KENYA:Murang'a:kliniki mpya ya Kiriaini ya Wamisionari wa Consolata!
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Jitihada ya Kanisa Katoliki nchini Kenya katika sekta ya afya inajikita zaidi na zaidi wa ajili ya walio maskini na walio katika mazingira magumu zaidi. Hospitali ya Kiriani ya Wamisionari, imeweza kuzindua kitengo kipya ndani mwake. Katika hafla ya uzinduzi huo ilifanyika tarehe 17 Julai 2020, akiwepo Katibu wa Baraza la Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe na aliyetoa baraka ni Askofu Joseph Ndembu Mbatia, mkuu wa Tume ya Maaskofu Kenya kwa ajili ya Huduma ya kichungaji ya Afya. Pia alikuwepo Askofu James Maria Wainaina, Askofu wa Murang'a, ambapo hospitali hiko iko katika eneo lake.
Hospitali ya utume ya Kiriaini kwa mujibu wa habari kutoka Cisa wanasema, daima imekuwa mstari wa mbele kutoa huduma kamili za matibabu za kukinga na kulinda wote, kwa umakini zaidi na zaidi maskini ambao hawana fursa, katika roho ya kutangaza huduma ya uponywaji wa Kristo.
Utambuzi na Shukrani kwa kazi ya Kanisa umeoneshwa na Mutahi Kagwe, ambaye alikumbuka kwamba muundo wa hospitali hiyo ni mmoja ya hutoaji huduma kuu ya afya ya wenyeji wa eneo hilo. Kunako mwaka wa 2019, kwa ujumla wagonjwa 63,772 walitibiwa katika Hospitali ya Kiriaini. Mwakilishi wa serikali pia alisisitiza juu ya mamlaka ya huduma bora za afya kuhakikisha ufanisi mkubwa, upatikanaji na ukasi katika matibabu, ambao tayari utakuwa wa siku zijazo!
Hospitali ya Wamisionari ya Kiriaini ilianzishwa na Watawa shirika la Wakonsolata kunako 1955 kama kiliniki ndogo. Kadiri ya siku zilivyoongezeka na kuongeza kwa vifaa vyake ikawa ni kituo cha kwanza cha uzazi na baadaye kuwa hospitali halisi yenye vitanda na idara 72 za Wanajinakolojia na Uzazi, Madaktari wa watoto na upasuaji.Kwa sasa hosptali hiyo inasimamiwa na jimbo la Murang'a.