Tafuta

Vatican News
Ulaya:Licha ya wahamiaji kupitia mediterranean lakini kuna hata njia mpya ya hatari kwa mfano kupitia mito katika mipaka ya nje ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya ambayo lazima izingatiwe. Ulaya:Licha ya wahamiaji kupitia mediterranean lakini kuna hata njia mpya ya hatari kwa mfano kupitia mito katika mipaka ya nje ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya ambayo lazima izingatiwe.  (AFP or licensors)

Ulaya:Tukumbuke watu waliopoteza maisha yao wakati wanakuja Ulaya!

Licha ya kuwa katika kipindi hiki cha kupaa kwa Bwana na Pentekoste kilicho jaa matumaini na mwanga kwa ubinadamu wote,bado kuna njia za msalaba,mateso,mahangaiko na vifo vinaendelea kwa maelfu ya ndugu kaka na dada,katika mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya.Ni kwa mujibu wa ujumbe wa Baraza la Makanisa Ulaya na Tume ya Makanisa kwa ajili ya wahamiaji Ulaya.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Baraza la Makanisa Ulaya (Cec) na Tume ya Makanisa kwa ajili ya wahamiaji Ulaya(Ccme) wametoa wito wao katika matazamio ya Siku ya Wakimbizi Ulimwenguni, ambayo imefikia kilele chake tarehe 20 Juni 2020, kuwa  “tukumbuke watu waliopoteza maisha yao wakati wanakuja Ulaya”. Katika kipindi hiki cha kupaa kwa Bwana na Pentekoste, kilicho jaa matumaini, na mwanga kwa ubinadamu wote, viongozi hao katika ujumbe wao wanaonesha huzuni wa kina na wasiwasi kutokana na kwamba njia za msalaba, mateso, mahangaiko na vifo vinaendelea kwa maelfu ya ndugu kaka na dada, katika mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya.

Waathirika wengi katikati ya bahari

Kwa mujibu wa wito wao uliotiwa sahini na Katibu Mkuu wa Cec, Jørgen Skov Sørensen, na Katibu Mkuu wa Ccme, Torsten Moritz unasema “Kama makanisa na kama Wakristo, wito wetu ni kuwa mashuhuda na watumishi wa ufufuko na maisha mapya katika haki na amani kwa wote, bila kujali kabila, taifa au dini. Kwa maana hiyo, tunajua sisi ni sehemu ya umoja wa ulimwenguni na Wakristo ulimwenguni kote, tukikumbuka watu walioathirika katika maeneo yao na sababu za kuhamishwa kwao”. Aidha “Majanga mengi katika Kanda ya Meditrannean kwa bahati mbaya yanaendelea” wanasema viongozi hawa wawili wa kikristo huku wakikumbuka kuwa “kwa mujibu wa takwimu za Kimaifa kwa ajili ya wahamiaji UNHCR, wamenukuu karibia watu 1,300 ambao wamepoteza maisha yao mwaka 2019 wakati wa miezi mitata ya kwanza kwa mwaka 2020 wamepoteza maisha watu 200”. Wakati takwimu zimepungua kwa miaka ya mwisho lakini kuna ongezeka la vifo wanasisitiza Jørgen Skov Sørensen na Torsten Moritz, hasa katika njia mpya ya hatari, kwa mfano kupitia mito katika mipaka ya nje ya Jumuiya ya Umoja wa  Ulaya, ambayo inabaki bila kufikiriwa au kuangaliwa. Viongozi hawa kwa maana hiyo wanaelezea masikitiko yao hasa kiukweli kwamba boti kadhaa zilijikuta zinapata ugumu mwisho wa wiki ya Pasaka katikati mwa bahari ya Mediterranean.

Makanisa kuwa mstari wa mbele kusaidia manusura

Kwa sababu ya kuchelewesha kupelekwa msaada wa meli za uokoaji na Nchi kadhaa ya Kimediterania, inasadikika kwamba wengi wa wale waliokuwa kwenye boti hiyo ambayo ilikuwa hatarini walizama wakati huo huo  wa Pasaka. Na kwa kuongezea  katika kuenea kwa covid-19 kumesimamisha shughuli nyingi. Mbele ya janga hili, kuendelea kupoteza maisha mipakani mwa Ulaya, Makanisa wamejibu kwa kutoa mshikamano, lakini hata kutoa msaada wa usalama na kisheria kwa ajili ya kuingia wakimbizi na wahamaiaji.Katika nchi kadhaa za bara,zaidi ya hayo, Makanisa yamejitolea kukaribisha wale ambao wameokolewa baharini au kuhamishwa ili kufungua uhamasishaji wa kisiasa na kuruhusu kutenguliwa lakini pia kuunga mkono au kuzindua mipango ya kutafuta namna ya uokoaji. Hatimaye mapango wa usalama uliozinduliwa miaka michache iliyopita na Ccme ambao wajumbe wanatoka katika Makanisa kadhaa ya Waprotestanti na Waorthodox barani Ulaya  yamewezesha kurahisha mabadilishano kati ya makanisa kwa kufungu njia ziliyo salama.

20 June 2020, 15:16