Tafuta

Vatican News
2020.07.31 lazima kukomesha utumwa na biashara haramu ya binadamu 2020.07.31 lazima kukomesha utumwa na biashara haramu ya binadamu 

AUSTRALIA:Siku ya kupinga biashara haramu ya binadamu.Ni uhalifu na mtindo wa kuondoa hadhi ya mtu!

Nyakati za utumwa bado hazijaisha yaani utumwa mamboleo na biashara ya usafirishaji wa binadamu bado ni hali halisi.Ni kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Sydney nchini Australia katika ripoti ya mwaka ya Mtandao Katoliki wa Australia dhidi ya utumwa.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika harakati za kilele cha Siku ya Kupambana na Biashara ya Binadamu Kimataifa, ifanyikayo kila tarehe Julai 30, Askofu Mkuu Anthony Fisher, wa jimbo Kuu katoliki la Sydney nchini  Australia, tarehe 29 Julai 2020 amewakilisha ripoti ya mwaka ya  Mtandao katoliki wa Australia dhidi ya Utumwa (Australian Catholic Anti-Slavery Network)ACAN. Katika ripoti hiyo anasema wakati wa utumwa haujaisha, utumwa mbamboleo na biashara hatamu ya binadamu bado ni hali halisi.

Jitihada za kufanya itambuliwe biashara haramu hii

Juhudi za kufanya hali halisi hii itambuliwe ili kuzuia  utekelezwaji wake ni mambo muhimu sana leo hii kulikoa karne zilizopita. Askofu Mkuu anatambua wazi kuwa nyakati za mwisho, kumekuwa na ongezeko la utambuzi wa jeraha kubwa hili katika hali halisi inayosababishwa ndani mwa jumuiya.

Biashara haramu ya binadamu na sala na tafakari juu yake

Inatosha kufikiria tu kwa mfano tangu mwaka 2013 umefanyika uamuzi wa Umoja wa Mataifa, kuwa tarehe 30 Julai kuadhimisha Siku ya Kupambana na Biashara ya Binadamu Kimataifa,  pili tangu tarehe 8 Februari 2015 sambamba na siku kiliturujia ya Mtakatifu Giusephine Bakhita, ni siku ya Kimataifa kwa ajili sala na tafakari dhidi ya biashara haramu ya binadamu. Hata hivyo mifano hii bado siyo dhamana ya kukomeshwa uhalifu huu ambao husababisha kashfa, hasa katika jamii ya Kikristo au ambayo inadai kuwa mfano wa maadili ya walioangaziwa na heshima ya haki na uhuru. Ikiwa usafirishaji hautakomeshwa, ameongeza kusisitiza Askofu Mkuu Fisher tunabaki kuwa washiriki wa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Biashara hii inaathiri watu milioni 40 ulimwenguni na maelfu Australia

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Sydney anashanga sana kuona kwamba Bunge la New South Wales la Kusini liliidhinisha kunako mwaka  2018, sheria mpya dhidi ya utumwa mambo leo bila, hata hivyo, kuifanya ianze kutumika. Askofu anasema “Serikali bado inaendelea kuwa ngumu, licha ya kutambuliwa rasmi kuwa biashara ya binadamu unaathiri watu wasiopungua milioni 40 ulimwenguni na maelfu nchini Australia.”

Kuendelea na lengo la kupambana dhidi ya utumwa

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Fisher anasema “ Ni aibu na ya kufedhehesha kuwa baada ya kukiri hadharani uhalifu huu na  kufanya kitu halisi ili kuweza kung’oa mizizi yake kabisa na hatua zote kupiga marufuku, kwa dhati wameacha wafanyabiashara na watumiaji kuendelea kufaidika na kazi ya watumwa.  Kwa kuongezea, katika muktadha wa janga kutoka Covid-19, Askofu Mkuu wa Sydney anawasihi wasipoteze lengo la kupambana dhidi ya utumwa.

Ongezeko la biashara ya binadamu nchini Australia

Katika  Ripoti ya ACAN, inabanisha ni kwa jinsi gani kuna  hatari inayoongezeka nchini Australia mitindo ya utumwa mambo leo, hasa kwa sababu ya dharura ya kiafya inayosababishwa na ugonjwa huo  wa virusi vya corona na matokeo mabaya ya kushuka kwa uchumi ambao umeleta wahamiaji, wakimbizi na watu walio na visa vya muda mfupi kuingia katika mzunguko wa kazi hii isiyowekwa wazi na isiyolindwa.

Mtandao katoliki dhidi ya utumwa uliundwa 2019

Matokeo msingi katika ripoti hiyo, ambayo ilikagua dola bilioni 3.18 (sawa na asilimia 98 ya matumizi) ya watoa huduma 2075, imeoneesha kuwa asilimia 54 yao wako katika hatari ya utumwa mamboleo katika mlolongo wa usambazaji wa masoko ya ndani, hasa kuhusu vifaa vya matibabu ya kiafya. Mtandao Katoliki wa kupambana na utumwa ulizinduliwa mwaka 2019 ambayo una wajumbe 32 miongoni mwake  unajumuisha majimbo, mashirika ya kitawa, vituo vya elimu, mashirika ya kiafya na vituo vya kutunza wazee, watoa huduma za kijamii na wote ni chimbuko katoliki.

30 July 2020, 14:02