Tafuta

Zaidi ya nusu ya wakimbizi ulimwenguni ni watoto.Ni wakati sasa wa kutoa kipaumbele cha kibinadamu kusaidia watoto. Zaidi ya nusu ya wakimbizi ulimwenguni ni watoto.Ni wakati sasa wa kutoa kipaumbele cha kibinadamu kusaidia watoto. 

Uswiss:Wakristo na Wayahudi waungana katika kulinda watoto wakimbizi!

Zaidi ya nusu ya wakimbizi ulimwenguni ni watoto.Sehemu kubwa wanasafiri bila kuwa na wazazi wao au ndugu au labda wametengenishwa wakati wa kukimbia kwao.Ni kwa mujibu wa taarifa ya Jumuiya ya kiyahudi na Makanisa ya Kikristo nchini Uswiss huku wakiomba jitihada za kulinda watoto wakimbizi ziwe ni kipaumbele kwa jamii yote na sera za kisiasa.

Sr. Angella Rwezaula- Vatican

Jumuiya ya Kiyahudi pamoja na Makanisa ya Kikristo nchini Uswiss, imetoa wito wake katika matazamio ya kukumbuka Jumamamosi na Jumapili Siku ya wakimbizi Ulimwenguni. Katika ujumbe wao wa pamoja, wawakilishi wa kidini wananukuu katika kitabu cha Nabii Isaya kifungu kisemacho “mpatieni yatima haki yake” yaani jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mteteeni mjane. (Is, 1,17), ili kukumbusha kuwa zaidi ya nusu ya wakimbizi ulimwenguni ni watoto. Sehemu kubwa wanasafiri bila kuwa na wazazi wao au ndugu au labda wametengenishwa wakati wa kukimbia kwao.

Kwa mujibu wa shirika la watoto Unicef, asilimia 60 ya watoto hawa wanahitaji ya msaada wa kibinadamu, milioni 2 yao hawawezi kwenda shule na milioni 3,3 wako hatarini za mabomu. Licha ya kuwa  wao ni  wakati endelevu wa jumuiya ya kibinadamu na pamoja na kustahili kulindwa, watoto hao utafikri wanageuka kuwa kizazi potevu kwa sababu katika hali ya ukimbizi, wanapoteza kila aina ya ulinzi na kila ya matarajio. Badala yake  Viongozi hao kutoka kwa wakristo na wayahudi wanabainisha kuwa  watoto ni msingi pekee ambao kila kanda ya mgogoro leo hii inaweza kujengewa wao matumaini ya kesho yaliyo na amani na hadhi ya kibinadamu. Muktadha wa kuhangaikia watoto wadogo kwa hakika ndiyo kipaumbele na wanaotegemewa  kwa wakati ujao wa Nchi zao asilia.

Katika ujumbe wao pia viongozi hawa wamesema usimamizi wa watoto hawa ni kama misingi. Inatosha kufikiria wimbi linalofika la watoto wasiosindikizwa ambao kati ya mwaka 2017 na 2019 walifika Ulaya kupitia Bahari ya Meditrannean, na walisukumizwa kutoka Libia, waliwekwa magereza katika hali mbaya sana. Si hiyo tu lakini pia katika makambi ya wakimbizi na vituo vya mapokezi Ulaya, watoto wako katika hali ngumu ya dhuluma, vurugu na manyanyaso kwa upande wa watu wazima, aidha katika ukiritimba ambao hauna umakini wowote kwa ajili ya mahitaji yao.

Katika mtazamo huo, wakristo na wayahudi nchini Uswiss, wametoa wito kwa viongozi wa kisiasa na haki ili wajikite kutazama baadhi ya vipaumbele  kama vile “Ukaribishwaji wa kutosha kwa watoto katika vituo vya mapokezi; pasiwepo vizuizi kwa watoto wahamiaji ; habari kamili katika lugha na kwa kiwango cha watoto zihakikishwe; msaada wa mtu binafsi kwa watoto ambao hawajasindikizwa wa upande wa wahudumu wenye taalam; kuharakisha upatikanaji wa mafunzo na kuunganishwa tena katika familia . Watoto ni baraka kutoka kwa Mungu,  wito unahitimishwa na kwamba hatima yao ni matarajio ya wakati wetu endelevu na matarajio ya maisha yetu yanategemea matarajio  yao. Kati ya watia sahini wa ujumbe huo ni  Rais wa Baraza la Maaskofu  wa Uswiss, Askofu  Felix Gmür, makamu wa rais wa Kanisa la Kitaifa la  Kiinjili, Esther  Gaillard, na Rais wa Shirikisho la Uswiss la Jumuiya ya Kiyahudi, Herbert Baridi.

20 June 2020, 16:09