu wa maafisa wa afya nchini humo mvua za mwaka huu nchini India zimenyesha katika wakati ambapo nchi hiyo pia inakabiliana na virusi vya corona. Vizuizi vilivyokuwa vimewekwa na serikali ili kuzuia maambukizi ya janga la virusi na ukosefu wa fedha ni mambo ambayo yanaendelea kuzuia Kanisa kuweza kuwafikia majimbo ya Assam ambayo yameharibiwa sana na mvua kubwa kwani ni watu milioni  3,6 waathiriwa  sana vifo  66 waliofariki kwa mujibu wa vya habari nchini humo UCA . Waliojeruhiwa sana ni katika majimbo ya Assam, Bihar na Jharkhand ambako mvua kubwa ilisomba maelfu ya vijiji katika muda wa saa 24 zilizopita. Maafisa wanajaribu kwenda kwenye maeneo hayo kuhakikisha watu hawakaribiani kwenye makambi ya msaada ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona

17 July 2020, 14:25