Tafuta

Vatican News
Nchini Cuba inafurahia kuzindua shughuli za utume kwa njia ya mawasiliano. Kanisa hilo limezindua kituo cha  Radio  "Bwana ni tumaini". Nchini Cuba inafurahia kuzindua shughuli za utume kwa njia ya mawasiliano. Kanisa hilo limezindua kituo cha Radio "Bwana ni tumaini". 

Cuba:Radio ya kwanza katoliki kurusha matangazo yake kwa njia mtandao!

Tangu tarehe 24 Julai yameanza matangazo kwa njia ya Radio Katoliki kupitia mtandanoni nchini Cuba.Nchini humo hakuna vituo vingi vya Televisheni na Radio.Kanisa Katoliki visiwani Cuba,limekuwa na utaratibu wa kuchapisha matangazo kwa njia ya Magazeti yanayoendeshwa na Parokia kwa takribani majimbo 11.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican News.

Kanisa Katoliki nchini Cuba linafurahia kuzindua shughuli za utume kwa njia ya mawasiliano. Kanisa hilo limezindua kituo cha  Radio cha ni  Bwana ni Tumaini kinachoeneza Injili kwa njia ya Mtandao wa Interneti. Radio hiyo ya vijana (RCJ), ni ya kwanza kurusha matangazo yake kwa njia ya masafa ya Radio nchini Cuba na ambayo yameanza kurusha tarehe 24 Julai usiku.

Kwa mujibu wa Rubén Trinidad, mwanzilishi wa huduma ya Mawasiliano na Mkurugenzi wa Mtandao wa Vijana Katoliki (RCJ) na mwanashilika wa Shirika la umisionari waWapaulini, vijana katoliki  nchini  Cuba wamejipanga kideti kuendesha program za Radio. Jumuiya hiyo ya vijana imeanzishwa mapema mwezi Februari, 2019 kama Jumuiya ya kijamii katika mtandao kupitia Facebook, Twetter, Instagram, Telegram na WhatsApp na inategemezwa na Baraza la Maaskofu huko Cuba (COCC). Bidii hizi zinalenga kulea na kutoa habari za Jumuiya Katoliki nchini Cuba kwa nji ya Mtandao. Jumuiya hii inatazamia kujenga daraja la kidijitali kati ya Maisha ya Wakristo kufuatana na mafundisho ya Kanisa Katoliki na mafundisho ya kijamii.

Aidha, katika maelezo kutoa kwa mkurgenzi amsema kwa muda wa mwaka mmoja, vijana wamefanya kazi kubwa na ya ziada katika kujitolea ili kuendesha na kuendeleza mawasiliano katika kupeleka ujumbe. Hili ni tunda la Kanisa Katoliki nchini Cuba kama kituo cha kwanza cha usambazaji habari. mbali na hatua hii iliyofikiwa, kwa Kanisa Katoliki kujikita kutatua hali halisi ya Mawasiliano nchini Cuba  na ambayo inakumbwa na changamoto nyingi nyingi sana za kijamii na kiuchumi.

Nchini Cuba hakuna vituo vingi vya Televisheni na Radio.  Kanisa Katoliki visiwani Cuba, limekuwa na utaratibu wa kuchapisha matangazo kwa njia ya Magazeti yanayoendeshwa na Parokia kwa takribani majimbo 11. Makundi ya wakristo walei yanatekeleza program ambazo zinatangazwa moja kwa moja kwa njia ya mtandao.

27 July 2020, 13:04