Tafuta

Vatican News
Marekani: Amani inapatikana tu kwa kutenda kazi kwa ajili ya haki Marekani: Amani inapatikana tu kwa kutenda kazi kwa ajili ya haki  

Marekani:Ikiwa unataka amani fanya kazi kwa ajili ya haki!

Marais wa Tume ya Haki,amani na mandeleo fungamani,Tume ya wahamiaji na Tume ya kupinga ubaguzi wa rangi ya Baraza la Maaskofu Katoliki,Marekani (USCCB)wametuma barua kwa wanachama wote wa Bunge la Marekani kwa tafakarijuu ya uwajibikaji wa polisi na mageuzi yanayotakiwa kufuatia na kifo cha G.Floyd,Rayshard Brooks na wengine wengi.Ni lazima kuondoa mifano ya ubaguzi na hukumu ili utekelezaji wa kweli uthibitishwe kabla ya maisha mengine kupotea.

Na Sr. Angela Rwezaula  Vatican

Kufuatia matukio mabaya ya hivi karibuni ambayo yalisababisha kifo cha Floyd na kuwekwa  mahabusu polisi na majadiliano ya kitaifa juu ya marekebisho ya polisi na haki za kikabila, nchini Marekani, Maaskofu wa Tume ya maaskofu kuhusiana na masuala haya kwa namna ya pekee  mada hii kuu ambayo imetikisa  mkubwa ulimwengini, hivi karibuni wametuma barua kwa wanachama wote wa Bunge la Marekani kwa kutoa tafakari na kanuni juu ya uwajibikaji wa polisi na mageuzi. Barua hiyo imetiwa sahini na Askofu Muu Paul S. Coakley wa mji wa Oklahoma, ambaye ni Rais wa Tume ya Haki na mandeleo fungamani ya binadamu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani (USCCB); Askofu  Mario E. Dorsonville, Msaidizi wa Jimbo Kuu la Washington, Rais wa Tume kwa ajili ya wahamiaji na Askofu  Shelton J. Fabre wa  Houma-Thibodaux, Rais wa Tume ya kupinga ubaguzi wa rangi.

Katika barua ya maaskofu  wanabainisha kuwa ingawa maafisa wa utekelezaji wa sheria hutoa huduma ili bora na muhimu  lakini  mauaji ya kutisha na yasiyofaa ya George Floyd, Rayshard Brooks na wengineo wengi  yameonyesha kuwa lazima kuwe na mazoezi yaliyo muhimu ya mafunzo na uwajibikaji wa polisi, na kwa uhakika katika kurekebisha utumiaji wa nguvu iliyo mbaya, lakini pia hata katika kuondoa mifano ya ubaguzi na hukumu ili uwajibikaji wa kweli uweze kuthibitishwa kabla ya maisha mengine kupotea.

Maaskofu hawa katika barua yao inaonesha hata barua nyingine ya kichungaji juu ukiukwaji wa haki na juu ya ubaguzi wa umma uliojionesha katika mchakato wa maisha ya kihistoria nchini humo na zaidi kuangazwa na maoni ya Papa Francisko kuhusu kifo cha George Floyd, vile vile hotuba kuhusu matumizi mabaya ya nguvu kwa upande wa polisi na kutazama juu ya jukumu la polisi katika jamii kwa mtazamo wa  ushauri wa Papa mstaafu Benedikto XVI na   Papa  Mtakatifu Yohane Paulo II.

Maaskofu  hao wanasisitiza kuwa “tunahifadhi kwa muda refu utamaduni wa Mtakatifu Agostino, Mtakatifu Tomasi wa Aquino, na mchungaji Dk. Martin Luther King ambaye anasema kwamba “kusudi la sheria na utekelezaji wa sheria ni kukuza haki” . Kwa maana hiyo wanaongeza kusisitiza kuwa “Suluhisho moja la changamoto za wakati huu ni kufuata ushauri wa busara wa Papa Mtakatifu Paulo VI aliyesema kuwa 'Ikiwa unataka amani, fanya kazi kwa ajili ya haki”

30 June 2020, 11:33