Tafuta

2020.04.16 Chiesa di Nangololo dopo l'attacco 2020.04.16 Chiesa di Nangololo dopo l'attacco 

MSUMBIJI:uharibifu wa makanisa na makazi ni mwingi huko Cabo Delgado

Kwa mujibu wa Askofu Luiz Fernando Lisboa, wa jimbo la Pemba amebainisha juu ya hatari inayokabili watu wa Cabo Delgado Kaskazini mwa Msumbiji kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya waasi wa ndani na nje ya nchi hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Uchungu na uharibifu ndivyo watu wanavyoviishi huko Cabo Delgado, Kaskazini mwa Msumbiji, kutokana na migogoro iliyoibuka kunako mwaka 2017. Hayo yamesema na Askofu Luiz Fernando Lisboa, wa jimbo la Pemba nchini humo wakati wa kuhojiwa na Tume ya Maaskofu kwa ajili ya Uchungaji kimisionari na Ushirikiano wa Makanisa ya kiaskofu nchini Brazili. Ni miaka mitatu sasa katika mkoa wa Cabo Delgado ambao umekuwa uwanja la  tukio la kushambuliwa na wanamgambo wa kiislamu kutoka nchi jirani au waasi wa ndani ambao wamesababisha maelfu ya waathiriwa na zaidi ya watu 200,000 kurundikana ndani. Kuhusu kipeo hicho kilikuwa  tayari kipo katikati ya ujumbe wa Papa Francisko wa “Urbi et Orbi” aliotangaza tarehe 12 Aprili 2020 siku ya Dominika ya Pasaka kwamba “Mgogoro ambao tunakabiliana nao usitufanye tusahahu hata dharura nyingine ambazo zinepelekea mateso kwa watu wengi. Bwana wa maisha ajionesha ukaribu  wake kwa watu wa Asia na  Afrika ambao wanaishi  kipeo kigumu cha kibinadamu kama vile Mkoa wa Cabo Delgado, Kaskazini mwa Msumbiji”.

Kwa mujibu wa Askofu Lisboa amesema “ huo ni wito muhimu ambao ulikuwa umeangazia tafakari juu ya Nchi ambayo inazidi kuteseka kwa sheria ya ukimya. Papa aliweza kuweka  juu ya ramani ya ulimwengi  hata mgogoro wa Wilaya ya Cabo Delgado na kwa maana hiyo ujumbe huo umetusaidia sana. Serikali kwasasa imeweza kuchukua hatua ya kuweka nguvu ya usalama katika kuthibiti wanamgambo hao”. Katika mahojiano yake Askofu wa Pemba kadhalika anasimulia matukio mengi ambayowanateska sana kama vile mauaji, uchomwaji wa nyumba, mashambulizi ambayo yametokea katika barabara, vyombo vya usafiri na vijiji kuharibiwa. “Watu wanaishi katika hali ya hofu ya kutisha” amesema askofu na kwamba kwa sababu ya kuwa na  mlundikano  wa ndani, makazi yanajaa watu kuanzia 15, 20, 25 na katika kipindi hiki cha janga la covid-19 ni vigumu kufuata sheria zilizowekwa za kijamii”.

Kwa yule ambaye hakuweza kuacha kijiji chake, amebainisha Askofu , anaishia kukaa kwenye vichaka kwa hofu ya migogoro hiyo. Na kwa yote hayo bado inaishia kuzidisha hali kuwa ngumu kwani “watu kwa kawaida ni masikini na sasa kile kidogo ambacho walikuwa nacho kimeharibiwa kutokana na ghasia hizo” Askofu amebainisha. Ni muhimu zaidi hasa katika nafasi ya Caritas mahalia, ambayo imeweza kuingilia kati katika Mkoa, hata nyakati zilizopita kwa kupeleka msaada wa watu ambao walikumbwa na kimbunga cha Kenneth , ambacho kimeacha maafa makubwa sana. “Hatuna chakula cha kutosha kwa sababu hakuna aliyekuwa na uwezo wa kutoka nje na kupanda lolote hivyo mwaka huu ni kuendelea kuteseka na njaa na tunahitaji ushirikiano wa wote” amesema Askofu wa Pemba.

Askofu Lisboa katika mahojiano hayo kadhaika ameeleza kuwa Kanisa mahalia daima limekuwa likizingumzia juu ya matatizo haya na kutangaza huku wakiomba msaada. Lakini ni baada ya tamko kutoka kwa Papa, na kwamba ilikuwa kama kupasua ukimya hata kwa ngazi ya kimataifa. Askofu Lisboa ametoa wito wa sala na kwamba  “ sala ni njia muhimu na ya kweli  kuweza  kutusaidia kusali kwa ajili yetu, kwa ajili ya watu wetu kwa sababu, sala ina nguvu sana na tunahitaji umoja wa kaka na dada! “Sisi ni Kanisa moja ambalo tunatakiwa kusali kwa ajili ya mmoja na mwingine. Kila mbatizwa anaweza kupeleka utimilifu wa utume wake katika familia, kazini, shuleni na katika ndani ya jumuiya nzima”, amehitimisha Askofu Lisboa.

03 June 2020, 15:12