Tafuta

Vatican News
Maskofu wa Afrika wanasema kuwa tendo la kutokuwa na utulivu kunaweza kudhoofisha hata mwenendo wa amani katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Maskofu wa Afrika wanasema kuwa tendo la kutokuwa na utulivu kunaweza kudhoofisha hata mwenendo wa amani katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.  

Afrika ya Kati:Maaskofu watoa wito wa kufanya kazi pamoja kukabiliana na covid-19!

Katika ujumbe wa maaskofu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya mkutano wao mkuu wanahitimisha wakitoa wito wa kuhamasisha kupambana vizuri zaidi dhidi ya janga la virusi vya Corona na kuunda hali zinazofaa kwa utumiaji wa haki za raia na kisiasa na kwa ushiriki mkubwa wa watu wa Afrika ya Kati katika mchakato wa uchaguzi wa kidemokrasia mwaka 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kujenga Jamhuri mpya ya Afrika ya Kati, kwa ajili ya uhuru wake kijamii, kiuchumi, kisiasa na kidini kwa kufuata mfano wa Musa wakati wa kukatisha jangwa. Ndiyo wito wa maaskofu wa Afrika ya Kanisa ulioelekezwa kwa watu wa Mungu na waamini wote wake kwa waume wenye mapenzi mema, baada ya hitimisho la mkutano wao Mkuu wa pili wa mwakauliofanyika kuanzia tarehe 20 hadi 26 Julai 2020 jijini Bangui.

Lengo la mkutano huu ulikuwa kuhusu dharura ya kiafya ya Covid-19 nchini humo na ambayo inazidi kuongeza kwa kasi hadi kufikia kesi za maambukizi zaidi ya 4.599 na vifo karibuni 59; kuhusu uchaguzi wa kisiasa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.  Na hili ni tukio ambalo hali ya kutokuwa na imani na mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini humo, ambapo, hata kama baada ya ziara ya Papa Francisko mnamo 2015 awamu kali ya mzozo mpya wa kisiasa ambao ulisababisha mzozo wa ndani wa umwagaji damu ulioibuka mwanzoni mwa 2013 ilipungua kidogo japokuwa kwa sasa, wanabaki na mivutano ya kijumuiya kati ya Wakristo na Waislam na wanamgambo wenye silaha ambao wanaendelea kutawala maeneo makubwa.

Hali hii inawatia wasiwasi maaskofu wa Afrika ya Kati ambao tayari wakati wa kikao chao cha kwanza cha mwaka mwezi Januari mwaka huu walikuwa wameangazia jinsi ya kupata suluhisho la mzozo wa silaha na kuwa siyo la kijeshi tu. Kanisa, ambalo liko mstari wa mbele kikamilifu katika mchakato mgumu wa kusuluhisha baina ya serikali kuu wanayo hofu ya vikosi mbali mbali vya waasi na kwamba tendo la kutokuwa na utulivu kunaweza kudhoofisha hata mwenendo wa amani katika uchaguzi ujao. Kwa mujibu wa tamko la mwisho la mkutano wao linasisititiza kuwa silaha nyingi sana zinazozunguka na wanamgambo walio na silaha katika hatua, ukandamizwaji ndiyo suala la kupewa kipaumbele.

Kufuatana na hilo wanaongeza kusema kwamba kutokuwa na uhalali katika mchakato wa usajili kwenye orodha za uchaguzi huwakatisha tamaa raia katika kushiriki kupiga kura. Kulingana na maaskofu, wanabainisha mafanikio ya uchaguzi ni lazima kujumuisha  vikosi hai vya taifa. Hivyo vingeruhusu mchakato wa uchaguzi kuendelea, kujenga uaminifu kati ya wadau wakuu, kuunda ushirikiano mkubwa kati ya wote.Ujumbe wa Kanisa unathibitisha kuwasindikiza viongozi wa Afrika ya Kati katika mchakato huu, kuhimiza uwajibikaji, kukemea kila aina ya dhuluma kama njia ya kuthibitisha madai ya mtu na kukumbusha kanuni msingi za Injili na mafundisho kijamii Katoliki. Hadhi ya mwanadamu, heshima ya maisha, chaguo la upendeleo kwa watu maskini na walio katika mazingira magumu, mshikamano, uzuri wa kawaida, demokrasia na ushirikiano.

Mshikamano wanasisitiza unapaswa pia kuhamasisha mapambano dhidi ya virusi vya corona. Ikiwa kwa upande mmoja, viongozi hawa wanatoa shukrani zao kwa nchi ambazo zinasaidia Afrika ya Kati kukabiliana na dharura ya kiafya, kwa upande mwingine wanataka uwazi zaidi katika usimamizi wa fedha hizo na wanakiri kukosekana kwa muundo wa kutosha katika Afrika ya Kati kuchukua huduma ya wagonjwa wazito zaidi. Kwa kuhitimisha wanatoa wito wa kuhamasisha kupambana vizuri zaidi dhidi ya janga la virusi vya Corona na kuunda hali zinazofaa kwa utumiaji wa haki za raia na kisiasa na kwa ushiriki mkubwa wa watu wa Afrika ya Kati katika mchakato wa uchaguzi wa kidemokrasia.

31 July 2020, 10:58