Tafuta

Vatican News
Jumuiya ya Mtakatifu Egidio katika harakati za msuala ya kibinadamu ilifungua Program ya Dream huko Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Jumuiya ya Mtakatifu Egidio katika harakati za msuala ya kibinadamu ilifungua Program ya Dream huko Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

Afrika ya Kati:Jumuiya ya Mt.Egidio yafanikiwa kuondoa vizuizi ili msaada uingie!

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambayo kwa miaka mingi imejikita katika kukuza na kuhamasisha amani katika nchi ya watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati,hivi karibuni imeingilia kati kutoa vizingiti vya mapinduzi na kusaidia kuingiza vyakula na misaada iliyopatikana,shukrani kwa ufadhili kutoka Mfuko wa Msaada Kimataifa.Jumuiya hiyo katika harakati za msuala ya kibinadamu ilifungua hata Program ya Dream huko Bangui.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Mshikamano unapelekea kuwa na amani na ndilo suala muhimu ambalo limefanyika hivi  karibuni huko Bouar, katika mkoa wa magharibi mwa nchi ya  Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo utume wa masuala ya kibinadamu wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio umefanikiwa kusimamisha mapinduzi ambayo yalikuwa yafanyike katika mkoa wote kwenye mpaka na Cameroun.

Waasi kuzuia njia

Kwa miezi kadhaa  kundi la waasi wanamgambo wa zamani, waliotengwa na wasio kuwa na rasilimali za kuishi kwa sababu ya janga la Covid-19, walikuwa wamezuia njia za kuingia katika mji wa Bouar, kitovu msingi cha  barabara kuu ya biashara ya nchi hiyo. Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ambayo kwa miaka mingi imejikita katika kukuza na kuhamasisha amani katika nchi ya watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, imeingilia kati ili kusaidia kupeleka vyakula na misaada iliyopatikana, shukrani kwa ufadhili kutoka Mfuko wa Msaada Kimataifa. (Fondation Assistance International)FAI

Operesheni kufanyika kwa ushirikiano na rais wa nchi

Operesheni hiyo, iliyofanywa kwa kushirikiana na urais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambao umeleta matokeo ya kukomesha uasi, na kufungua tena njia ya kuweza kufikia jiji hilo na kurudisha imani katika kukomesha silaha, katika nchi ambayo vikundi kadhaa vya askari bado vinaendelea kuyumbisha nchi hiyo. Rais wa nchi Faustine Archange Touadéra na viongozi wa eneo hilo mahalia wametoa shukrani kwa uingiliaji huo ulioamua katika hali ambayo ilikuwa inaonesha hatari ya uharibifu. Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ambayo imeshiriki katika mpango wa kitaifa wa kukomesha silaha tangu 2017, itaendelea kutuma msaada hata katika  wilaya nyingine na vijiji nchini humo.

Program ya dream

Ikumbukwe katika mji wa Bangui, nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, mwaka jana Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ilifungua shughuli mpya ya kituo cha Afya cha “program ya Dream". Katika nchi  hiyo mara baada ya sahihi ya makubaliano ya amani na maridhiano  iliyotiwa sahini kunako tarehe 6 Februari 2019, shukrani kubwa kwakulingilia katikati kama mpatanishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, pamoja na  Umoja wa Afrika, (UA) Umoja wa Mataifa(UN) na viongozi wa mikoa.

Mambo mengi yanahitajika katika kulijenga taifa katika miundo ya afya na elimu 

Bado kuna mambo mengi ya kusaidia serikali katika nchi ili kuweza kujenga kwa upya miundo ya kiafya, elimu , mafunzo na maendeleo ya amani.Hata hivyo Program ya DREAM, tangu kuanza kwake Kumeleta  matumaini mapya kwa watu na hamu ya kuishi na kila siku mama na watoto wapya huwasili kuomba kutibiwa na kuponywa. Ni ishara kweli ya utabiri na utume wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kwa nchi hiyo maskini na kwa rasilimali chache sana kwa sababu ya kuwa na vita vya muda mrefu habari mpya zaidi kwa watu wengi wa Afrika ya Kati ni kusikia kwamba wakati tofauti endelevu unawezekana!

30 July 2020, 15:21