Tafuta

Kardinali Berhaneyesus Souraphiel Kardinali Berhaneyesus Souraphiel 

Ethiopia:Kanisa linatoa huduma kwa ajili ya ustawi wa taifa

Kwa mujibu wa Kardinali Berhaneyesus Souraphiel,wa Jimbo Kuu Katoliki Addis Abeba na Rais wa Tume kwa ajili ya Upatanisho wa Kitaifa iliyoanzishwa na Waziri wa Mkuu Abiy Alì, anasema mshikamano,mazungumzo na uhusiano kimataifa vijahitajika nchini Ethiopia na Kanisa linajikita katika kuhudumia kwa ajili ya wema wa taifa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tunaishi hali halisi ya mivutano ambayo imesababishwa na kipindi cha mabadiliko ya kina na idadi kuwa za mageuzi yaliyofanywa na serikali ambayo kiukweli haifanyi wakubaliane wote. Kanisa lipo na linaalika kuwa ni wakati wa kufanya mazungumzo ya dhati ili kweli thamani zza pamoja ziweze kuonekana kwa njia ya kukutana  kufanya kazi pamoja kwa ajili ya wema na ustawi wa nchi. Ni maneno yaliyo wazi ya Kardinali Berhaneyesus Souraphiel, wa Jimbo Kuu Katoliki Addis Abeba na Rais wa Tume kwa ajili ya Upatanisho wa Kitaifa iliyoanzishwa na Waziri wa Mkuu Abiy Alì, mwenye Nobel kwa ajili ya amani  2018  yaliyowafikia Shirika la habari za Kimisionari Fides.

Akizungumza kuhusu hali ya sasa nchini Ethiopia nchi ambayo labda ni ishala ya hatua ya kuanza maendelea na mpito wa kidemokrasia katika bara la afrika, na wakati huo huo, imekumbwa na mivutano ya kina ambayo imeongezewa na janga na kwa maana hiyo Kardinali anaeleza nafsi muhimu hasa ya Kanisa kujikita mstari wa Mble kuwa karibu na watu. Janga  linla sasa linaleta madhara makubwa, na kama  Kanisa wamemeamua tangu mwanzo kufuata maagizo yaliyotolewa na kuzindua mipango ya haraka ya kusaidia. Waliopoteza maisha ni wengi na miongoni mwako hata Askofu Angelo Moreschi,  Msimamizi wa Kitume wa Gambella, nchini Ethiopia Mashariki. Alikuwa|Italia kwa sababu ya matatizo ya afya na kukumbana na Covid-19,  kifo chake kilitokea tarehe 25 Machi 2020.

Aidha Kardinali amesema kuwa virusi vya corona bado vinaendelea kutoa matokeo mengi mabaya moja ya haya ni kuongezeka kwa unyanyasaji na kutumia nguvu dhidi ya wanawake na watoto  majumbani mwao ambao wamerekodiwa katika kipindi cha karanti kuwa  na idadi kubwa ya waathirika. Pamoja na  matokeo hayo Kardinali amesema kikundi kimoja cha wanaharakati kiitwacho Zim allilin * maana yake sinyamzi, kimeomba msaada kwao na kwa pamoja wakazindua makakati kwa ajili ya kuangazia kila wakati matukio hayo, ili kuingilia kati, kuzuia na kulinda ambaye ameguswa. Aidha wameweka jitahada  zao za kulinda wanyanyaswaji wa kijinisi  wna anafanya kazi katika kitengo chao ambacho ni kwa ajili ya kuhamsisha kampeni na kusaidia waathirika.

27 July 2020, 12:52