Tafuta

Hali ni tete sana dhidi ya hatua ya Isreali kutangaza mpango wa kunyakua ardhi ya Wapalestina inayokaliwa na wapelestina ukingo wa Magharibi. Hali ni tete sana dhidi ya hatua ya Isreali kutangaza mpango wa kunyakua ardhi ya Wapalestina inayokaliwa na wapelestina ukingo wa Magharibi.  

Nchi Takatifu:Tamko jipya la Makanisa ya Kikristo WCC dhidi ya kunyakua ardhi ya Wapalestina!

Umetolewa Wito wa pamoja wa Baraza la Makanisa ya Kikristo ulimwengu Wcc dhidi ya hatua ya Isreali kutangaza mpango wa kunyakua ardhi ya Wapalestina inayokaliwa na walowezi katika ukingo wa Magharibi.Viongozi wanasema amani haiwezekani katu ikiwa inashurutishwa au kupatikana kwa njia za dhuluma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mpango wa Israeli wa kutaka kunyakua maeneo ya Palestina ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa na inawakilisha kizuizi kikubwa cha kufanikisha haki na amani kati ya Israeli na Palestina. Haya yamethibitishwa na tamko la pamoja lililosainiwa na Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WCC), Jumuiya ya Madhehebu ya marekebisho ulimwenguni, Muungano wa kiekumene  na Shirikisho Kilutheri  Ulimwengu ambapo katika  masaa machache  yaani tarehe Mosi Julai 2020 imeoneshwa na Benyamin Netanyahu kama tarehe ya kuanza Upanuzi wa enzi kuu kwa maana hiyo wanasasisha  tamko lao  kwa jamuiya  ya kimataifa ili kudhibiti tendo hili  ambalo pia linagawanya jamii ya Israeli.

Kwa mujibu wa  viongozi wa Makanisa ya Kikristo, tishio jipya la nyongeza linajumuisha na kuongeza kazi iliyopo ambayo kwa muda mrefu sana imekuwa ikihatarisha haki na hatma ya watu wa Palestina. Viongozi hao wanatambua kuwa shida hiyo ina mzizi mgumu wa kihistoria, lakini wanathibitisha kwamba matokeo ya vitendo vya umoja, usio kuwa na usawa na utumiaji wa nguvu na vurugu, badala ya mazungumzo na michakato wajua kuwa   amani haiwezekani katu ikiwa inashurutishwa au  kupatikana kwa njia za dhuluma.

Viongozi wa Kikristo kwa maana hiyo wanathibitisha jitihada zao  kwa ajili ya  amani ya kweli na ya kudumu katika Nchi Takatifu. Na ili kufikia lengo hilo Makanisa na mashirika ya kidini ulimwenguni  wanahimiza kuendelea kuonyesha mshikamano na msaada kwa kutambuliwa na kulinda haki za Wapalestina katika wilaya zilizochukuliwa, kuunga mkono mazungumzo kati ya Israeli na Palestina kwa ajili ya suluhisho ambalo liko katika mchakato huo  na sheria za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Matsifa na kuunga mkono kuwasaidia wale ambao ni Wakristo, Wayahudi wa Kiislam na watu wa imani nyingine wanaofanya kazi kwa ajili ya upatikanaji wa amani na maridhiano. Hatimaye wito wao wanaomba Jumuiya ya Kimataifa  kuingili kati suala hili ili kumaliza suala hili la eneo la   Israeli tangu mwaka 1967, kizuizi cha Ukanda wa Gaza na hatimaye kupinga mipango na kusukuma Israeli kuheshimu majukumu yake ya kimataifa kama nguvu ya kutawala.

Ukanda wa Gaza ni eneo la pwani la Palestina linalokumbwa na migogoro ya mara kwa mara kati ya vuguvugu linalotawala la Hamas na jeshi la Israeli. Gaza inaitegemea Israeli kwa huduma za umeme, maji na mawasiliano. Jumapili makundi ya kupinga mpango wa Israeli wa kutaka kunyakua kwa nguvu maeneo ya Wapalestina katika ukingo wa Magharibi wameandaa vipeperushi kwa pamoja na makundi ya kiislamu na makundi ya wanamgambo walioko Gaza kwa kutoa wito ili kushiriki kwenye tukio litakalohudhuriwa na makundi yote ya Palestina pamoja na viongozi wa kisiasa  katika ukanda wa Gaza Julai mosi 2020. Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na serikali yake ya mseto na aliyekuwa mpinzani wake Benny Gantz anatarajiwa huenda akawasilisha mbele ya bunge na baraza lake la mawaziri, pendekezo la kunyakuliwa kwa ardhi hiyo ya Wapalestina wanayoikalia tangu mwaka 1967 baada ya vita vya siku sita. 

30 June 2020, 16:02