Tafuta

Ugaidi katika ukanda wa Sahel unatishia msimamo wa nchi kama vile Burkina Faso Ugaidi katika ukanda wa Sahel unatishia msimamo wa nchi kama vile Burkina Faso 

Burkina Faso-Ocades:Ugaidi wa kijihadi unatishia msimamo kijamii

Katika ripoti ya Caritas mahalia nchini Burkina Faso inabanisha kuwa ugaidi wa kijihadi unatishia msimamo kijamii katika nchi yote na kuashiria hatari za ghasia katika kipindi cha uchaguzi mkuu 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Hatari za kigaidi nchini Burkina Faso inatishia umoja na msimamo wa kiungo cha kijamii nchini kote. Ni uthibitisho wa ripoti ya mwisho ya mwaka ya  Ocades, ya Caritas mahalia, iliyotangazwa siku za hivi karibuni. Tangu kuanguka kwa utaalawala wa Rais Muammar Gheddafi nchini Libia, kunako 2011, na zaidi baada ya kuunda kwa serikali mpya ya Kiislam nchini Iraq, makundi kadhaa ya kisilaha yamepandikiza hofu kubwa sana katika matataifa ya Ukanda wa Sahel. Miongoni mwa nchi hizo ni Burkina Faso, mahali ambamo katika miaka hii ya mwisho makundi ya kiitikadi yamesimika mizizi yake huko Kaskazini mwa nchi na kusababaisha hisia mbaya, miongoni mwa sera za kisiasa na kiuchumi kwa baadhi ya makundi ya kikabila.

Mashambulizi yamesababisha maelfu ya vifo vingi

Tangu 2015 mashambulizi ya makundi ya kiislam yamesababisha mamia elfu ya vifo na zaidi ya watu 765.000  kurundikana ndani wakitafuta usalama wao. Kati ya washambuliwaji daima wamekuwa ni viongozi na wajumbe wa madhehebu madogo madogo ya kikristo ambao wamekuwa waathirika sana tangu mwanzo wa mwaka huu  kutokana na mashambulizi karibu mara tano. Magaidi asili ya kijihadi yanaendelea kusababishwa hofu kuwa na majaribu zaidi hasa namna ya kuishi katika makabila na kidini nchini Burkina Faso, nchi ambayo kihistoria iliyokuwa ya amani.

Mjadala wa umma unaleta migawanyiko nchini humo

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Ocades, inabainisha kuwa hata majimbo katoliki ambayo bado hayamo katika mpango yao ya ushambulishi, lakini tishio lakini linaendelea kuongeza: “hali ya kushambulia na ghasia imekuwa tishio kubwa wakati mjadala wa umma unazidi kuleta migawanyiko zaidi kulingana na taarifa hiyo. Aidha kwa mujibu wa Caritas, ya Burkina Faso wanasema maasofu wakati wa mkutano wao wa mwaka mwezi juni mwaka huu, wameendeleza mada kuhusu amani za uchaguzi mkuu ujao tarehe 22 Novemba 2020 na kwamba siyo wakati wa kuendeleza mivutano. Ili kuweza kupingana matokeo haya, kuna ulazima wa kuwapo kwa mazungumzo kati ya Serikali, wadau wa jamii  na nguvu za mazungumzo ya kidini hata katika sikukuu na mikutano ya jumuiya nyingine za madhehebu ya dini.

Caritas mahalia kwa msaada wa Caritas Internationalis

Kwa upande wa chombo cha Caritas (Ocades) kinajikita katika mantiki mbali mbali ya msaada wa watu walio athirika zaidi. Kunako mwaka 2019 kwa msaada wa Caritas Internationalis na wadau wengine walitoa bilioni 10,2 CFA za kifranka, takribani Euro 154.233 miongoni mwa mambo menginge pia ni kusaidia watu walio lundikiana ndani mwa nchi, maskini na ujenzi karibia wa shule 90.

31 July 2020, 10:37