Tafuta

Vatican News
2020.06.09: Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro huko Geneva 2020.06.09: Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro huko Geneva   (Gfuerst)

WCC:Kukataa kila aina ya ubaguzi ni ushuhuda wa kikristo

Baraza la Makanisa Ulimwenguni WCC wametoa wito wa nguvu wakiomba makanisa kuwa na uongofu na kukataa kila aina ya ubaguzi hasa kwa kutazama matukio yaliyotokea Marekani na katika kipindi cha janga la virusi vya corona.Baraza hili linawakabidhi kwa mara nyingine tena wakristo wote kazi ya kueneza zaidi upendo,uaminifu,matumaini na ujasiri.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kulaani vikali dhidi ya vurugu, ubaguzi wa rangi na upyaisho wa jitihada za Makanisa ya kikristo ulimwenguni ili kujibu kwa matumaini na mshikamano katika wakati huu wa mgogoro uliosababishwa na Janga la virusi vya corona ndizo mada msingi zilizojitokeza katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao hivi karibuni wa Tume tendaji ya  Baraza la Kiekumene la Makanisa Ulimwenguni (WCC). Ni kiungo thabiti cha mkutano wa kiekumene kati ya Makanisa zaidi ya 300 ya kikristo katika nchi 110 Ulimwenguni. Hata hivyo janga la virusi limelazimu kuahirisha Mkutano mkuu uliokuwa ufanyike 2021 katika mji wa Karlsruhe, Ujerumani kati ya mpaka wa Ufaransa na marekebisho kadhaa za mipango kutokana na athari za kifedha za afya ili uweze kufanyika kunako mwaka 2022.

Upendo,imani, matumaini na ujasiri

Vatican News ikihojiana na Fr. Lawrence Iwuamadi  Rais wa Taasisi ya Kiekumene ya Bose jijini Geneva kuhusiana na mantiki zilizokabiliwa na chombo hicho amesema wakati mgumu kama huu uliosababaisha na virusi vya corona Makanisa yanaalikwa kuwa na matumaini na ushuhuda wa imani. Katika mkutano wao uliohitimishwa tarehe 3 Juni 2020, Baraza la Makanisa Ulimwenguni walitangaza hata hati yao kuhusu nafasi ya Makanisa katika Muktadha wa janga, kwa kuipatia jina “upendo, imani, matumaini na ujasiri”. Baraza Makanisa Ulimwenguni limewageukia na kutoa wito kwa makanisa yote wanachama na wakristo wote “ili tuweza kuhudumia vema watu wa Mungu katika ulimwengu huu na katika kipindi hiki cha mgogoro wa kiafya na mabadiliko yake. Hata hivyo amebainisha pia ni kwa jinsi gani, virusi havitazami mipaka na wala kujali utajiri na hali halisi ya mtu aliyo nayo kutegemea na maisha, bali ni hatarishi hasa kwa watu waliohatarini zaidi kama vile maskini, makabila madogo, watu wa asilia, walemavu, wahamiaji, mlundikano ya ndani na ambapo kama  Kanisa kwa hakika linatakiwa lishuhudie kuwasindikiza watu na jumuiya zilizo hatarini zaidi.

Hali ya janga ifanye kutafakari zaidi

Baraza la Kiekuemene la Makanisa ulimwenguni (Wcc),limebainisha pia kwamba hali halisi iliyoundwa na janga ni fursa kutafakari kwa kina  kuhusu thamani msingi na kutafuta kupyaisha familia zetu, na jamii katika kujenga ile mitindo  iliyo bora ya jumuiya ya  haki na endelevu. Wito ni ule wa kupata ujasiri wa kukabiliana na janga na kuwa na maono zaidi,  lakini hasa kuendelea kuwa Kanisa la Kristo katika kipindi hiki kisichokuwa na ahakika kwa ajili ya wale ambao wanahitaji zaidi na kuepuka kutelekeza na ubaguzi ili kukumbatia kwa upendo ambao unaponya kama vile virusi, upendo ambao haujuhi mipaka na unaobomoa kila kila aina ya ukuta. Kwa masikitiko makubwa Baraza la makanisa Ulimwenguni  limebainisha baadhi ya maeneo yenye hofu na ukosefu wa uhakika ambao umeletwa na  janga hili kwa  kuongezea ardhi yenye rotuba kwa sehemu ambazo zilikuwa tayari zimeathiriwa. Kwa maana hiyo Makanisa yote ulimwenguni yaanalikwa kuungana kwa pamoja, kwa imani na ukweli dhidi ya sauti zinazohamasisha migawanyiko na shuku.

Ubaguzi nchini Marekani

Katika mkutano wao, vile vile hakusahau kile ambacho kinaendelea nchini Marekani hasa katika mapambano ya ubaguzi, ambapo Baraza la makanisa Ulimwenguni, limebanisha ni kwa jinsi gani  limekuwa daima linapambana dhidi ya ubaguzi wa rangi na kila aina ya ubaguzi. Tayari miaka ya “70-“80- na “90, mapambano hayo yalikuwa ni sehemu ya historia ya Baraza hilo kwa kila sehemu ulimwenguni. Kwa njia hiyo kile ambacho kimetokea Marekani, kinaonesha kweli sababu za kuendeleza jitihada zaidi za mapambano. Kwa mara nyingine tena   Baraza la makanisa ulimwengu limetangaza kwa uthabiti kwamba hali kama hii  lazima iishe na hitaji kubwa uongofu, tafakari, kutubu na kukataa kila aina ya ubaguzi wa rangi. Lazima kuwa na utambuzi wa kweli kuhusu  hadhi na thamani kutoka kwa Mungu kwa kila binadamu aliyeumbwa naye bila kujali rangi au kabila.

09 June 2020, 17:31