Tafuta

Maandamo makali kila pande za dunia kufuatia na kifo cha George Floyd huko Minneapolis nchini Marekani Maandamo makali kila pande za dunia kufuatia na kifo cha George Floyd huko Minneapolis nchini Marekani 

MAREKANI-Kifo cha Floyd:Askofu Mkuu Gomezi:uvumilivu wa ubaguzi umekuwa wa muda mrefu!

Kufuatia na kuuwa kwa George Floyd huko Minneapolis,Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani analaani kitendo na kwamba ubaguzi huo umekuwa wa kuvumiliwa kwa kipindi kirefu katika jamii ya Marekani.Uuaji wa kikatili na usio na busara ni dhambi ambayo inatakiwa haki mbinguni.

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Rais wa Baraza la Maaskofu Nchini Marekani Askofu  Mkuu José H. Gomez, anaungana na wote walioshikwa hasira katika siku za hivi karibuni na marais wa tume saba za Baraza la Maaskofu wa Marekani (Usccb) kufuatia mauaji ya George Floyd, mwenye umri wa miaka 46, Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyeuawa huko Minneapolis na afisa wa polisi, na wakati huo huo maandamano hayaachi nchini  humo na ulimwenguni kwa kile kilichotokea.

“Uuaji wa kikatili na usio na busara, ni dhambi ambayo inaita haki mbinguni. Ninasali kwa ajili ya George Floyd na wapendwa wake na kwa niaba ya Maaskofu, ninashiriki hasira ya jumuiya ya kiafrika na kwa wale ambao wako karibu huko Minneapolis na kwa nchi yote”, amethibitisha Askofu Mkuu wa Los Angeles katika barua yake illiyosambazwa Jumapili, tarehe 31 Mei 2020.

Pamoja na Baraza zima Askofu Mkuu Gomez ameomba kuwa mamlaka ya raia iweze kufanya uchunguzi ambao unahakikisha haki na uwajibikaji, na kwa kuwa na uelewa wa kufadhaika na hasira ya “Wamarekani wenye asili ya Kiafrika ambao bado wanateseka kwa kunyenyekeshwa, kutendewa vibaya na kwa kudhauriwa hadhi yao na ubaguzi kwa sababu ya kabila na rangi ya ngozi yao”.

“Ubaguzi umevumiliwa kwa muda mrefu sana (...). Lazima twende kwenye mzizi wa ukosefu wa haki ambao bado unaambukiza maeneo mengi ya jamii ya Marekani”, amesisitiza kwa nguvu Askofu Mkuu huku akionya kwamba vurugu ambazo zimeshuhudiwa katika siku hizi hazipeleki mahali popote zaidi ya “kujidhuru”.

Kwa kufuatia na hilo ndipo ametoa wito wa kuandamana kwa amani: “Hatupaswi kuruhusu kusema kwamba George Floyd amekufa bure. Lazima tuheshimu sadaka ya dhabihu yake kwa kuondoa ubaguzi wa rangi na chuki kutoka mioyoni mwetu na kupyaisha dhamiri yetu ya kutimiza ahadi takatifu ya taifa letu na kuwa jamuiya ambayo inahakikisha maisha, uhuru na usawa kwa wote, amehitimisha Askofu Mkuu Gomez .

Uchunguzi wa madaktari umebaini kifo cha George Floyd kuwa ni mauaji. Wakati huo huo, mvutano unabaki kuwa mwingi nchini humo kwa kwa njia ya maandamano makali. Familia ya Floyd kabla ya hapo ilipokea ripoti ya uchunguzi wa kifo chake na kuonesha kuwa alifariki kutokana na kukosa hewa. Uchunguzi huo unakinzana na maelezo rasmi ya serikali kuwa alifariki kutokana na matatizo mengine ya moyo aliyokuwa nayo.

Kifo cha Floyd, Mmarekani mwenye asili ya Afrika, kilichosababishwa na afisa wa polisi mzungu kimezua wimbi la maandamano na ghasia katika miji mbali mbali ya Marekani. Rais Donald Trump ameapa kuweka wanajeshi kadhaa wenye silaha  ili kuzima machafuko hayo. Amri ya kutotembea usiku imewekwa katika miji mingi nchini Marekani. Maafisa mjini New York wamechukua hatua kama hiyo, kuweka amri ya kutotembea usiku ambayo itaanza saa 5 ya usiku na kumalizika saa 11 asubuhi kwa saa za Marekani. Usikilizaji wa awali kwenye mahakama wa afisa huyo wa zamani Derek Chauvin, aliyekamatwa siku ya Ijumaa iliyopita kwa mauaji hayo, imehahirishwa hadi tarehe 8 Juni.

02 June 2020, 11:35